Hamad Rashid vs Freeman Mbowe=mt kilimanjaro vs kichuguu

Ni kweli, Hamad Rashid aling'ara sana na kumfunika Mbowe kwa mbali sana. Tatizo Mbowe alikuwa akiegemea katiaka uzushi unaopatikana katika MWANAHALISI na JF. Kuiita CUF kuwa na kibaraka, si sahihi. Tatizo lenu mkishindwa uwanjani ndani ya dakika 90 mnaanza kejeli na mzaha

Usitumie kichwa kubebea masikio.
mbowe kama kiongozi wa Chadema ameweza kukifanya chama kuwa imara na kupata idadi zaidi ya wabunge na kuwapoka CUF hata uongozi wa upinzani Bungeni.

Sasa CUF mmefanikiwa kupata nini zaidi ya kuolewa na CCM na huyo mwali wenu kuwa Mama wa nyumbani asiye na kazi yoyote zaidi ya kusubiri kuonja ftari mwezi wa Ramadan?

Nyie upinzani umewashinda tulizeni viuno chini.
 
Ama kweli kupend kubaya.Inavyoelekea hata Mbowe angetoa ushuzi wana cdm mtashangilia!!!!!!!!!!!!!

Can we at least behave like real thinker? People, the whole thing was about the one side(upinzani) that seem to give tanzanian hope. Sasa naona wapinzani wenyewe kwa wenyewe mnaanza kupishana kweli are we going to make it? Alafu i dont think hapa JF ni pahala pa mizaha, we are respected so let's respect ourselves. Toa hoja na sio mizaha!
 
Jamani kitu kimoja kikubwa kwa binadamu. kila mtu ana mawazo yake tofauti na mwingine. kila mtu huchukulia au huelewa tofauti na mwingine japo wanaweza kuwa wameangalha ama kuona tukio moja. FREEMAN alikuwa vizuri kwa upande wangu.
 
mie naona kuna wanasiasa hawajui wala kutafuta kujua vipaumbele vya taifa kwa sasa.
haiwezekani kukawa na pande tatu zinazopingana bungeni. lazima kuweka maslahi ya nchi kwanza na ya siyo ya chama. kama mwaka huu nafasi hazikutosha msitake kujikweza kwa kuanzisha vurugu ili kufanya masuala ya uongozi kuwa in chaos.
Hamad anataja fedha milion 100 sijui 200, ni dhana hiyo inayomsukuma kujaribu kuunda kambi ndogo ya upinzani ili wachote fedha za umma. acheni uhuni jamani
ujumbe huu uwafikie CUF na vyama vyenzake vinavyounda kambi ndogo ya upinzani.
 
Mleta maada amepunguza hadhi ya JF kwa kuleta mada kishabiki zaidi kuliko kutumia akili ya kujenga hoja. Anasema tu kuwa Hamad alikuwa Kilimanjaro na Mbowe kichuguu bila hata ya kueleza hata jambo moja linalounga jumuisho lake. Watu kama hawa wanatupotezea muda, na hapa siyo mahali pao, mahali panapowafaa ni kwenye vikao vya kahawa. Hapa leta hoja ambayo inaweza kujadiliwa kwa kuzingatia vigezo vilivyotumika ili wachangiaji waweze kuafiki au kupinga kwa kuangalia vigezo ulivyotumia na usahihi wake.

Poor Dos.
 
Tuangalie kwa mtazamo wa taifa zaidi,chadema imejikita bara na imespread maeneo tofauti imepata wabunge huku ccm ikichukua sehemu kubwa zaidi,CUF ZNZ tena Pemba tu,ccm Unguja.sasa nafikiri CUF itazamwe kama ya upande fulani ambao imepata umaarufu wa mkumbo mkumbo tu.Ni kweli wapemba wengi kwa akili zao na fikra huru wamekubaliana na mustakabali wa CUF?au Unguja wengi wao CCM? Je hapa haitupi mashaka kidogo kuwa kinachopiganiwa ZNZ sio siasa tunazozijua bali ni ushindani wa makundi kwa itikadi wa sehemu wanazotoka na si itikadi za vyama kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla?ukiwasikiliza CUF na CDM vizuri katika swala la kuunda kambi ya upinzani bungeni,kama unapendelea upinzani ueendelee kukua sidhani kama utakubaliana na CDM kuishirikisha CUF achilia vyama vingine ambavyo vilishaonyesha wazi kuegemea upande wa ccm.

Kwa vile maamuzi ya muungano wa upinzani bungeni ni wa hiari kwa CDM kuwashirikisha wengine tuwaache waamue kwa utashi wao,na CUF wasilalamike kwani CDM wanayo haki ya kisheria na wao CUF hawawezi kuidai popote nafasi hiyo.Wasubiri uchaguzi ujao kama watabahatika tena kuipata nafasi hiyo.
 
Ama kweli kupend kubaya.Inavyoelekea hata Mbowe angetoa ushuzi wana cdm mtashangilia!!!!!!!!!!!!!

Sasa hayo ni maneno gani Kalamazoo, ina maana hata wewe kwa kumpenda huyo unayempenda hata angekunya ungeshangilia sivyo? halafu naomba niwaambie jambo moja, suala hapa halikuwa mashindano ya nani kamfunika nani ilikuwa ni kuhusu mustakabali wa taifa zaidi, nadhani tungeelekeza fikra zetu katika kuitafuta tanzania tunayoitaka, THE TANZANIA WE WANT.

Wewe kalamazoo nikikusikia unatukana tena nakufuata hukohuko eboh!!!
 
Tusiandikie mate jamani:

Nyingine nendeni Youtube kwa kubonyeza hiyo Video na mtasikiliza zaidi. Hapo ndipo mjuwe nani alifunika au alifunikwa. Nani ni Kilimanjaro na nani ni Kichuguu..........
 
Last edited by a moderator:
Mbowe ni mtoto mdogo tu katika historia ya Zanzibar
Chadema musitulilie sisi bali lilieni na bunge la tanzania ambalo limewakosesha haki zenu za kupiga kura,na haki nyengine za msingi,sisi zanzibar tunalilia na baradha letu la wawakilishi kwani ndio lenye maamuzi yote wakisema tuitishe kura ya maoni juu ya muungano tukisema noo basi tumeuvunja,tukisema serikali tatu basi tutahakikisha serikali tatu zimekuwa au tumevunjaa muungano.
 
kwa mashabiki wa CDM.Mbowe alifunika, kwa mashabiki wa CUF na CCM..Hamad alifunika..as simple as that!!
 
in fact it was as it was supposed to be! i said be4 the dialogue that chadema will fall under CUfs jaws.
 
ukomavu wa hamad ni kuja kwenye mdahalo kuanika kila aliloongea na wenzake? Ili atuoneshe kuwa ni kidume kweli, mbona hakuaanika alichongea au kufanya na mkewe??? naona CCM imewapa kazi ya kutaka kutufanya tu divert attention yetu ya kushughulikia ufisadi ktk nchi hii

Hata ulichoongea na mkeo hatukitaki hapa!!!
 
..huu utaratibu wa kuwa kukaribisha hata WAHUNI kwenye midahalo naomba ukome.

..moja ya masharti ya midahalao inayoheshimika ni kwamba si ruhusa hata kidogo kupiga makofi au kushangilia wakati wa mdahalo.

..MDAHALO ulikuwa umejaa WAHUNI wengi.
 
watu wa pwani utawajua tu.

kiswahili kingi na vijimisemo vya hovyo hovyo kwa wingi, kazi 0.

Jitu hili ukiliuliza linaishi wapi, atakwambia limelowea Pwani. Kwao huko angebaki kuwa mbeba mizigo ya watalii wanaopanda Mlima Kilimanjaro!
 
Tuangalie kwa mtazamo wa taifa zaidi,chadema imejikita bara na imespread maeneo tofauti imepata wabunge huku ccm ikichukua sehemu kubwa zaidi,CUF ZNZ tena Pemba tu,ccm Unguja.sasa nafikiri CUF itazamwe kama ya upande fulani ambao imepata umaarufu wa mkumbo mkumbo tu.Ni kweli wapemba wengi kwa akili zao na fikra huru wamekubaliana na mustakabali wa CUF?au Unguja wengi wao CCM? Je hapa haitupi mashaka kidogo kuwa kinachopiganiwa ZNZ sio siasa tunazozijua bali ni ushindani wa makundi kwa itikadi wa sehemu wanazotoka na si itikadi za vyama kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla?ukiwasikiliza CUF na CDM vizuri katika swala la kuunda kambi ya upinzani bungeni,kama unapendelea upinzani ueendelee kukua sidhani kama utakubaliana na CDM kuishirikisha CUF achilia vyama vingine ambavyo vilishaonyesha wazi kuegemea upande wa ccm.

Kwa vile maamuzi ya muungano wa upinzani bungeni ni wa hiari kwa CDM kuwashirikisha wengine tuwaache waamue kwa utashi wao,na CUF wasilalamike kwani CDM wanayo haki ya kisheria na wao CUF hawawezi kuidai popote nafasi hiyo.Wasubiri uchaguzi ujao kama watabahatika tena kuipata nafasi hiyo.

Tafuta magazeti mengine zaidi ya MwanaHalisi halafu ndiyo utajua kuwa CUF ina wabunge kutoka mikoa gani kabla ya kuandika madai ya utumbo ya hapo juu. Umefunga milango ya akili yako ndiyo maana ufahamu wako wa mambo ya siasa yamejifunga kiasi cha kutoa madai ya utumbo!
 
Hivi yule mwanamke aliyedai yeye ni Mkatoliki na ni lazima chama chake kiwe CHADEMA alikuwa anamaanisha nini vile?

Mtajificha kama mapanya yanavyojichimbia kwenye mashimo yao lakini end of the day mtaropoka yaliyokuwa ndani ya vifua vyenu!
 
Halafu huyo Mbowe jamani elimu yake ni kiwango gani?

Sitoshangaa watu kula bati kwenye swali hili. Kupenda mno hata chongo utaita "kuona kwa jicho moja".
 
Back
Top Bottom