Hamadi Rashid afunguka; adai Mtatiro, hajarejesha 'chenji' ya helikopta!

Shida walifikiri kutumia muda mwingi kuishambulia chadema ndio kufanya siasa wakasahau majukumu ya kujenga chama chao sasa dhambi yao imewarudia na wanaanza kuumbuana wenyewe kwa wenyewe.
 
Great Thinkers kweli wamo humu ndani!!! Mada inaachwa na kukimbilia hoja taka na kupakazana matope. kama Mtatiro hajarudisha chenji ya helikopta basi ni mwizi tu, kama vile magamba. Cha msingi ni kumuomba HR atoe ushahidi kama anao!


Nadhani stori hii kuhusu ufisadi wa helikopta yaja wiki ijayo full kabisa ktk gazeti moja la Jumatano! Just wait!!!! Patachimbika1

Kwa mara ya kwanza sakata hili lilipotiwa na Mwanahalisi, hivyo basi ni matumaini yangu na kwa namna ninavyomfahamu Saed Kubenea, Mwanahalisi la Jumatano ijayo litakuwa balaa, litawaacha watu uchi na bila kumsahau huyu Mujahidina mwenye jina la Kigalatia, Julius Mtatiro.
 
Hatimae CCM imewaweza CUF. Watageukana sana na mvuto unazidi kulegea. Uzuri ni wao kwa wao wanaumana na wanataka kwenda mpaka jimboni kwa Hamad Rashid. Tatizo langu ni gharama za serikali kurudia tena uchaguzi wakati hosipitali hazina vifaa wala dawa
 
Great Thinkers kweli wamo humu ndani!!! Mada inaachwa na kukimbilia hoja taka na kupakazana matope. kama Mtatiro hajarudisha chenji ya helikopta basi ni mwizi tu, kama vile magamba. Cha msingi ni kumuomba HR atoe ushahidi kama anao!

Nadhani stori hii kuhusu ufisadi wa helikopta yaja wiki ijayo full kabisa ktk gazeti moja la Jumatano! Just wait!!!! Patachimbika1
Umejuaje ndugu yangu kama hii stori kama itatoka kwenye gazeti wiki ijayo?
 
HR vipi kuhusu matumizi ya 100m za kambi ya upinzani ktk bunge lililopita, maana mpk leo hii hujajibu mapigo
 
Hamadi Rashidi akiwa anafunguka kupitia kipindi cha Baragumu cha chanel 10 anamesema kuna maswala ya msingi ya kuhoji kwenye chama, sio kuhoji haki ya mtu kutangaza nia.
"Mambo ya msingi ni kuhoji kwa nini chama kinapoteza mvuto, mtatiro alikodi helkopta change hajarudisha, ukihoji haya unaonekana una matatizo"

mtatiro rudisha change ya helkopta.

Shilingi ngapi?
 
Cuf imepoteza mvuto kwa sababu ya HR. alipokuwa KUB alishindwa kuongoza hasa chama chake kiongolee maswala ya msingi na kuuacha mwanya huo utumiwe peke yake na CDM.
wabunge wa CUF wakawa wanaongea pumba huku CDM wakiongea dhahabu jambo ambalo HR alikuwa anaweza kuwakumbusha wabunge wake nini hasa cha kuongelea bungeni.
Wabunge wenyewe wa kukumbushwa wako wapi hawa hawa vilaza wa Pemba, HR kinachomsumbua ni uroho wa madaraka na misifa ya kukutana na kina Pinda nafikiri na elimu pia hata kama kasoma hajaelimika.
 
Viongozi wetu wapo kama miungu watu hawatakiwi kupewa changamoto,akitokea mtu kuonesha nia ya kugombea uongozi cheo chake tu,ni mchochezi sasa nn maana ya democracy?na nn maana ya uchaguzi upite bila kupingwa?leo tunayaona cuf na itapotokea mtu kuonesha nia ya kugombea uenyekiti tutayaona cdm na hata nccr hata ccm wanataka kuka madarakani bila kupingwa sasa democracia tunayohihubiri maana yake nn,mbadilike watanzania wasasa sio wale wa wakati wa vidumu fikra za mwenyekiti
Ubinafsi unatuumiza sana mkuu... watu dnani ya hivi vyama, hasa wale walio katika mafasi za juu za uongozi si progressive
 
Mimi sidhani kama anayopigania Ahmad Rashid yanatoka moyoni mwake bali nahisi ni tamaa tu ya madaraka kwani baada ya kufikiria kuwa angekuwa kiongozi wa upinzani bungeni anufaike na mafao akakosa, akabuni njia ingine ya kuanzisha kambi isiyo rasmi ya upinzani, ikashindikana, sasa anataka maalim achague moja kuacha ukatibu mkuu achukue yeye kwa manufaa yake ili aweze kujitengenezea mazingira ya kujiweka kuwa mgombea uraisi zanzibar kwa CUF na hatimaye kuwa makamu wa kwanza
 
Halafu mbona anasema kijujuu tu kuwa hajarudisha si aseme kila kitu kama ana ushahidi wa uhakika vinginevyo naona haya ni malumbano ya maji taka either mmoja wapo alikosa nafasi fulani muhimu kwenye chama sasa anataka kuvuruga wenzake
 
Kweli lakini kumbuka na pemba kua aina tatu ya wapemba'
I - Wapemba wenyewe
2- Wapemba unguja
3- Wapemba bara.
Sasa hapo ndo tatizo linapoanzia nina wa kuwasemea wapemba ,Je ni Mtatiro.?

Mimi kinachonishangaza ndani ya CUf yani uchaguzi ukishamalizika Mwenyekiti wao huwa anasepa zake nje ya nchi hadi uchaguzi mwingine sasa ni nani atakayekijenga chama? Kabla ya maridhiano Maalim Seif ndo alikua akihangaika kujenga chama sasa keshapewa kahawa ya bure na Tende za ikulu amekaa kimya kamuachia mtatiro chama bila kujua kua Mtatiro ni mtu kuropoka and then anakuja kufikiria alichonena wakati kishaleta impact kwa jamii...
 
Mimi kinachonishangaza ndani ya CUf yani uchaguzi ukishamalizika Mwenyekiti wao huwa anasepa zake nje ya nchi hadi uchaguzi mwingine sasa ni nani atakayekijenga chama? Kabla ya maridhiano Maalim Seif ndo alikua akihangaika kujenga chama sasa keshapewa kahawa ya bure na Tende za ikulu amekaa kimya kamuachia mtatiro chama bila kujua kua Mtatiro ni mtu kuropoka and then anakuja kufikiria alichonena wakati kishaleta impact kwa jamii...
Ulidhani Lipumba ni mwanasiasa, Lipumba ni mmoja wa wanasiasa watakaohukumiwa na historia kwa kuchelewesha na kudumaza demokrasia nchini kwa kuwapumbaza wananchi kuwa anapigania haki kwa kugawa kura za wapinzani kwa miongo mitatu.
 
CUF walijisahau sana na huo ubwabwa waliopewa na CCM, sasa CCM hao hao wanawamaliza!
hamad na Seif si brothers hawa? sasa ni nini kiko hapa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom