Leonard Robert
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 11,064
- 7,196
tulijua haya madubwasha yake yatamfikisha mahali pabaya.mnafiki wa kambi ya upinzani aliiwangia,sasa yamemshinda.
hapo kwenye red naomba msaada hivi kila chama kina kambi yake? Ufahamu wangu bungeni kuna kambi mbili ya Serikali na ya Upinzani ( Ya Pinda na nyingine ya Mbowe) sasa hii ya Mnyaa ni kitu ganiCUF yafanya mabadiliko ya uongozi Thursday, 26 May 2011 22:25 0diggsdigg
Elizabeth Ernest
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemteua Julius Mtatiro, kuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara na Ismail Jusa Ladhu kushika wadhifa huo huko Zanzibar.
Akitangaza uteuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema tayari Baraza Kuu la CUF, limewapitisha.Alisema baraza hilo pia limepokea na kuridhia mabadiliko yaliyofanywa na wabunge wa CUF, kwa kumchagua Mohamed Habib Mnyaa, kuwa kiongozi wa kambi ya CUF bungeni na Magdalena Sakaya, kuwa Katibu wa kambi hiyo.
Mbunge mwingine ni Hemed Salim ambaye alichaguliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya CUF.Katika hatua nyingine, CUF imemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kujiuzulu kwa madai kuwa ameshindwa kutumia vyanzo vya umeme vilivyopo, kukabiliana na tatizo la nishati hiyo.
Chama hicho kimesema Tanzania ina uwezo wa kufua umeme wa megawati 5,000 ikilinganishwa na megawati 791 za sasa zinazoingizwa katika gridi ya taifa.Kwa mujibu wa Profesa Lipumba vyanzo vya maji vinachangia kwa megawati 562 ya umeme huo.
Alisema makaa ya mawe yaliyogunduliwa yanaweza kuzalisha umeme wa megawati 1000 kwa zaidi ya miaka 50 ijayo wakati gesi iliyogunduliwa Mnazi Bay, mkoani Mtwara, Mkuranga na Songosongo, Kilwa inaweza kuzalisha umeme zaidi wa megawati 1000 kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.
"Lakini pia madini ya uraniamu yaliyogunduliwa Namtumbo na Manyoni, yana uwezo wa kuzalisha malaki ya megawati za umeme kwa muda mrefu. Gharama za kuzalisha umeme wa jua na upepo zimepungua na zinaendelea kushuka,"alisema Profesa Lipumba. "Miaka 50 baada ya uhuru hatuna sababu ya kutokuwa na umeme wa uhakika, lakini Serikali ya CCM na Waziri Ngeleja,
Source: Mwananchi 27/5/2011
Nice CUF wameonyesha kuwa sio wadini kwa Mabadiliko hayo... Tungojee tuone Ushiriki wao utakuwaje
Inachekesha CCM wanaukimbilia Udini; CUF inataka kujisafisha...
MZEE WA KAMBI NDOGO YA UPINZANI.... CUF KAZI KWENU
Tayari mgogoro mkubwa wa kimaslahi binafsi umeikumba Cuf baada ya hamad Rashid kumpinga waziwazi maalim seif na sasa anamkakati wa kumngoa ktk nafasi ya katibu mkuu wa cuf na pia kutaka kuiteka kambi ya maalim seif huko Pemba. Mkakati huo umekuja baada ya hamad rashid na kundi lake kutumia muda mwingi kutembelea kisiwa cha Pemba ili kumkosanisha maalim seif na wakazi wa Pemba ambao idadi yake kubwa ni Cuf.
Hamad rashid amechukua hatua hiyo baada ya kugonga mwamba kupata nafasi ktk bunge kama mmoja ya viongozi wa kambi ya Upinzani bungeni baada ya CDM kumwekea vikwazo. pia hatua ya rashid inakuja baada ya kuongolewa nafasi ya mkuu wa kambi isiyorasmi bungeni ambapo habib mnyaa ameichukua.
habari amabazo zimeenea eti Mpango huo wa hamad rashid kutaka kutafautiana na Maalim unatoka na mpango hamad rasdhid kutaka kuahmia chadema. rashid licha ya kuonekana waziwazi kutomshinda maalim seif . mapngo huo unafanywa ili hamad aone ameonewa na apate sababu ya kuhamia cdm. kwani cdm ilihusishwa na hamad rashid kutaka kuwa mgombea mwenza wa dk slaa 2010
Mwe huyu alikuwa wapi? naona leo amerudi kwa kasi mno.