Hamad Rashid apiga hodi ADC; Asema yuko tayari kujiunga kama akiombwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
ALHAMISI, AGOSTI 30, 2012 05:21 NA BAKARI KIMWANGA, DAR ES SALAAM

*Asema yuko tayari kujiunga kama akiombwa
*Aonya Watanzania hawataki mitafaruku

MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), hatimaye amevunja ukimya na kusema yupo tayari kujiunga na Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC), kama chama hicho kitapinga ubinafsi kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Kauli hiyo, ilitafsiriwa kama kijembe kwa wanasiasa wanaofanya vyama kama mali zao binafsi.

Kwa kipindi kirefu sasa, Hamad amekuwa na msuguano na Chama chake cha CUF, hali iliyopelekea kufikishana mahakamani kupinga hatua ya kufukuzwa kwake uanachama pamoja na wenzake 10.

Akihutubia Mkutano Mkuu wa ADC, uliofanyika juzi mjini Dar es Salaam, ambapo Hamad, alikuwa kama mgeni mwalikwa, alisema kupatikana kwa usajili wa kudumu kwa ADC ni kuendelea kufungua njia ya demokrasia nchini.

Alisema vyama vingi vya siasa, vimekuwa na viongozi wengi walevi wa madaraka ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi kutatua migogoro ya ndani, kuliko kuwasaidia Watanzania kuondoa matatizo yanayowakabili.

"Ninajua hadi kufikia hatua ya kupata usajili wa kudumu ADC, haikuwa kazi rahisi … kikubwa kinachotakiwa ni kuepuka viongozi walevi wa madaraka, kama ambavyo tumeona siku zilizopita.

"Ulevi wa madaraka ni tofauti na pombe, hakuna dalili ya kuumwa kichwa wakati wowote unapokuwa madarakani, hautoki mwilini mpaka ufe au ufukuzwe. Na humfanya mtu awe haoni wala hasikii na hafahamu isipokuwa yale anayoyataka yafanyike kwa kutumia nguvu za maamuzi.

"Nami nipo tayari kujunga na ADC, wakati wowote huko mbele, ikiwa mtaongoza kwa kuepuka migogoro na kauli za kibabe za sasa bwana mkubwa amesema.

"Wengi wale wanaolewa hubaki na maruirui ya madaraka hata baada ya kustaafu au kutolewa madarakani…kila mlevi wa aina hii, hutaka abaki na madaraka na hufanya kila njia ili alinde madaraka hayo yasimtoke."

Alisema kutokana na hali hiyo, Watanzania wamekata tamaa na kuachwa njia panda na wanasiasa wa aina hiyo.

Hamad, ambaye muda wote alionekana kujiamini na hata wakati mwingine kujisahau kwa kujitambulisha kuwa ni mwanachama wa ADC, alisema anasikitishwa na hila chafu zilizofanywa na baadhi ya vyama kuhujumu zoezi la uhakiki kwa wanachama wake kwa kununua kadi kwa wanachama wa chama hicho.

"ADC ni chama kipya, ufisadi wa aina hii ni lazima mjiepushe nao, na hali hii, kwenu iwe fursa nzuri katika kutimiza kauli mbiu yenu ya dira ya mabadiliko. Watanzania wameweka matumaini yao katika chama cha ADC kwa misingi yake, ni vema tusiwakatishe tamaa.

"Muepuke virusi vya dhambi, tuliyoyafanya nje ya ADC, ili yasije yakajirudia ndani ya ADC, kwani kosa si kufanya kosa, bali ni kurudia kosa. Na ninarejea tena upukeni kukigawa chama baina ya bara na visiwani ili muweze kuwa chama chenye umoja, upendo na kuaminiana," alisema Hamad.

Aliwataka viongozi waliochaguliwa katika mkutano huo kutotumia vibaya midomo yao kwa kutoa kauli za kibabe, matusi, vitisho na udhalilishaji kwa kisingizio chochote kile, kwani kufanya hivyo watashindwa kulinda na kuendeleza urithi na maadili ya kitaifa.

Alisema ADC, imeanzishwa katika kipindi cha changamoto hasa kwa vyama vya upinzani kuwa na kazi ya ziada katika kupigania maendeleo ya kidemokrasia, huku vikitafuta ridhaa ya wananchi ili kupewa dhamana ya kuongoza.

"Ukweli vyama vya siasa vinakabiliwa na mazingira mazito na kutoshindana na CCM pekee, bali vinashindana na kundi kubwa la taasisi za umma na binafsi ambazo zimejaa makada wa CCM.

"Moja ya matatizo yanayoathiri upinzani ni kukosa ajenda ya pamoja ya kudumu, kwani baadhi ya vyama vimejikuta vikiingia katika ushindani baina yao, badala ya kuwa na makakati wa pamoja wa kuiondoa CCM.

"Badala ya mkakati wa kuiondoa CCM na kupata fursa ya kurekebisha, kusimamia na kuratibu vipaumbele vitakavyoleta maendeleo ya haraka ili kuondokana na uchumi tegemezi kutokana na madhara yaliyosababishwa na watawala.

"Mtaalamu maarufu zaidi wa masuala ya kivita kutoka China, Sun Zu anasema yeyote ambaye hawezi kushinda vita, lazima ajilinde na anayeweza kushinda, lazima ashambulie.

"Hivyo nashauri mtumie busara, hekima na ukomavu wenu kisiasa wa kushambulia kwa kutumia njia zinazokubalika kisheria, kanuni na taratibu za kiutawala," alisema Hamad.

Baada ya kuhutubia mkutano huo, wajumbe wa mkutano huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Said Miraj, walipitisha jina la Hamad kuwa mlezi wa chama hicho, kwa kauli moja.

Januari 10, mwaka huu, Hamad na wenzake walifungua kesi Mahakama Kuu, wakidai Baraza la Taifa la Uongozi la CUF lilipuuza amri ya mahakama iliyolizuia kuwajadili wala kuwachukulia hatua zozote, wakati wa mkutano wake wa Januari 4, 2012, mjini Zanzibar.

Amri hiyo, ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa Januari, kutokana na maombi waliyoyawasilisha mahakamani hapo Januari 3, 2012, chini ya hati ya dharura.

Mbali na Hamad, wengine waliofukuzwa uanachama CUF ni Doyo Hassan Doyo, Shoka Khamis Juma na Juma Saanane, wote wakiwa Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho.

 
Wanasiasa wa Tanzania wamezama kwenye kasumba mbaya sana ya kudhani wananchi ni mazuzu. Mara utasikia wananchi ndio waliniomba nigembee, mara waandishi wa habari ndio walinifuata na kunihoji. Zama hizi za dotcom Hamad Rashid anasema atajiunga na ADC kama ataombwa? Hivi mtu anajiunga na chama kwa sababu ameombwa au kuna jingine? Vipi kuhusu itikadi na sera?
 
Hii ya kupewa ulezi wa ADC sioni uhalali kwake kuendelea kupinga kufukuzwa CUF mahakamani. Mahakama iwatendee haki CUF. Kama ni kurudia uchaguzi agombee hukohuko ADC.
 
hamad ana kesi mahakamani dhidi ya cuf na mpaka leo anatambulika kuwa ni mbunge wa cuf bungeni. sasa kuteuliwa kuwa mlezi wa ADC haiwezi kuathiri shauri lake mahakamani dhidi ya CUF?
 
Back
Top Bottom