Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa ndipo utaona tofauti ya kwenda shule na madrasa, mara Hamad Rashid mara Wazanzibar mara Uislam, Hebu kokotaneni wenyewe kwa wenyewe huko kwa waponda urojo
Mimi nashangaa sana wa Zanzibar wapo kimya na wamefurahia kufukuzwa kwa Hamad Rashid. Kwanini Bara mnawaingilia.
Je ni nongwa kwa pandikizi lenu kufukuzwa?
Mbona Chadema walimuengua Zitto kabwe katika kinyang'anyiro cha kugombea uenyekiti wa Chadema taifa kwa kutumia mizengwe na watu hawakusema.
Mbona wamefukuza madiwani wao Arusha, lakini hakuna aliyesema?
Kwanini iwe nongwa kwa CUF.
Tunasikia Mpaka maaskofu Akina Kilaini wanalisemea hilo.
Hii inajionyesha kulikuwa na namna kati ya hamad Rashid na maaskofu na chadema pia.
Ok all in all amefukuzwa na hatakiwi na kama nyie mnamtaka mchukueni basi kuliko kuleta zogo hapo.
Kwa CUF hilo sio tena tulufu bali ni Galasa. kama mnamuona tulufu mchukueni.
Ami mkuu wangu unaposema CUF sio chama cha Waislaam kisha ukasema haya yaliyotokea ni mwendelezo wa kuzima Ushiriki wa WAISLAAM ktk siasa, hapa una maana gani? ikiwa kweli waislaam wanataka kuingia ktk siasa na wapo CUF ambacho sii chama cha waislaam..Je huoni kama waislaam wanataka kukitumia chama hiki kama jukwaa kufanya siasa hivyo kukifanya chama kiwe cha kiislaam?.Uasi wa Hamad Rashid ndani ya CUF umepata uungwaji mkono usio wa kawaida katika vyombo vya habari Tanzania kama kwamba tukio kama hilo halijapata kutokea kwa vyama vyengine au ni mara ya mwanzo katika CUF.
Zaidi ya uungwaji mkono huo, sasa msajili wa vyama bwana Tendwa na Jaji Werema nao wameingilia kati kuonesha kutoridhishwa kwao na uamuzi madhubuti uliochukuliwa na uongozi wa CUF. Haipendezi kwa wanasheria hao kushikilia habari za mahakama ilhali viongozi wa CUF wameshasema hawakupokea amri ya mahakama.
Ukweli ambao wanasiasa na wanaJF hawapendi kuusema ni kuwa Hamad ni mtaji maalum wa kukivuruga CUF. Na kwanini iwe CUF? Ni mkakati wa kuimeza Zanzibar.Kwa upande mwengine CUF si chama cha kiislamu lakini kwa vile kimeasisiwa Zanzibar waislamu ni wengi na hii imekuwa nongwa. Katika mtazamo uliompana huu ni mwendelezo wa kuzima ushiriki wa waislamu katika siasa na hii ni vita ya kimataifa dhidi ya uislamu.
Mkuu na mimi ningependa unifafanulie ni kwa namna gani kufukuzwa kwa Hamad Rashidi kuna uhusiano na vita dhidi ya uislamu duniani?
Mimi nafikiri kama wewe unacho cha kuchangia kuhusu kufukuzwa kwa Hamad Rashid (muislam) kulikofanywa na Wakristu; na kama unaweza kujadili mchanganyiko wa mambo ya dini na hayo mengine, basi wewe changia tu hamna shida, sisi wengine tumekosa la kusema ndo maana tulikaa kimya.yaani kila kitu kina mashiko ila dini ndio haina mashiko?, haijadiliki? Kutajwa kwake ni dhambi? Kwanini ikitajwa dini kuna watu wako mstari wa mbele kabisa kuzuia isitajwe! Hivi huyu mdini ni nani? Na hiyo dini yenyewe ni ipi? Mbona habari za ngono, mipasho, madanguro, ufuska ni ruksa kujadili lakini ikija suala la dini linakuwa nyeti! Kuna usiri gani hapa?
James Magai na Aziza Masoud-MWANACHI
MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake 10 sasa wameiomba Mahakama Kuu Dar es Salaam iiamuru Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi(CUF) wajieleze ni kwa nini wasitiwe hatiani kwa kukiuka amri ya mahakama hiyo.Ukiacha wadhamini hao, jana Hamad Rashid na wenzake, waliomba mahakama iamuru pia wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad wajieleze kwanini wasitiwe hatiani kwa kukiuka amri hiyo.
Pia wanaiomba mahakama hiyo ibatilishe uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho wa kuwavua uanachama hapo Januari 4, 2012, kwa madai kwamba walikiuka katiba ya CUF.
Kabla ya uamuzi huo wa kuwavua uanachama, Januari 3, 2012, Hamad Rashid na wenzake waliwasilisha ombi Mahakama Kuu Dar es Salaama chini ya hati ya dharura wakiomba mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho uliokuwa ukitarajiwa kufanyika Zanziba, uzuiwe kuwajadili.
Kupitia kwa mawakili wao, kampuni ya uwakili ya GF Law Chambers Advocates walidai baraza hilo lina nia ya ama kuwasimamisha au kuwavua uanachama na kwamba uamuzi huo ungeathiri haki zao za kikatiba.
Waliendelea kudai kwamba, kuna kesi ya msingi ya madai namba 1 ya mwaka 2012 waliyoifungua mahakamani hapo wakihoji muundo wa Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho na uteuzi wa wajumbe wa kamati hiyo.
Tayari Jaji Augustine Shangwa katika uamuzi wake wa Januari 4, 2012, aliamuru CUF kusitisha uamuzi wa ama kuwasimamisa au kuwavua uanachama walalamikaji hao.
Hamad Rashid jana alirejea amri hiyo ya mahakama kuu chini ya Jaji na kueleza kwamba CUF waliikaidi na badala yake kuendelea na kutekeleza azma yake ya kuwavua uanachama.