Hamad ana wafuasi wengi Tanganyika na Unguja, Seif Anaibeba Pemba

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,599
3,220
GreaThinkers,
Kuna Tetesi ya kutolewa hadharani matokeo ya Uchaguzi 2010 visiwani ambapo kwa tetesi zilizoenea mdogo mdogo ni kuwa Maalim(CUF) alimshinda Shein(CCM) kwa tofaouti ya kura zisizopungua elfu Ishirini ivi(20,000)

Baada ya kikao cha siri baina ya wakubwa hao, kura zilirekebishwa na ule msimamo wa CUF wa kuwa na Serikali tatu ukafia pale pale. Hakuna hakika kama Katiba ya CUF pia imerekebishwa hapa.

Tetesi zinasema CUF inaelekea kumegeka na kuwa kundi kubwa la Hamad ni bara na Unguja huku CUF ya Pemba inamuunga mkono Seif.

Hamad anaweza kuanzisha Chama chake ilaTetesi zinasema pia kuwa anataka kuunga mkono chama kimojawapo chenye nguvu Tanganyika

Je ni kweli akijiunga na chama chenye nguvu Tanganyika atafanikiwa?

Je akianzisha Chama chake atafanikiwa?

Nini maoni yako?
 
Waasisi wa CUF nao wanamuunga mkono Hamad, malengo ya CUF ya awali yamechakachuliwa. Huu U CCM-B unakiua chama chao.
 
Kitu ambacho wengi wetu wanashindwa kuelewa ni kuwa, system ipo kazini kuhakikisha kuwa CUF hawapati majority ya kura za Zanzibar 2015. Seif na Hamad wote wapo kwenye system na hii ni assignment yao ya sasa. Divide and Rule.
 
Hicho chama chake hakiwezi kufanikiwa kwa sababu
  • Mbinu zilizotumika kuidhoofisha CUF ndizo zitakazotumika kukimaliza hicho chama
  • Seif ana lungu la serikali hivyo ni rahisi kumshughulikia Hamad
Suala la kujiunga na upinzani wenye nguvu mfano akirudi CCM atafanikiwa zaidi, CCM ni chama chenye dola na bado kinauwezo wa kuendelea kutawala kutokana na mbinu zake za kuhadaa wapiga kura na kuiba kura.

Suala la kujiunga na CHADEMA ni gumu kwani mitizamo ya Hamad inatofautiana kwa kiasi kikubwa na wana CDM, labda akiri makosa na kutubu hadharani hicho alichopata kulishwa CCM ili akiteme na kumeza vya CDM.
 
Inwezekana kabisa waliahidiwa kupewa urais 2015, ila kumbe CCM-A wanawazid ujanja CCM-B.

CUF inabaki historia, Seif inawezekana alikuwa anatumika nao
 
hivi hamad rashid ameisaidia nini tanzania kama kiongozi,.
Maandamano,
Sikumbuki ni nini hasa alichokifanya kwa Tanzania huyu Hamad ila nakumbuka alikuwa anataka awe kiongozi wa Upinzani Bungeni licha ya kuwa CDM kina wabunge wengi kuliko CUF
 
Maandamano,
Sikumbuki ni nini hasa alichokifanya kwa Tanzania huyu Hamad ila nakumbuka alikuwa anataka awe kiongozi wa Upinzani Bungeni licha ya kuwa CDM kina wabunge wengi kuliko CUF

Kwani Mbowe kaifanyia nini Tanzania? zaidi ya kujineemesha kwa kukopa fedha za wafanyakazi NSSF na kukataa kuzilipa mpaka leo.
 
GreatThinkers,

Kama ambavyo ilitarajiwa ndivyo ilivyotekea,

sasa kinachosubiriwa ni kuanzisha chama cha wananchi (CCW)

Je atafanikiwa?
 
Good strategy would be:

Kuanzisha chama kwa sasa. Kukijenga. 2015 kujiunga na CCM, yaani chama chao kujiunga na CCM.
 
CUF kwisha kazi, wanasiasa wanajua wanachokitafuta, yote tutayapata hapahapa tu, lakini sijafurahishwa na kuvuliwa uanachama kwa sababu eti katangaza kumung'oa kiongozi nafasi aliyonayo. ujinga tu huu
 
Akili yako ina matatizo ya kiakili unahitaji tiba za kiakili zaidi na ushauri wenye akili zaidi utapona kabisa ako kaugonjwa chako cha akili
 
Hapa kazi ipo,
sijajua lile Tamko la WanaCUF Dar na Mtatiro anamuunga mkono Hamad?
 
Maandamano,
Sikumbuki ni nini hasa alichokifanya kwa Tanzania huyu Hamad ila nakumbuka alikuwa anataka awe kiongozi wa Upinzani Bungeni licha ya kuwa CDM kina wabunge wengi kuliko CUF
Hapo kwenye red ndio tatizo la HR. Chama kitakachompokea wajiandae kwa hilo, na hata akianzisha chake hao wafuasi wake waende wakijua hilo.
 
Back
Top Bottom