Hamad Rashid amuumbua Maalim Seif; agoma kuhojiwa!

another sarakasi ndani ya cuf oh men hawawezi kutumia wazee wa chama kwa hekima na busara wakayamaliza kila siku wanakuja na jipya au ndo kujaribu kukirusisha chama kwenye ramani
 
Ni kweli ndio naskiliza sasa hivi kwene kijiredio gani vile sijui! Mawingu radio! Jamaa anaoongea kwa uchungu sana
 
Japo post haisomeki vizuri lakini nadhani hoja ya msingi ni kutuhabarisha juu ya kile kinachoendelea au matokeo ya kikao cha kamati ya maadili na nidhamu iliyokaa leo kujadili suala la Hamad Rashid,haya mengine naona mnasukuma muda tu,mwenye taarifa rasimi atujuze
 
Hamad Rashid amegoma kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CUF kuhusu tuhuma zake za ‘uasi' katyika CUF. Ameyatamka hayo mbele ya waandishi wa habari leo.

Amesema sababu ni kwamba kamati hiyo haipo kikatiba (katiba ya CUF), hana imani na wanakamati, na kwamba tayari ameshahukumiwa kabla hata ya kwenda mbele ya kamati

Anasema Maalim Sewif baada ya kufanya ziara Pemba na kwingineko bara na visiwani na kufanya vikao na watendaji wa chama, alimuandikia barua M/Kiti Prof Lipumba kwamba "kwa mawazo ya wengi aliyopata, ni kwamba Hamadi Rashidi afukuzwe kutoka chama."

Kuna mengine mengi kayasema ambayo Ch 10 bulletin ya 7pm ilimkatiza.


Nawasilisha.
 
Nimemuona CH 10. Mie nafikiri hilo suala la maalim Seif kuandika barua kwa Lipumba kwamaba "kwa mawazo ya wengi, Hamadi afukuzwe" ndilo litakuja kumuumbua Maalim na genge lake.

Ni kweli, maana ni kama alikuwa anamshauri profesa akubaliane na maamuzi ya genge lao kwani CUF haiko Pemba na Zenji tu, bali Bara pia.

Je, Seif kafika kote huko, au alituma mablue guards kufanya tathmini?
 
MHE. Hamad Rashid amegoma kuhojiwa na Kamati ya maadili ya CUF. Sababu alizotoa ni kwamba kamati hiyo ipo kinyume na katiba ya CUF. Sababu nyingine ni kwamba Maalim Seif ashamhukumu kupitia email iliyotumwa kwa Prof Lipumba kutoka kwa Maalim Seif. Katika email hiyo, Maalim Seif anamueleza Prof. Lipumba kwamba Wanachama wengi wanataka Hamad Rashidi afukuzwe Cuf ( Katika ziara ambazo Maalim Seif alizofanya Unguja na Pemba)
Hamad Rashid amesema kwamba anamheshimu Maalim Seif na akazidi kusisitiza kama Maalim Seif anataka kubaki na heshima hiyo, afuate nyayo za Nelson Mandela na Hayati. Mwalimu Nyerere.

Wakati huo huo, Kamati ya Maadili ya CUF imesema kwamba baada ya Hamadi Rashid kugoma kuhojiwa, kinachofuata ni kupeleka taarifa kamati ya utendaji na baadae baraza la taifa la CUF

Source. CHANEL 10

Nawasilisha
 
Mungu wangu, huyu naye inaelekea watamKafulila. Nahofia chaguzi ndogo wakuu.
 
Wanatanza(cuf) mwaka 2012 kwa migogoro naona hapo taratibu zimekiukwa ili kutimizwa kw malengo ya viongozi walio madarakani bila hata kuangalia madhara ya matendo hayo. Tusubiri Mtatiro anasemaje?
 
Star TV news saa mbili:

Hamad Rashid amesema hawezi kukubali kuhojiwa na kamati ya maadili ya CUF maana amepata waraka ulioandaliwa na Maalim Seif unaotaka afukuzwe chamani. Amesema kama maamuzi hayatakuwa ya vikao rasmi, atakwenda mahakamani

M/Kiti wa Kamati ya maadili Bw. Kambaya anasema uamuzi wa Hamad RAshid ni uvunjifu wa katiba na wao wataandaa taarifa kupeleka ngao za juu za CUF.

Maoni yangu: Mwisho wa mgogoro huu sijui kama CUF itakuwa hai.
 
Mbunge wA Wawi HAMAD RASHID amegoma kuhojiwa na kamati ya nidhamu ya chama hicho, na kueleza kuwa haikubali kamati, maana si ya kikatiba, na pia Mwenyekiti wa kamati hiyo alishiriki kutoa tuhuma dhidi yake, na hivyo kwa namna yoyote hawezi kumtendea haki.

SOURCE: TBC NEWS BULLETIN.
 
safi sana.... ubwabwa-ubwabwa tu yakhe... MIE NAMUONA HUYU KAMA COMICAL ALI VILE
information_minister_oscar.jpg
 
Mfumo kristo haukupenda hii kitu ndio maana watu wao ndani ya serikali wameamua kuingia kazini kumzunguka Kikwete.

Mmh.!how?wamemuonga HR na MS kufanya fujo cuf?hakuna kitu kama hicho bana,mfumo kristo ni mawazo yako ya kufikirika.
 
Nimemuona CH 10. Mie nafikiri hilo suala la maalim Seif kuandika barua kwa Lipumba kwamaba "kwa mawazo ya wengi, Hamadi afukuzwe" ndilo litakuja kumuumbua Maalim na genge lake. Ni kweli, maana ni kama alikuwa anamshauri profesa akubaliane na maamuzi ya genge lao kwani CUF haiko Pemba na Zenji tu, bali Bara pia. Jee Seif kafika kote huko, au alituma mablue guards kufanya tathmini?

Kama ni kweli Maalim Seif alifanya hivyo, basi alikuwa na ajenda ya siri dhidi ya HR. Nilifikiri Maalim ni mtu wa busara, kumbe... au kisha onjeshwa na magamba?

naona sasa anajimaliza mwenyewe. Nawasikitikia CUF bara, sijui nani atawatetea, maana Mtatiro kisha viukwa kilemba cha kipemba. Too sad!
 
Back
Top Bottom