Hamadi Rashid wa aliekuwa CUF

Babamu

Member
Dec 15, 2011
10
1
Amani juu yenu.Jamani mimi nahitaji kueleweshwa zaidi kwani haya mambo ya siasa sina ujuzi nayo. Huyu Hamadi Rashid wa aliekuwa Mbunge wa Kavu baada ya kuvuliwa GAMBA na CUF wenzake, nimeonasehemu ya kuwa anataka kuunda chama cha kwake sasa huu sio UROHO ama UCHU wa madaraka? Nielewesheni wajuzi wa mambo ya siasa ya hapa kwetu TZ.
 
unadhani wajua, lakini una hofu kuwa hujui, waulizaje kundule mbwa hali ya kuwa umeushika mkia????????!!!!!!!!!
 
Basi kama hata habari za hamad rashid huzijui sasa kwenye siasa we unafanya nn? kwani unaonekana mzembe sana so mayb uimbe taarabu kama komba wa ccm ndo itakufaa.
 
Nitatumia busara kidogo walau nikujibu maana sijaona jibu kwenye posts zilizotangulia hapo juu. Kwanza kwenye siasa, mwanasiasa yeyote anataka kile ambacho anakifikiria kiweze ku "influence the political situation in the country or in the party". Sasa kama Hamadi Rashidi hakuweza kutimiza hiyo haja ndani ya CUF anayo haki ya kuanzisha chama kingine cha siasa ili aweze kupitisha mawazo yake ya kile anachoona ni cha maendeleo kwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla. Kwa hiyo sioni kwamba kama Hamadi Rashidi akiamua kuanzisha chama chake itakuwa ni UROHO wa madaraka. La hasha hii ndio maana ya DEMOCRACY kwamba kila mtu ana uhuru wa kuanzisha chama na vile vile kutengeneza platform ambayo ataitumia kuwakilisha mawazo yake. Tumwach Hamadi Rashidi atekeleze azma yake ya kuanzisha chama na huwezi jua kwamba chama hicho kinaweza kuwa njia madhubuti kuelekea kwenye ukombozi wa mtanzania kwani kwa sasa sioni kama CUF inaweza kweli kuja na ideas ambazo zitakuwa kinyume na CCM hasa kwa Zanzibar baada ya ndoa iliyofungwa kati ya CCM na CUF.
 
Back
Top Bottom