Hamad Rashid aigeukia serikali

bagwell

Senior Member
Sep 19, 2012
113
25
Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed ametoa wito kwa Serikali kuanza kutekeleza miradi kwa muda uliopangwa ili kuokoa nchi kupoteza fedha nyingi bila sababu ya msingi.

Akizungumza na wananchi wa Kibaha wakati wa mahafali ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Vision, Hamad alisema Serikali imekuwa na tatizo la kukamilisha miradi kulingana na wakati, badala yake miradi mingi imekuwa mzigo kutokana na kugharimu fedha nyingi.

Akitolea mfano, Mbunge huyo alisema mradi wa daraja la Kigamboni na Uwanja wa Ndege wa Songwe imekuwa miradi inayogharimu fedha nyingi baada ya kuzembea huko nyuma kuijenga kwa gharama nafuu.

"Kuna tatizo la Watanzania na Serikali yetu kwa ujumla ni kutokwenda na muda, kuna miradi mingi inatufuna pesa nyingi kutokana na uzembe wetu wa kutokimbia na muda, badala yake tunapoanza kuijenga tayari tumechelewa na inatubidi tutumie fedha nyingi," alisema Hamad.

Aliwahasa wanafunzi wanaomaliza shule hiyo kuhakikisha wanajenga tabia ya kukimbia na muda ili kujijenga katika utendaji wao na mara watakapopewa madaraka mbalimbali wataweza kufanya maamuzi kwa haraka.

"Kimbieni na wakati kwa sababu mtakapopewa madaraka mtakuwa na maamuzi sahihi na haraka kwa ajili ya manufaa ya nchi na jamii kwa ujumla," alisema.

Alisema hata Mungu hapendi watu waliogawanyika kwa misingi yoyote iwe ya kidini, kikabila na kiasiasa kwa sababu hawana umoja wa ukweli, hivyo ni vyema Tanzania ibaki kuwa moja kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Katika sherehe hiyo, Hamad aliendesha harambee ya kuchangia mradi wa umeme shuleni hapo na zaidi ya Sh.200,000 zilipatikana na kuahidia kuisadia shule hiyo kwa kuwaombea misaada katika Taasisi na watu binafsi ili kutimiza lengo hilo.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Magesa Kubebika alisema jumla ya wanafunzi 24 wamemaliza masomo yao ya darasa la saba na wanamatumaini wanafunzi wote kuendelea na masomo ya sekondari kama ilivyokuwa mwaka jan
a.
 
Wakaanzishe chama cha mamluki akimjumuisha Kashilila na wengine,...bado anaweweseka kwa kukosa nafasi katik kambia rasmi ya upinzani bungeni.nadhani kasoma upepo na kuona akizozana na CDm muda huu atamalizikia kisiasa.
 
Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed ametoa wito kwa Serikali kuanza kutekeleza miradi kwa muda uliopangwa ili kuokoa nchi kupoteza fedha nyingi bila sababu ya msingi.

Akizungumza na wananchi wa Kibaha wakati wa mahafali ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Vision, Hamad alisema Serikali imekuwa na tatizo la kukamilisha miradi kulingana na wakati, badala yake miradi mingi imekuwa mzigo kutokana na kugharimu fedha nyingi.

Akitolea mfano, Mbunge huyo alisema mradi wa daraja la Kigamboni na Uwanja wa Ndege wa Songwe imekuwa miradi inayogharimu fedha nyingi baada ya kuzembea huko nyuma kuijenga kwa gharama nafuu.

"Kuna tatizo la Watanzania na Serikali yetu kwa ujumla ni kutokwenda na muda, kuna miradi mingi inatufuna pesa nyingi kutokana na uzembe wetu wa kutokimbia na muda, badala yake tunapoanza kuijenga tayari tumechelewa na inatubidi tutumie fedha nyingi," alisema Hamad.

Aliwahasa wanafunzi wanaomaliza shule hiyo kuhakikisha wanajenga tabia ya kukimbia na muda ili kujijenga katika utendaji wao na mara watakapopewa madaraka mbalimbali wataweza kufanya maamuzi kwa haraka.

"Kimbieni na wakati kwa sababu mtakapopewa madaraka mtakuwa na maamuzi sahihi na haraka kwa ajili ya manufaa ya nchi na jamii kwa ujumla," alisema.

Alisema hata Mungu hapendi watu waliogawanyika kwa misingi yoyote iwe ya kidini, kikabila na kiasiasa kwa sababu hawana umoja wa ukweli, hivyo ni vyema Tanzania ibaki kuwa moja kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Katika sherehe hiyo, Hamad aliendesha harambee ya kuchangia mradi wa umeme shuleni hapo na zaidi ya Sh.200,000 zilipatikana na kuahidia kuisadia shule hiyo kwa kuwaombea misaada katika Taasisi na watu binafsi ili kutimiza lengo hilo.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Magesa Kubebika alisema jumla ya wanafunzi 24 wamemaliza masomo yao ya darasa la saba na wanamatumaini wanafunzi wote kuendelea na masomo ya sekondari kama ilivyokuwa mwaka jan
a.
Laki mbili????
 
Back
Top Bottom