Halmashauri za CHADEMA zaongoza kwa usafi.

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Nimefurahi sana kusikia Halmashauri 3 ambazo ni ngome ya CHADEMA zimeshika nafasi 3 bora katika usafi wa miji na majiji.

Hii inamaanisha, tukitaka miji safi, basi Halmashauri zote ziongozwe na CHADEMA.

1. Mwanza
2. Moshi
3. Arusha

Chanzo: Taarifa ya Habari ya Channel Ten ya saa 1 usiku, tarehe 5 Juni 2012.
 
Hiyo inatokana na Chadema kupata kura nyingi kwa wasomi, sasa nyinyiem wanapata kura kwa wajinga na maskini wakutupa usafi watafanya sa ngapi, watz tubadilike
 
Kuna anayejua vigezo wanavyotumia kuchagua jiji na miji?hapa mwanza kweli wanajitahidi sanasana kwa usafi
 
Chadema yenyewe safi,ila kwa Arusha mhh!!hapo umeniacha mbali,labda kama ni usafi wa mwili na mavazi,ila kwa mazingira arusha ni CHAFU balaa,ukiondoa barabara inayotokea moshi maeneo ya phillips hadi mianzini ndio yenye unafuu,katikati ya mji hapafai.
 
Halmashauri ya jiji la Arusha linaongozwa na Meya feki wa Kichina
 
Chadema yenyewe safi,ila kwa Arusha mhh!!hapo umeniacha mbali,labda kama ni usafi wa mwili na mavazi,ila kwa mazingira arusha ni CHAFU balaa,ukiondoa barabara inayotokea moshi maeneo ya phillips hadi mianzini ndio yenye unafuu,katikati ya mji hapafai.

Pamoja sana kamanda!
Ilitolewa fungu kwa ajili ya usafi wa mazingira, akina Lyimo sijui wameenda kujengea mabaa oloirieni!
 
si unajua hata watu wa hicho chama walivyo wasafi, si kama wale jirani zetu wenye mavazi ya rangi ya bange
 
kiukweli sijabaatika kufika Moshi na Arusha ila Mwanza kwa usafi wanatisha yani mitalo ya maji inapitisha maji masafi kama vile chemchem Halmashauri inagari maalu kwaajili ya kunyonya vumbi barabarani, hongera MWANZA.
 
Chadema yenyewe safi,ila kwa Arusha mhh!!hapo umeniacha mbali,labda kama ni usafi wa mwili na mavazi,ila kwa mazingira arusha ni CHAFU balaa,ukiondoa barabara inayotokea moshi maeneo ya phillips hadi mianzini ndio yenye unafuu,katikati ya mji hapafai.

Arusha bado hawajapata uhuru kamili, ndiyo maana bado kuna kasoro kama hizo. Angekuwa Meya ni wa CHADEMA, hizo kasoro zote zisingekuwapo. Mbali na kasoro hizo, bado wameshika nafasi ya 3; hapo ujue miji mingine ni majalala kabisa!
 
hivi mikoa mingine mnasubiri nini??? chagueni chadema mweze kuona mafanikio si tu kwenye usafi bali kwenye kila sekta.
 
huo ni mwanzo tu mheshimiwa baada ya miaka mitatu au minne ijayo halimashauri karibu zote zitakuwa hivyo, maana zitakuwa zinaongozwa na CHADEMA
 
Hiyo inatokana na Chadema kupata kura nyingi kwa wasomi, sasa nyinyiem wanapata kura kwa wajinga na maskini wakutupa usafi watafanya sa ngapi, watz tubadilike

Haya nimaneno hatari na ya kibaguzi, na tunayalaani
 
Nimefurahi sana kusikia Halmashauri 3 ambazo ni ngome ya CHADEMA zimeshika nafasi 3 bora katika usafi wa miji na majiji.

Hii inamaanisha, tukitaka miji safi, basi Halmashauri zote ziongozwe na CHADEMA.

1. Mwanza
2. Moshi
3. Arusha

Chanzo: Taarifa ya Habari ya Channel Ten ya saa 1 usiku, tarehe 5 Juni 2012.

vp Karatu, Iringa mjin, Mbeya mjini, mbozi magharibi, ubungo, kawe, hai, singida mashariki, kwa zitto...mbona wao hawajitahidi
 
Una kichwa cha panzi nini? Hivi Kawe ni Mji au Jiji? Mbozi Magharibi ni Mji au Jiji? Ebu nikujaribu IQ yako: 2-6=? Najua utajibu haiwezekani!
 
Back
Top Bottom