Hivi huu utaratibu wa kila halmashauri/municipal kujiwekea viwango tofauti tofauti vya maegesho ya magari wanatupeleka wapi?? mbona hatujulishwi vizuri dhana hii au ni yaleyale? nauliza hivi kwa sababu nimeshuhudia tozo hizi kwenye maeneo mbali mbali tena maeneo mengine ni aibu tupu. unatozwa kodi ya maegesho sehemu ambayo hata ukimuonesha mtu atashanga mfano ngaramtoni arusha tshs 1000 kwa gari pickup, canter 2000, namanga canter 5000, pkup 2500. arusha mjini canter 2500,puck 1000. kwanini viwango siyo sawa? na je maegesho mengine hayafai hata kuuza hela kama hiyo? pabovu sana kwa nini tunaumizwa bila sababu na serekali yetu ni moja?