Hamad Rashid amesahau 1995 - 2000?

Makubwa,Jamaa hatari sana kumbe alikuwa anajaza mifuko ya suruali na mashati noti zote hizo,lakini kwanza atambue walichokifanya CUF 1995-2000 kuwatosa wenzao hasa NCCR walio kuwa na wabunge 28,hakuna tofauti na wanachofanya CDM,pili yeye sio lazima awe kiongozi CUF ingekuwa na wabunge wengi alikuwa na uhakika gani wa yeye kuendelea kuwa kiongozi au ndio sera zao za kuwa kiongozi milele mpaka aende baburini,maana element hiyo inaonekana CUF,toka wamfukuze mwanzilishi Mzee J.Mapalala mpaka leo hawabadili viongozi kwamba hawana mpinzani,CDM hakuna ulafi bana alikuwapo Mzee Mtei,akaachia,akaja Mzee Makani akaacha,Mbowe sasa hivi.
Hamad kaendelee kula ULOJO.:msela:
 
Huyu HR ni wakuogopa kama ukomo. Mbona katika bunge lililopita mwanzoni CUF iliunda kambi ya upinzani yenyewe tu bila ya kushirikisha chama chochote. Hivi sasa nini kimebadilika? Kwa mwenendo huu, hata kama chadema ilikua na nia ya kushirikisha vyama vingine kwenye kambi yake, ni vema kikasubiri kwanza, uenda yakajitokeza mengi.
 
Sure, ikiwa kila siku yeye ni kuitisha waandishi na kuzungumzia hilohilo haoni kuwa anazidi kuwachefua CDM.
 
Hapa ndipo tunaona umuhimu wa kubadilisha katiba, maana mie nashindwa kuelewa kama CUF bado ni chama cha upinzani. Na hata kama kingekuwa bado ni chama cha upinzani, kwa nini huyu HR anang'ang'ania yeye kuwa inclusive?
Ina maana kuwatumikia wananchi wako mpaka uwe inclusive au waziri kivuli? I don't get it............kuna kitu behind.
 
jamani kamabi ya upinzani ina marupurupu si haba. vikao kila siku, posho mbilimbli na hata tatutatu kila siku na kiongozi wake anatunzwa na serikali kama waziri. kila kikao cha kamati ya uongozi ya bunge anahudhuria, katika kikao cha kupanga shughuli za kila siku za bunge anahudhuri ana posho anatia kibindoni, ukichanganya na posho ya kikao chenyewe cha bunge na kamati zake, utajua hamadi anasumbuliwa na ugonjwa gani. mnadhai hata zito alipolilia cheo kile alikuwa mjinga? hamadi anakumbuka mbali jamani msameheni!
 
Baada ya kuona kuwa kambi ndogo ni kinyume na kanuni za Bunge HR amegeuka tena kukipigia magoti CDM! Kaaaaazi kweli kweli mwaka huu!
 
mimi nakishauri chadema wamchukue mrema peke yake. tlp imeshirikiana chadema moshi vijijini, arusha na maeneo mengine. wanaweza kufanya kazi pamoja. ila cuf kuanzia bungeni walimsusa chadema. hata umeya mwanza waliungana na ccm. sasa watu kama hawa ukiungana nao si watakusaliti? je umoja unalazimishwa au ni hiyari?
 
Kuna maslahi sio mchezo. Kuwa kiongozi wa upinzani unavuta mpunga mzuri sana. Jamaa anatamani sana kwani alishaonja na anajua utamu wake. Sasa Mbowe achague halafu asimchague yeye uone atakavyokuwa mwekundu.
 
Kwa hakika katika maisha yangu sijawahi kuona wala kusikia mwanamke analazimisha kufunga ndoa na wanaume wawili kwa wakati mmoja!! Kama itatokea hiyo itakua ni UCHURO!
 
CUF na HR ni machangudoa wa kisiasa kabisa, mshika mbili moja humponyoka, lazima wachague moja chama tawala au upinzani! Nadhani wanakosa ile nafasi muhimu ya kuzungumza kutoka kambi ya upinzani, sasa walitaka kujificha kwa mwamvuli wa NCCR, TLP na UDP ili watimize azma yao, wamewapoteza wenzao sasa wana mangamanga hovyo kama wendawazimu

Hawa wanafaa kupigwa chini tu bila huruma, lakini chadema wawakubalie, cheyo, kafulila, mkosamali, mrema na yule mama wa NCCR, CUF wapigwe chini
 
jamani kamabi ya upinzani ina marupurupu si haba. vikao kila siku, posho mbilimbli na hata tatutatu kila siku na kiongozi wake anatunzwa na serikali kama waziri. kila kikao cha kamati ya uongozi ya bunge anahudhuria, katika kikao cha kupanga shughuli za kila siku za bunge anahudhuri ana posho anatia kibindoni, ukichanganya na posho ya kikao chenyewe cha bunge na kamati zake, utajua hamadi anasumbuliwa na ugonjwa gani. mnadhai hata zito alipolilia cheo kile alikuwa mjinga? hamadi anakumbuka mbali jamani msameheni!

Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ndiye waziri mkuu kivuli, hivyo anapata
Ofisi pale bungeni Dodoma yenye wafanyakazi 4 na ofisi ndogo Dar es Salaam yenye wafanyakazi 2
Nyumba ya serikali pale Dodoma yenye watumishi wawili na ulinzi 24/7
Gari la serikali lenye hadhi, na dereva/bodyguard, mafuta kumwezesha kuzunguka nchi nzima.
Posho kama ya Waziri Mkuu.
Ndiye mtu wa kwanza kuulizwa swali kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo.
Kipaumbele kwenye safari za nje
etc etc
Sasa yote haya uyakose!, hata ningekuwa mimi, ningeomba kanuni zibadilishwe na kupata japo nusu ya marupurupu haya!

kumbe ndiyo maana mpemba amechanganyikiwa! CDM wasikubali kuungana naye mpaka amewaomba msamaha hadharani.

hata zito ndiyo yanayomchanganya
 
Back
Top Bottom