Halmashauri wezi, wanaifilisi nchi-MREMA

BONGE BONGE

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
3,721
2,106
Wakati Halmashauri za wilaya zikipokea chini ya 23% ya keki ya taifa (77% kwa ajili ya safari za nje ya nchi na mambo mengine kwenye mawizara), ile singo maarufu inayopigiwa upatu na baadhi ya viongozi ambao ama ni wavivu kufikiri kwa makusudi au wanasukumwa na hoja nyepesi pamoja na utashi binafsi ya "Halmashauri kuna Mchwa" imeibuka tena na kupromotiwa; Safari hii ni Augustine Mrema, yule Mwenyekiti aliyechoka; mwenyekiti wa TLP na kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa; Anataka kuwaaminisha watanzania wasio na fikra kwamba umaskini wao unatokana na ama uzembe au Halmashauri hizi kula fedha zao.
Nawasilisha
 
huamini kuwa anaongea ukweli? Ungekuwa unafanya kazi halmashauri bila shaka imani yako ingebadilika wewe. watu wanakamua sana hela huku halmashauri za wilaya.
 
Suala la wizi wa fedha za umma hata huku kahama upo.tunaomba serikali ichunguze halimashauri zetu.watu wanauziwa viwanja hewa,maeneo ya wazi nk.imekuwa kawaida kuona ujenzi ukiendelea kwenye maeneo ya wazi.
 
Back
Top Bottom