Hamad Rashid amuumbua Maalim Seif; agoma kuhojiwa!

sisi agent

Member
Nov 19, 2011
30
16
Katika hali isiyokuwa ya ya kawaida, Mbunge wa Wawi amepata nyaraka muhimu za kufukuzwa kwake kabla hata kusikilizwa katika kamati ya madili.

Waraka huo ulikuwa unatumwa kwa Lipumba ukiwa umemaliza kazi ya kummaliza kabla ya kusikilizwa na tayari CUF ikiwa imechajipanga kwa uchaguzi baada ya wiki moja; sasa akitambulishwa mgombea Jaji Yahya kuwa ndio chaguo la Maalim Seif.
Hamad Rashid amegoma kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CUF kuhusu tuhuma zake za ‘uasi' katyika CUF. Ameyatamka hayo mbele ya waandishi wa habari leo.

Amesema sababu ni kwamba kamati hiyo haipo kikatiba (katiba ya CUF), hana imani na wanakamati, na kwamba tayari ameshahukumiwa kabla hata ya kwenda mbele ya kamati

Anasema Maalim Sewif baada ya kufanya ziara Pemba na kwingineko bara na visiwani na kufanya vikao na watendaji wa chama, alimuandikia barua M/Kiti Prof Lipumba kwamba "kwa mawazo ya wengi aliyopata, ni kwamba Hamadi Rashidi afukuzwe kutoka chama."

Kuna mengine mengi kayasema ambayo Ch 10 bulletin ya 7pm ilimkatiza.

Mbunge wa Wawi HAMAD RASHID amegoma kuhojiwa na kamati ya nidhamu ya chama hicho, na kueleza kuwa haikubali kamati, maana si ya kikatiba, na pia Mwenyekiti wa kamati hiyo alishiriki kutoa tuhuma dhidi yake, na hivyo kwa namna yoyote hawezi kumtendea haki.

SOURCE: TBC NEWS BULLETIN.
Hamad Rashid ngangari

  • Aisambaratisha Kamati ya Nidhamu, yashindwa kumhoji
na Asha Bani na Abdallah Khamis

MBUNGE wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), sasa anaonekana kuwa mwiba mkali dhidi ya viongozi wa juu wa chama chake wanaodaiwa kuwa katika njama za kumfukuza, baada ya kuweka hadharani nia yake ya kuwania ukatibu mkuu wa chama hicho, Tanzania Daima Jumatano, limebaini.

Katika hali isiyotarajiwa, mwanasiasa huyo jana aliweka pingamizi na kufanikiwa kukisambaratisha kikao cha Kamati ya Nidhamu na Maadili iliyoitishwa Makao Makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumhoji yeye na wenzake kwa tuhuma za kwenda kinyume cha katiba ya chama hicho.

Vyanzo vyetu vimeeleza kamati hiyo ya nidhamu na maadili iliyo chini ya Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Hamis Machano, haikuwapo ndani ya chama hicho, lakini iliundwa ghafla hivi karibuni kwa lengo la kumshughulikia Rashid na wanachama wenzake 12, wanaodaiwa kuwa ‘waasi ndani ya chama.'

Hata hivyo, jana wakati akisubiriwa kuhojiwa, mwanasiasa huyo alifika na kuwasilisha barua kwa Katibu wa Kamati hiyo, Hamis Hassan, akihoji uhalali wa kamati na wajumbe wake, huku akisema: "Nina hakika kuwa hakuna haki katika kikao hichi."

Katika hoja zake za kupinga kuhojiwa, Rashid alisema uhalali wa kamati hiyo upo mashakani, kwani katiba iliyotumika kuiunda haijawekwa wazi, huku akibainisha kuwa kwa ufahamu wake Katiba ya CUF ya mwaka 1992 inayotumika hadi sasa haina kitu kinachoitwa "Kamati ya Maadili na Nidhamu ya Chama", na ile ya mwaka 2010 ikiwa bado haijaanza kutumika.

Alikosoa pia uhalali wa kamati hiyo kwa maelezo kuwa hata baadhi ya wajumbe walioteuliwa kumhoji tayari walishasikika hadharani wakimtuhumu na kumtia hatiani.

"Katika pingamizi langu pia nimewakataa wajumbe watano kati ya wanane walioteuliwa katika kamati ya maadili kwa ajili ya kunijadili ambao kati yao tayari walishanitolea tuhuma mbalimbali na hata kutuma walinzi kuweza kuvuruga mikutano mbalimbali iliyokuwa imeandaliwa na wanachama na kuwataka walinzi kutumia silaha za maneno na vitendo ambavyo vilikuwa vikifanyika hadharani," alisema Rashid.

Aliwataja wajumbe hao kuwa ni Hemed Said, Hamis Machano Hamis, Abdul Kambaya na Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Juma.

Katika kuthibitisha hayo, Rashid katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Crystal Palace Hotel, aliweka hadharani mawasiliano ya siri yaliyofanywa kwa njia ya ‘internet' baina ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad na Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba, yakihusu haja na mbinu za kutaka kumfukuza kwenye chama hicho.

Katika mawasiliano hayo yaliyofanywa kwa kutumiana barua pepe, wametajwa pia kwa vyeo vyao, Machano Hamis Machano na Hamis Hassan, ambao ndio viongozi wakuu wa Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama, hivyo kumfanya Rashid apinge uhalali wa kuhojiwa na kamati hiyo.

Maandiko yenye jina la Maalim Seif kupitia barua pepe ya
msellemshariff@yahoo.co.uk, yanasomeka yakimtaka Profesa Lipumba ahakikishe kuwa Rashid anafukuzwa kwenye chama hicho na ikibidi ahamie CHADEMA au CCM.

"Sisi tunahisi chama ki-act decisively, hasa dhidi ya jamaa yako (Rashid). Yeye muono wetu tumfukuze kwenye chama na akiamua kwenda mahakamani na mahakama kutoa uamuzi wa kumpendelea yeye, mwache awe mbunge wa mahakama kama walivyokuwa kina Asha Ngede na Naila Majid," ilisomeka sehemu ya maandiko ya Maalim Seif kwenda kwa Profesa Lipumba.

Pia sehemu nyingine ya mawasiliano hayo ilisomeka hivi: "Sasa ni kumuacha jamaa yako (Rashid) aendelee kufanya kazi aliyopewa na rafiki yake ya kuivuruga chama au chama kimvuruge yeye! Ikishajulikana kuwa si mwanachama tena, atakuwa hana mashiko na muache aende CCM au CHADEMA akawe mgombea mwenza."

Aidha, ujumbe mwingine wa barua pepe ulioandikwa na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama aliyetumia anuani ya
makapahamis@yahoo.com kwenda kwa Profesa Lipumba, wenye kichwa cha habari, unaeleza kunasa taarifa za vikao vya siri vya kundi la Hamad, ikiwamo ya hali ya kutokuaminiana na kuazimia kulishana viapo, ikibidi hata kuuana, pindi ikigundulika kuna msaliti miongoni mwao.

Mawasiliano ambayo Rashid aliyatumia kuwaeleza waandishi wa habari jinsi ambavyo ameshahukumiwa kabla ya kusikilizwa.

Mbali na kufichua siri hizo kwa wanahabari, pia Rashid kupitia barua yake ya pingamizi alimtaka Katibu wa Kamati hiyo ya Nidhamu amueleze ni vifungu vipi vya kikatiba alivyokwenda navyo kinyume.

Kutokana na barua hiyo ya pingamizi, kikao cha kamati hiyo iliyokuwa imhoji hatimaye kilivunjwa bila wanahabari kuelezwa hatua zitakazofuata.

Katika hatua nyingine, mbunge huyo alijibu tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa dhidi yake kuwa alishindwa kukijenga chama wakati akiwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, pamoja na kutumia fedha za chama bila kuzitolea maelezo.

Alisema tuhuma hizo hazina mashiko na kusisitiza kuwa alipokuwa kiongozi wa kambi ya upinzani alitekeleza wajibu wake kikamilifu kwa kuwaonyesha njia wabunge wote wa upinzani, lakini wale wa CUF walishindwa kuwa mahiri kulinganisha na wale wa CHADEMA.

"Wananilaumu kwa hilo, lakini ni wajibu wa kila mbunge kuwa mbunifu. Hoja nyingi nilizoziibua wenzangu wa CUF walishindwa kuzitumia, matokeo yake wabunge wa CHADEMA kwa umakini wao walizitumia vizuri na kupata umaarufu," alisema.

Kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, alisema yeye binafsi ameshaisaidia CUF zaidi ya mara tano pindi wanapokwama katika masuala mbalimbali ya kitaifa hivyo hawezi kufuja fedha za chama hicho.

Kuhusu tuhuma za kujihusisha na Lowassa, Hamad alisema viongozi wake hao wameamua kumchafua kwa kutumia propaganda bila sababu za msingi.

Alimtaka Maalim Seif afuate nyayo za hayati Mwalimu Nyerere na Nelson Mandela kwa kusoma alama za nyakati kwani wao waliamua kujiuzulu na kulinda mazuri yao waliyoyafanya.

"Sisi kwetu Pemba tuna msemo kuwa mtu mzima akivuliwa nguo huchutama kuficha aibu yake, na kwa kuwa Maalim anajua dhambi aliyoifanya mimi simshauri ajiuzulu, kwa kuwa nina amini ni mwenye akili ya kupima mambo na ataamua njia nzuri ya kupita," alisema Hamad.

Source: Tanzania Daima
Hamad Rashid ngangari
 
Jamani sio muda mrefu ukweli mtaujua maana bomu likiripuka ndio mtakubali kazi yangu ni kuwapa hoja sio kuwafikirisha kama mimi ndio hamad au seif habari ni habari hata kama imekukwaza
 
Jamani sio muda mrefu ukweli mtaujua maana bomu likiripuka ndio mtakubali kazi yangu ni kuwapa hoja sio kuwafikirisha kama mimi ndio hamad au seif habari ni habari hata kama imekukwaza

Tupatie update za kikao cha kamati ya nidhamu kinachoendelea. Hii story imekaa kama vile mnaitafutia cuf coverage kwenye vyombo vya habari. Maana tangu wafunge ndoa na ccm wamepotea kwenye ramani.
 
Mtoa habari za kikaoni tupe update, mbona kimya au Hamadi Rashidi wameshanyang'anywa kadi
 
Kikao kinaendelea lakini dalili zinaonyesha uasi ndani ya cuf ni mkubwa sana kiasi ambacho hata kikao ni kigumu sasa huenda hamad akafanya press na kugawa waraka huo mimi nilipata natupia jamvini

Please ukifanikiwa kuupata tutupie na sisi tujue kama Ndoa yao na CCM ipo au wameachika. bwana wao CCM yupo hoi anaumwa sijui kama 2015 atakuwa mzima. Mungu amuangamize CCM na huu umaskini aliotututia
 
Maalim Seif mjanja sana, sasa hivi anajitafutia uhalali na umaarufu kwa Wazanzibari kwa madai ya kijinga kama:
-BOZ
-Urais wa kupokezana bara na Zanzibar
 
Dhambi ya unafki cuf inawaangamiza waache wamalizane waliyataka mambo ya ndoa na ccm wakaingia mkenge hawakujua nia ya ccm ni kuwkomoa na kuwaua kisiasa
 
Hamad ni kijana wa Pinda kummaliza Seif ili kuiuwa CUF hivyo msaada wowote anaotaka atapata tu.
 
Kikao kinaendelea lakini dalili zinaonyesha uasi ndani ya cuf ni mkubwa sana kiasi ambacho hata kikao ni kigumu sasa huenda hamad akafanya press na kugawa waraka huo mimi nilipata natupia jamvini

Kama hizo nyaraka Rashid anazo, kwanini asimgeuzie kibao maalim? Maana tunaambiwa kuna idadi ya wabunge CUF wanaomuunga mkono Rashid kwenye harakati zake hizi ingawa nguvu ya pesa iko kwa maalim!
 
Dhambi ya unafki cuf inawaangamiza waache wamalizane waliyataka mambo ya ndoa na ccm wakaingia mkenge hawakujua nia ya ccm ni kuwkomoa na kuwaua kisiasa

akili zawatu zime pararaiz eti kwa kujitia wanaisema cuf. Midomo yao inatoa povu na harufu kwa kusema kitu kisicho na mantiki eti ndoa na usaliti. Eti unaumiza akili inaoza kwa kuiwazia cuf yenye wa bunge zaidi ya thelathini. Inayopata ruzuku yake na inayoungwa mkono na wa tanzania hapa mtu povu litatamtoka tu ngoja nione.
 
akili zawatu zime pararaiz eti kwa kujitia wanaisema cuf. Midomo yao inatoa povu na harufu kwa kusema kitu kisicho na mantiki eti ndoa na usaliti. Eti unaumiza akili inaoza kwa kuiwazia cuf yenye wa bunge zaidi ya thelathini. Inayopata ruzuku yake na inayoungwa mkono na wa tanzania hapa mtu povu litatamtoka tu ngoja nione.
Wabunge wenyewe wako wapi mbunge gani anawakilisha mtaa mmoja na kwa wazenji wanavyooana utakuta mtaa mzima ni wa familia moja usikute mzee mwenyewe ndiye mbunge.
 
Hamadi Rashid amekataa kuhojiwa na Kamati ya Maadili kwa kile alichodaiu kuwa haina mamlaka kisheria ...
 
Mbona BAKWATA imechelewa kutoa tamko juu hawa jamaa?

BAKWATA inahusiana vipi na hawa? kuna watu wanaoendesha serikali utawasikia tu " fulani amekemea hili" fulani amekemea lile! kwanza kwa taarifa tu BAKWATA sio chombo cha waislamu wale wapo kwa maslahi yao na matumbo yao! kama ingekuwa ni uwezo waislamu wangeitoa siku nyingi!
 
Back
Top Bottom