Halima Mdee Yupo Juu

Asalam Aleikum waungwana. Kwa mara ya kwanza nimemuona kwenye clip kamanda Mdee akimwaga hoja bungeni na I must admit huyu dada yupo makini. Ni kweli machache nijuayo kuhusu yeye najua kwamba ana masters ya laws lakini kuongea kwa ujasiri namna vile huku amezungukwa na wanyonya damu mbumbumbu zaidi ya 200 toka CCM, wabunge wafu kadhaa toka CUF na vibaraka wengine toka NCCR, TLP na UDP si mchezo. Kwa mtazamo wangu, yupo juu zaidi ya Zitto na Mnyika. Kwamba ni yeye binti ni bonus nyingine. NA zaidi nafurahi kuwa ni binti msomi wa kiislamu amabe nina uhakika kwa miaka mingi ijayo atakuwa taa ya kuonyesha njia waislamu kwa wakristo mpaka waje kula mema ya nchi yao siku moja. Atakae muoa huyu, atakuwa ame-hit jack pot.

Huu Mstari umenifanya nitabasamu :
" wabunge wafu kadhaa toka CUF na vibaraka wengine toka NCCR, TLP na UDP si mchezo"
 
Wakati huo kauli kama hizi hazikuleta ukakasi jamvini. Kuna haja ya kubadili mtazamo mzima wa maana ya siasa za vyama kwa CDM kubaki sokoni kwa muda wa kutosha.
 
Ofkoz mbunge wangu Halima Mdee yuko juu. Huwezi kumlinganisha na puppet wa Mbowe Mnyika, au mpenda masifa Zitto. As the matter of fact apart from Slaa, the only asset in that party is Halima Mdee. She just need to be more independent off Mbowe eraticism and less pampous like Tundu Lissu.

Mkuu tupo vitani hivyo tuna makamanda wa aina mbalimbali. Tuna wapiganaji wa angani, ardhini, wanamaji na wasoma ramani. Siasa is very complicated ndio maana Mnyika ni tofauti na Lema pia tofauti na Lissu. Slaa na Mbowe pia wana utofauti. Hii ni kawaida na mchanganyiko huu ndio unaleta mafanikio unayoyaona leo. Wote wakifanana itakuwa monotonous halafu itaboa. Inampasa kila mtu kuwa real that is human nature.
 
Back
Top Bottom