Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,500
Mbunge wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani Mhe. Hamad Rashid Mohamed ameteuliwa na kamati tendaji ya chama cha Mabunge duniani (IPU) kuwa mjumbe wa kamati ndogo ya ukaguzi wa ndani kwa mahesabu ya mwaka 2013 ya chama hicho.
Uteuzi huo ulifuatia pendekezo la umoja wa Mabunge ya Afrika lililowasilishwa na katibu mkuu wake Koffi N'Zi tarehe 22 Oktoba, 2012 kufuatia kikao cha wajumbe wa umoja wa Mabunge ya Afrika kumchagua Mhe. Hamad kuwakilisha Afrika kuwania pendekezo hilo mbele ya kamati tendaji ya chama hicho.
Mhe. Hamad Rashid Mohamed, hii ni mara ya pili kuiwakilisha Tanzania na Afrika katika kamati mbalimbali za IPU ambapo mwaka jana katika Mkutano uliofanyika Mjini, Benn, Uswis, alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya IPU cheo ambacho anakitumikia hadi hivi sasa.
Katika kamati hiyo ya ukaguzi wa ndani, Mhe. Hamad Rashid atafanya kazi pamoja na mjumbe mwingine aliyeteuliwa Mhe. Duarte Pacheko kutoka Ureno, ambapo wanatarajia kutoa taarifa ya kazi yao mwaka 2014 katika mkutano mkuu wa IPU
JIWE WALILOKATAA WAASHI LINAPOKUWA JIWE KUU LA PEMBENI