Hamad rashid alikuwa msaliti kweli?

Jiwe la Ukara

Member
Jul 15, 2011
44
31
Gazeti moja la kila siku liliwahi kuandika kuwa moja ya sababu zilizopelekea kumwengua Mhe. Hamdi Rashidi kwenye nafasi yake ya kuwa Kiongozi wa wabunge wa CUF bungeni ni ukaribu wake na Mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Gazti hilo lilikwenda mbali na kusema kuwa Mhe. Hamad Rashidi alifikia hatua ya kuwa anamdokeza Pinda maswali atakayo muuliza bungeni wkati wa kipindi cha hapo kwa hapo. Kauli ya Pinda ya jana inaelekea kuthibitisha kile kilichoandikwa na gazeti hilo.
Soma hapa:
Gazeti la Majira katika story yake ‘Hamad Rashid amshtaki Nape bungeni’ lilimun kuu Mhe. Hamadi akimuuliza PM kuhusu kauli ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye ya kumkejeli Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Bw. Maalim Seif Sharif Hamad na muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Gazeti la Majira linaandika kuwa “Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alieleza kushangazwa na mbunge huyo kutomweleza suala hilo, kwani ni rafiki yake sana na wamekuwa wakikutana mara nkwa mara.”
Nalo gazeti Tanzania Daima katika habri yake ya ‘Nape, Mchemba washtakiwa kwa Pinda bungeni’ l ikaandika kuwa “ Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alieleza kushangazwa na mbunge huyo kutomweleza suala hilo, kwani ni rafiki yake sana na wamekuwa wakikutana mara kwa mara.”
 
Hamad Rashid hajawahi kuwa msaliti. ametoka kwenye uongozi wa kwa sababu ya mabadiliko ya kisiasa nchini ambapo CHADEMA imekuwa chama kikuu cha upinzani nchini na kuipiku CUF. Hivyo CHADEMA kunyakuwa nafasi zote za uongozi wa kambi ya upinzani.
 
Kwani cheo na madaraka ya Maalim Seif yamo kwenye KATIBA yetu ya JMT? Ni Hamad huyuhuyu alimuuliza Pinda kama Zanzibar ni NCHI. Majibu ya Pinda yaliwaudhi Wazanzibar hadi kesho.
 
Hamad Rashid hajawahi kuwa msaliti. ametoka kwenye uongozi wa kwa sababu ya mabadiliko ya kisiasa nchini ambapo CHADEMA imekuwa chama kikuu cha upinzani nchini na kuipiku CUF. Hivyo CHADEMA kunyakuwa nafasi zote za uongozi wa kambi ya upinzani.

Soma vizuri kaka sina maana ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni..nimesema kiongozi wa wabunge wa CUF.
 
Hamad Rashid hajawahi kuwa msaliti. ametoka kwenye uongozi wa kwa sababu ya mabadiliko ya kisiasa nchini ambapo CHADEMA imekuwa chama kikuu cha upinzani nchini na kuipiku CUF. Hivyo CHADEMA kunyakuwa nafasi zote za uongozi wa kambi ya upinzani.
mwanzisha thread anaongelea uongozi wa wabunge wa CUF bungeni, wewe unaongelea uongozi wa kambi ya upinzani bungeni so ni vizuri uwe unasoma mwanzo hadi mwisho then unarudia tena mara 2 asu zaidi kujiridhisha kwamba umeelewa taarifa.
 
hamad rashid hajawahi kuwa msaliti. Ametoka kwenye uongozi wa kwa sababu ya mabadiliko ya kisiasa nchini ambapo chadema imekuwa chama kikuu cha upinzani nchini na kuipiku cuf. Hivyo chadema kunyakuwa nafasi zote za uongozi wa kambi ya upinzani.

mkubwa soma kwa umakini taalifa kabla hauja comment
 
Back
Top Bottom