HAMADI ni mtaji tosha kwa CHADEMA

Taarifa nilizonazo kutoka vyanzo vya ukweli ikiwemo mzee mmoja wa WAWI ni kwamba huyu jamaa hakubaliki kule kwa sasa hasa kwa hizi harakati zake za kumpinga Maalim, kwani inasemekana kama kweli anakubalika ungekuta kaanzia wawi then huku bara lakini swala ni kwa nini anafanyia harakati zake magomeni na Manzese?

Kingine ili CDM kishike madaraka focus yake si Zenji ni kwenye watu wengi, kwani propaganda za CCM hazitoki kwenye vichwa vya baadhi ya waTZ including waZenj.

Kwa hiyo hatuhitaji watu wa kutimuliwa kama HR au Kafulila watakuwa kamaa Shibuda tu......, wakaanzishe chama chao ili wagombanie madaraka wenyewe kwa wenyewe.
Wala msije danganyika kabisa kwamba rashid Hamad hana nguvu Zanzibar..Ana nguvu kubwa na ifahamike tu kwamba sababu yake kufanya kambi bara ni kwa sababu CUF inakufa bara na ndipo anapotakiwa kuwasikiliza wananchi na kuwakilisha mawazo yao ambayo viongozi kama Seif hakubaliani nao.. Seif Sharrif kaua kweli nguvu ya CUF bara kwa sababu yeye kama Seif anajua hana lake Bara isipokuwa visiwani na ndio maana akaibadilisha CUF kuwa chama kinachotetea zaidi maslahi ya Wazanzibar.

Rashid yeye anaitazama picha kwa mapana zaidi na ndio ugonvi uliopo..Rashid hana sababu ya kwenda wawi wakati chama kinakubalika huko ila anakwenda sehemu ambazo zina matatizo kazi ambayo Seif.S. Hamad alitakiwa kuifanya. yeye sii ndiye katibu wa chama mbona haondoki Ikulu badala ya kushughulikia maswala ya chama?

Ukitazama Chadema kweli hawana nguvu Zanzibar kama CCM au CUF na wameshindwa kupenyeza kutokana na dhana ile ilokuwepo zamani kwamba CCM ni chama cha wakristu sasa hivi kimebatizwa Chadema. Inahitaji mtandano mkali sana na wa ajabu kuweza kupenyeza Zanzibar na bahati mbaya Chadema nayo sasa hivi inaelekea kupendwa zaidi na wakristu baada ya kupandikizwa Udini, watu wamefuata kweli kujiunga ama kutojiunga kwa dhana hizo - MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO..
 
MKANDARA umeongea UKWELI kabisa..lazima cdm ikubali kwamba inahitaji breakthrough zanzibar na maeneo ya pwani ili kujijingea sura ya kitaifa zaidi na zenji si eneo la kubeza hata kidogo.
 
mkuu hata mimi nakuunga mkono,kwani point kuu, ni kitu gani kinachosababisha hawa wazenji wagombane? Mimi binafsi naona kuna mgawo haukugawiwa kwa ufanis.
 
unaweza kushinda uchaguzi wowote na kukabidhiwa dola bila hata kupata kura moja zanzibar na pemba- jimbo la ubungo pekee ni sawa na pemba yote!! kwa hiyo sioni hoja unless huyo Hamad aje tu kwa hiari yake mwenyewe lakini si kwa hoja ya kuwa mtaji wa CDM 2015. unless wafanye marekebisho mengine ndani ya katiba kwamba chama kinachounda dola lazima kipate kura nusu au zaidi toka zanzibar na pemba. CDM kwa sasa haihitaji mtaji wa mwanasiasa yeyote toka vyama vingine kwani yenyewe ndiyo mitaji kwa hawa wanasiasa ambao wana matatizo kwenye vyama vyao wanaweza kuja kama wanataka.
Chama kinategemea vyuma chakavu!!!? Tafakari
 
ndio mkuu MONONGO hoja ya msingi hapa ni kuwa maalimu seif anashindwa kutimiza majukumu yake ya chama ipasavyo na perfomance ya cuf inaporomoka sana..igunga ni standing evidence na hoja ya msingi kabisa..ikiwa HR atafukuzwa cuf kwa hoja hiyo basi atakua hana kosa na historia itamtetea.
 
unaweza kushinda uchaguzi wowote na kukabidhiwa dola bila hata kupata kura moja zanzibar na pemba- jimbo la ubungo pekee ni sawa na pemba yote!! kwa hiyo sioni hoja unless huyo Hamad aje tu kwa hiari yake mwenyewe lakini si kwa hoja ya kuwa mtaji wa CDM 2015. unless wafanye marekebisho mengine ndani ya katiba kwamba chama kinachounda dola lazima kipate kura nusu au zaidi toka zanzibar na pemba.

CDM kwa sasa haihitaji mtaji wa mwanasiasa yeyote toka vyama vingine kwani yenyewe ndiyo mitaji kwa hawa wanasiasa ambao wana matatizo kwenye vyama vyao wanaweza kuja kama wanataka.

Absolutely right!!
Nakuunga mkono!
 
Aisee mbona hii kweli inaleta mantiki!!! Tumwombe Mungu ili hasma ya CUF kufukuza huyu jamaa itimye. Kama hii itatimia basi CDM kitakuwa kitatumia hizi halfside tricky kuwauwa mafisadi kuanzia bara hadi visiwani. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibaariki Cdm kishinde 2015!!!

Hapo kwenye red na wino uliokorezwa. Hivi Hamad ni msafi kiasi cha kutyumika kama zana ya kuwangoa mafisadi?
 
Mbona watu walioshindikana kwenye vyama vyao ndio mnataka wajiunge na chadema? e.g Kafulila, Hamad etc
Kila mbunge analeta kiasi fulani cha ruzuku katika chama. More MPs more financial stability ya vyama kuwafikia watu wengi vijijini. Shibuda yupo CDM hadi leo for only one reason financial na uwiano wa kuhalalisha kambi rasmi bungeni. So sioni shida kuwapata na kina Hamad etc. Ni wabunge wataongeza ruzuku! Wapo wengi tu mbona kina Selasini etc. We keep very close monitoting kwa hao watu and hatuna haja ya kupambana nao. Pia uanachama uko wazi kwa yeyote anayetaka kujiunga na CDM
 
ikiwa tetesi zinazoendelea za cuf kumvua gamba mbunge wake wa jimbo la wawi zitakuwa kweli, bila shaka CDM kitakua na nafasi adhimu kujijenga visiwani iwapo watamshawishi mbunge huyo kujiunga na chama hicho.HII ni kwa sababu Cdm haina kamanda wa uhakika ambaye ana uzoevu mkubwa wa siaza za zenji...pia Cdm kinaweza kumpendekeza awe mgombea mwenza wa dr slaa 2015 kuliko kumpendekeza mtu ambaye hana historia inayofahamika kama ilivyokua 2010 ... hii itazidi kuongeza kura za uraisi kwa Cdm..

Mh!Katika hili CHADEMA kuweni makini!
Akili za kuambiwa changanyeni na za kwenu!!!!!!
Kumbukeni ule msemo,"adui mwombee njaa!"
Msijeongeza ma-Shibuda mengine,ohoooooooooo!!!
 
Kwani CDM si wana yule aliyekuwa mgombea mwenza wa Dr Slaa ambaye sijui amesoma mpaka darasa la saba.Hivi kwanza siku hizi yuko wapi yule?sini mzenji yule?kwanini wasimtumie yule?Au kama vp wampe uenyekiti wa chama Taifa hapo watawapata wazenji lakini sijui bara itakuwaje tena?
 
Back
Top Bottom