Hamad Rashid na kauli tata!!

Chigwiyemisi

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
531
225
Wadau jana nilimsikiliza HR akiongea na waandishi wa habari mara baada ya shauri lake kusikilizwa na mahakama! Katika maelezo yake alidai kuwa ana imani kubwa na mahakama na ana imani kuwa itatenda haki. Kimsingi ukimuangalia HR ni kwamba anaung'ang'ania uanachama wa CUF kwa udi na uvumba na ndio kisa cha kwenda mahakamani!

Lakini kinachonishangaza ni kwamba katika maelezo yake aliendelea kusema kwamba CUF IMEPASUKA na wananchi wasubiri tumaini jipya. Akatoa mfano akimnukuu Mwalimu Nyerere kuwa alipata kusema kuwa kioo kikiingia vumbi kifute na kikipasuka kiondoe kwa hiyo alimaanisha kwamba CUF imepasuka na inapaswa kuondolewa. Hapa mimi nilifikiri anazungumzia wazo lake la kuanzisha Chama.

Maswali yangu ni haya;
  1. Kwa nini kama CUF imepasuka anaing'ang'ania hadi mahakamani?
  2. Ikumbukwe kuwa Mtatiro anasema hata kama mahakama itamrudisha maamuzi yao POLITICALLY yako palepale, je HR anaweza kufanya kazi bila ushirikiano na wenzakle endapo atarudishwa?
  3. Kwa nini kama yeye ni jasiri na ana support ya watu kama anavyodai asiachane na hiyo kesi akaendelea na taratibu nyingine za kufungua chama chake na kuleta tumaini jipya analosema wananchi wanahitaji?
Nawasilisha
 
Anaweweseka tu.

Kumbuka CUF siku zote wakivunja basi hawajengi tena pale.awaulize akina Mapalala au Bi Naila jidawi watamjuza hilo.
 
Maswali yangu ni haya;
  1. Kwa nini kama CUF imepasuka anaing'ang'ania hadi mahakamani?
  2. Ikumbukwe kuwa Mtatiro anasema hata kama mahakama itamrudisha maamuzi yao POLITICALLY yako palepale, je HR anaweza kufanya kazi bila ushirikiano na wenzakle endapo atarudishwa?
  3. Kwa nini kama yeye ni jasiri na ana support ya watu kama anavyodai asiachane na hiyo kesi akaendelea na taratibu nyingine za kufungua chama chake na kuleta tumaini jipya analosema wananchi wanahitaji?
Nawasilisha

Kuna mambo mawili yanayong'ang'aniwa
1. HR anajua kuwa ndani ya cuf hana nafasi hivyo anapigania abaki na ubunge wake hata kama ni ubunge wa mahakama
2. cuf hawamtaki HR na hivyo wanaona bora abaki na ubunge wa mahakama lakini ndani ya cuf asiwepo
 
Anaweweseka tu.

Kumbuka CUF siku zote wakivunja basi hawajengi tena pale.awaulize akina Mapalala au Bi Naila jidawi watamjuza hilo.

Kijana umekunywa maji ya bendera ya KAFU maana ukiona jina la HOUR povu lakutoka kulikoni!!?
 
Kwa nini kama CUF imepasuka anaing'ang'ania hadi mahakamani?

Ili aendelee kula posho & mishahara ya ubunge ambayo ni jasho la mlipa kodi (mwananchi)

Ikumbukwe kuwa Mtatiro anasema hata kama mahakama itamrudisha maamuzi yao POLITICALLY yako palepale, je HR anaweza kufanya kazi bila ushirikiano na wenzakle endapo atarudishwa?

Ataendelea kupata ushirikiano na wale walompa hilo dili la kusambaratisha nguvu ya CUF hususan Pemba.

Kwa nini kama yeye ni jasiri na ana support ya watu kama anavyodai asiachane na hiyo kesi akaendelea na taratibu nyingine za kufungua chama chake na kuleta tumaini jipya analosema wananchi wanahitaji?
Nawasilisha

Kwasababu anataka lengo la kuisambaratisha CUF litimie kwanza.
 
Huyo ni mnafiki, ameenda mahakamani kwa ajili ya kutetea posho za ubunge. Wakati huo huo amesema mwezi machi anaanzisha chama kipya. Anajidaganya chama chake kitaishia Tanganyika; Unguja na Pemba hatakiwi
 
Huyo ni mnafiki, ameenda mahakamani kwa ajili ya kutetea posho za ubunge. Wakati huo huo amesema mwezi machi anaanzisha chama kipya. Anajidaganya chama chake kitaishia Tanganyika; Unguja na Pemba hatakiwi

Ajifunze kutoka kwa akina nanihii walokuwa CCJ
 
Sawa ia issue ni kubaki bungeni kwanza!

Na hilo ndilo tatizo/wivu mkubwa walionao.....walioingia bunheni kuachia posha ni maumivu na wasiomo wanaumia kuona wenzao wanavuta mkwanja....eg Mbatia
 
nimemsikia akizungumza kwenye tv,kauli yake ni kwamba kuna chama kipya kinakuja mwezi wa march,kwa kauli yake,sasa sijui kama anategemea kupata followers huku bara-atakuwa anajidanganya,arudi kwao zanzibar akafanye shushuli zake huko,.kisiasa ndo ameshastaafu hivyo bila yeye kupenda
 
Jana niliona kwenye taharifa ya habari baadhi ya viongonzi wa CUF wamekwenda kwenye jimbo lake la WAWI huko Pemba,Duni Hajji Duni alisikika akisema kuwa wameshammaliza,huku wananchi wakishangilia.....japokuwa umati ulikuwa ni mkubwa lakini wengi walikuwa ni wanawake....HR naona anawakati mgumu kuliko Kafulila,Kafulila anaweza toka NCCR nakwenda chama kingine na kushinda,huu ndio utamu wa siasa za bara,sio huko Pemba watu wamechanjia CUF
 
Posho tamu meku! mmesahau hawa jamaa Samweli Sita, na Mizengo pinda waliwahi kumwaga chozi walipotishiwa kuwajibishwa
 
Kuna mambo mawili hujayaweka aliyasema mimi nilimsikia BBC akiongea:
1. Pamoja na kusema anaiamini mahakama na mahakimu, alilaumu kwa nini kwamba shauri lao la kupewa muda halikukubaliwa na mahaka lakini hili la CUF limekubaliwa
2. Baada ya hiyo issue ya kioo alisema wananchi wawe na subira mwezi wa tatu atakuja na chama kipya kitakacho toa dira. So kuanzisha chama chake ameiweka wazi kabisa.

My take: kama kesha amua kuanzisha chama anahangaika nini mahakamani???
 
Kwa mtazamo wangu, Hamad Rashid ana haki ya kupinga mahakamani kufukuzwa kwake kwenye chama. Akirejeshewa uanachama ndipo anaweza kuamua kujiondoa kwenye CUF, na hiyo itamjengea heshima zaidi kuliko kufukuzwa. Tuhuma zilizosababisha kufukuzwa kwake hazina uzito kivile. Naona zaidi ni uhuni tu uliofanywa na Maalim Seif na wafuasi wake. Viongozi wetu wajifunze kuwa wavumilivu wanapokosolewa. Kwa hili namuunga mkono Hamad Rashid, japokuwa huwa sikubaliani na baadhi ya misimamo yake kwenye masuala mengine.
 
Back
Top Bottom