Zed
JF-Expert Member
- Mar 28, 2009
- 435
- 257
Nadhani mjadala unakwenda pasipo, haitoshi kumtukana Hamad Rashidi, la kujadili ni kwamba CUF watashirikiana CCM na pengine hata NCCR ingawaje TLP mwenyekiti ameshatoa msimamo wa kukiunga mkono CHADEMA na kubadili kanuni za bunge zitakazo weza kuwa- disadvantage kwa CHADEMA kama kambi rasmi ya upinzani. Cha kujadili ni kwa vipi hili linaweza kuzuilika? Viongozi wa Chadema lazima wafikiri kabla vema strategies zao kabla ya mafisadi wa CCM pamoja na CUF. CCM watalipendana hili sana. Je si vema Chadema wakafanya mazungumzo na TLP na NCCR angalau kuzuia CUF wakishirikiana na CCM kuchakachua kifungu chenye kuipa uhalali Chadema kama kambi rasmi ya upinzani? JF lazima tutambue sasa multiparty politics si jazba bali strategies na sharpness. Isije ikawa kama uchaguzi wa spika na naibu wake...Let us try to strategize here!