Halmashauri zisitwae wala kuuza Ardhi.

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Jambo hili la Halmashauri kutwaa na kisha kuziuza tena Ardhi naona ni kinyume cha Katiba yetu na pia ni kinyume cha sheria Mbalimbali. Halmashauri inapotaka kutwaa Ardhi kutoka kwa wananchi ama kutokana na kukua kwa mji au kusudio maalum la matumizi ya Ardhi hiyo hulipa Fidia.

Lakini katiba yetu inasema nini kuhusu haki ya mtu kumiliki mali?

Haki ya kumiliki
mali
Sheria ya 1984Na.15

ib.6 24.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi
zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya
hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.


(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku
kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya
kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria
ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili


Kama katiba inatoa ulinzi wa mali inayomilikiwa na mtu kihalali sijaona kama mtu kumiliki Ardhi ambayo "haijapimwa" ni kinyume cha sheria. Hakuna sheria yoyote ile inayosema ni lazima ardhi ipimwe ndiyo iwe imemilikiwa kihalali. Mtu ananunua ardhi Ekari ishirini kwa mwananchi mwenzake Halmashauri baadaye wanakuja kuitwaa eti kwa sababu haijapimwa, huu si unyang'anyi?

Halmashauri inalipa fidia ya Shilingi 2,000,000 kwa ekari zote 20 kwa kisingizio kwamba ilikuwa ni Ardhi "tupu". lakini baada ya kuipima Ardhi hiyo hiyo, Halmashauri inatoa viwanja 40 kwenye hizo ekari 20 na kuuza kila kiwanja kwa shilingi milioni 2 hadi 4. kwa Hisabati rahisi Halmashauri itapata kati ya shilingi milioni 40 hadi 80. Hii ni haki kweli?

Sheria zetu na sera zetu zinawalinda vipi watu wanaomiliki ardhi kabla ya kupimwa na fidia inayotolewa kwa nini haimwezeshi anayelipwa fidia kununua tena viwanja kwenye eneo lile lile alilolipwa fidia na kuchukuliwa na Halmashauri?
 
Back
Top Bottom