HAMAD RASHID katika Njama za Kumng'oa Maalim Seif?

CUF wanavuna walichopanda. Kwamba CUF kiliingia chumba cha wagonjwa mahututi pale ilipofunga ndoa na CCM.

Nakubaliana na Gurtu asilimia mia moja. CUF kwisha. Gurtu laway. Nai' sayutia nee kihhoe?

Watu munatakiwa kujua kua zanzibar ya sasa hatuhitaji sana vyama vya siasa tunahitaji maendeleo zaidi.

Kule zeji watu wameshashituka sasa na nyinyi Tanganyika mkikua mutatuelewa na huenda mukafuta hizo njia tutakazopita.

Nasema haya kwakujiamini kwani kila nikiiangalia Tanganyika naiona zanzibar yazamani imehamia huko(wanasiasa kupigana,viongozi kuzomewa,wafuasi wa vyama vyaupinzani kusweka ndani bila ya kesi,maandamano yasioisha,risasi nje nje polisi kuwapiga raia n,k) Hivyo ndivyo ilivyokua zanzibar ya 1995-2005.

Kwasasa hatujajuta bado na tunatamaa kubwa ya maendeleo ya wananchi na sio ya vyama,huenda sikuza mbele vyama vikakosa soko Zanzibar.
naona mnataka kurejesha utawala wa kisulutani sasa

Wakimgusa tu maalim anarudi CCM, kumbe haijui vizuri siasa ya Zanzibar, mara moja kuundwa sheria na kupitishwa na Baraza la Wawakilishi imruhusu Maalim arudi nyumbani.

Yule bingwa wa kambi ndogo ya upinzani bungeni, amepigwa chini tena cuf.sasa atabadili kanuni ili cuf iwe na kambi mbili ndogo za upinzani bungeni,moja kubwa inayoongozwa na mnyaa,na ndogo atakayoiongoza yeye.au ataenda nccr akawe mkuu wa kambi yao. Al tatur munafik

CUF yafanya mabadiliko ya uongozi Thursday, 26 May 2011 22:25 0diggsdigg

Elizabeth Ernest
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemteua Julius Mtatiro, kuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara na Ismail Jusa Ladhu kushika wadhifa huo huko Zanzibar.

Akitangaza uteuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema tayari Baraza Kuu la CUF, limewapitisha.Alisema baraza hilo pia limepokea na kuridhia mabadiliko yaliyofanywa na wabunge wa CUF, kwa kumchagua Mohamed Habib Mnyaa, kuwa kiongozi wa kambi ya CUF bungeni na Magdalena Sakaya, kuwa Katibu wa kambi hiyo.

Mbunge mwingine ni Hemed Salim ambaye alichaguliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya CUF.Katika hatua nyingine, CUF imemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kujiuzulu kwa madai kuwa ameshindwa kutumia vyanzo vya umeme vilivyopo, kukabiliana na tatizo la nishati hiyo.

Chama hicho kimesema Tanzania ina uwezo wa kufua umeme wa megawati 5,000 ikilinganishwa na megawati 791 za sasa zinazoingizwa katika gridi ya taifa.Kwa mujibu wa Profesa Lipumba vyanzo vya maji vinachangia kwa megawati 562 ya umeme huo.

Alisema makaa ya mawe yaliyogunduliwa yanaweza kuzalisha umeme wa megawati 1000 kwa zaidi ya miaka 50 ijayo wakati gesi iliyogunduliwa Mnazi Bay, mkoani Mtwara, Mkuranga na Songosongo, Kilwa inaweza kuzalisha umeme zaidi wa megawati 1000 kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

"Lakini pia madini ya uraniamu yaliyogunduliwa Namtumbo na Manyoni, yana uwezo wa kuzalisha malaki ya megawati za umeme kwa muda mrefu. Gharama za kuzalisha umeme wa jua na upepo zimepungua na zinaendelea kushuka,"alisema Profesa Lipumba. "Miaka 50 baada ya uhuru hatuna sababu ya kutokuwa na umeme wa uhakika, lakini Serikali ya CCM na Waziri Ngeleja,

Source: Mwananchi 27/5/2011

Habari njema. Kati ya wana siasa ninao wachukia ni JK na Hamad Rashid. Alitaka awe kiongozi wa kambi ya upinzani wakati hata Chama chake hakimwamini?

Mtatiro anafanya nini huko? Kuwa CUF ni sawa na kusukuma gari bovu ukiwa ndani.

Am happy kusikia habari ya CUF hapa JamiiForum! Nimechoshwa na habari za cdm na ccm

Back
Top Bottom