Halima Mdee: Jumba la Mch. Rwakatare nalo libomolewe ili Kuepuka Double Standard!

Huyu mchungaji si ndio yule mwizi wa umeme? Alichukuliwa hatua gani vile?

mchungaji wa kondoo wa bwana wewe unamwita mwizi!!! Ina maana Lwakatare anapingana na kile anachowaelekeza wafuasi mathalani amri ya 7 ya Mungu inayosema USIIBE.
 
tibaijuka anataka kuibomoa lakini rwakatare kashaenda mahakamani kuzuia isibomolewe..na si mnajua mahakama zetu? ukitoa hela pale basi nyumba haivunjwi lakini tibaijuka aliahidi hiyo nyumba itavunjwa sasa rwakatare kaona isiwe taabu kaamua ahamie kabisa aishi humo ndani....msifanye mchezo na hela bongo hapa
 
Hili nalo neno. Ila atajitetea shule zake.

vyote hivyo; sule, sadaka Ngo yake ya watoto yatima fedha za ubunge nk. ndo hivo tena anawaambia waumini watafute ufalme wa mbinguni wampe Mungu kilicho chake naye anapata humo humo sijui wamini nao wanaambulia ...
 
Naunga mkono 100% Libomolewe tuu! sheria msumeno bana.

Mkuu sheria msumeno si hapa Tz. Tumeona siku zote nyumba za maskini zinabomolewa bila hata kujiuliza mara mbili lakini ikifika kwa serikali au matajiri sheria usita kidogo. Tumeona jinsi jengo la Tanesco lilivyoleta kizaazaa baada ya Magufuli kusema lipo barabarani nalo libomolewe kama nyumba nyingine za wananchi maskini!

Ni hapo tutakapokuwa na utawala wa sheria ndo maana ya neno "Sheria ni msumeno" litatimia.

 
Na Hotel ya Golden Tulip pale ilipo ni sawa? Labda sheria ibadilishwe vinginevyo watekelezaji wataendelea kupepesa macho kutegea mhusika.
 
Naunga mkono kubomolewa nyumba,kama ni kweli ilijengwa kinyume cha sheria
 
Wakati hii nyumba inajengwa diwani wa hii kata alikuwa wapi? Huyu mama alijenga hii nyumba kwa kiburi maana aliandikiwa barua za onyo yeye akadharau kisa, alishalizwa hela tayari na tapeli. Kalizwa hela sawa lakini hili si kosa la serikali inabidi abomolewe ili haki itendeke.
 
To my knowledge sio kazi ya Nemc kugawa viwanja...so mtu mwenye akili atafanya search mwenyewe kujua eneo analojenga nyumba ya dhamani kama hii ni salama kisheria[/QUOTE]

Ni kweli si kazi ya NEMC kugawa viwanja ila mamlaka za serikali (idara ya ardhi na mipango miji) wanatakiwa wawe wamepima viwanja vya kutosha na mwananchi jukumu lake ni kuhakikisha mchoro wa nyumba yake umepitishwa na idara husika na kupewa building permit kama sheria ya mipango miji inavyotaka i.e. Township (Building) Rules, Cap. 101. Na si kumwachia mtu afanye search mwenyewe bila mamlaka zinazohusika kuruhusu ujenzi uendelee. Tatizo kwa Dar ni kubwa sana kwa kuwa watu wanabadilisha matumizi ya ardhi bila kufuata taratibu za kutoa matangazo ikiwa pamoja na kubandika bango la kizushi kwenye kiwanja ili mwananchi yeyote mwenye pingamizi atoe. tukirudi kwenye NEMC wao hawagawi viwanja ila kazi yao ni kufuatilia kama kanuni za mazingira zimefuatwa hivyo wakiibuka sehemu na kugundua kitu maana yake lazima upande mmoja uumie ikiwa na maana kama serikali iliruhusu kibali cha ujenzi huku ikijua kuna athari ktk mazingira (watendaji wa serikali wanapigwa adhabu though serikali yetu sikivu huwa haitekelezi adhabu kwa watumishi wake) na bado nyumba itavunjwa based on sheria za mazingira (yananufaisha wengi) alafu na wao wataangaliana na mteja wao sasa kuona nini cha kufanya. Mpaka NEMC wanagundua tatizo maana yake ardhi na mipango miji wamelala hivyo hata kuchukua hatua inakuwa ngumu.
 
hawa ndio watu wanaoharibu image ya ukiristu sasa mchungaji mvunja maadili mlafi wa madaraka, mpenda rushwa yaani huyu mama ana kila sifa za kuharibu maadili ya kichungaji nashangaa mpaka sasa wachungaji mko wapi na maaskofu kumfuta huyu lwakatare kwenye jumuia yenu kunusuru muonekano wa kikiristo
 
To my knowledge sio kazi ya Nemc kugawa viwanja...so mtu mwenye akili atafanya search mwenyewe kujua eneo analojenga nyumba ya dhamani kama hii ni salama kisheria[/QUOTE]

Ni kweli si kazi ya NEMC kugawa viwanja ila mamlaka za serikali (idara ya ardhi na mipango miji) wanatakiwa wawe wamepima viwanja vya kutosha na mwananchi jukumu lake ni kuhakikisha mchoro wa nyumba yake umepitishwa na idara husika na kupewa building permit kama sheria ya mipango miji inavyotaka i.e. Township (Building) Rules, Cap. 101. Na si kumwachia mtu afanye search mwenyewe bila mamlaka zinazohusika kuruhusu ujenzi uendelee. Tatizo kwa Dar ni kubwa sana kwa kuwa watu wanabadilisha matumizi ya ardhi bila kufuata taratibu za kutoa matangazo ikiwa pamoja na kubandika bango la kizushi kwenye kiwanja ili mwananchi yeyote mwenye pingamizi atoe. tukirudi kwenye NEMC wao hawagawi viwanja ila kazi yao ni kufuatilia kama kanuni za mazingira zimefuatwa hivyo wakiibuka sehemu na kugundua kitu maana yake lazima upande mmoja uumie ikiwa na maana kama serikali iliruhusu kibali cha ujenzi huku ikijua kuna athari ktk mazingira (watendaji wa serikali wanapigwa adhabu though serikali yetu sikivu huwa haitekelezi adhabu kwa watumishi wake) na bado nyumba itavunjwa based on sheria za mazingira (yananufaisha wengi) alafu na wao wataangaliana na mteja wao sasa kuona nini cha kufanya. Mpaka NEMC wanagundua tatizo maana yake ardhi na mipango miji wamelala hivyo hata kuchukua hatua inakuwa ngumu.
hawa nemc nao wakifuatilia saana wanahofia usalama wao maana hapa wanadili na fisadi mkubwa mwenye ulinzi nje na ndani ya ikulu mwishowe mtasikia maafisa wa NEMC wamepelekwa kuleeee mabwe pande
 
Huyu mama umri wake ulipaswa kujenga nyumba ndogo yenye kupunguza ghrama na mihangaiko ya kumaintain ktk umri huu wazee huibiwa na wafanyakazi kutoroka au hata kupekea hel ya kazi wasioyfanya.
 
Frank Mushi na yule Ringo, ana mtoto ambaye ni pilot, ni matapeli wakubwa wa viwanja Tanzania. Inasikitisha kuona ya kuwa Mchungaji anashirikiana na mtu kama Mushi.
 
WARAKA WA MHE HALIMA MDEE KWA MEDIA

Hivi karibuni Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa walitoa tamko kwamba nyumba zote zilizojengwa kando kando ya fukwe za bahari na mito zitabomolewa, bila wamiliki kulipwa fidia kutokana na kukiuka Sheria za Ardhi na Mazingira za mwaka 1992, 1995 na 2004.
Kauli hiyo ilitokana na ukweli kwamba imekuwa ni jambo la kawaida kwa watu wenye nguvu ya fedha kuharibu mazingira kwa makusudi pasipo kujali athari ambazo zinaweza kutokea sasa na baadae kwa wakazi wa maeneo husika, jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla! Kwa watu wengi, kauli ya mawaziri hao ilionekana kama ni hatua muhimu sana katika kulinda mazingira ya fukwe zetu na jamii nzima hasa kutokana na umuhimu wa kulinda mazingira katika wakati huu wa athari za mabadiliko ya tabia nchi. Lakini baadhi yetu tuliona kama ni mwendelezo wa kauli za Serikali ambazo utekelezaji wake ama huwa ni wa mashaka au ukitekelezwa basi utekelezaji wake hutawaliwa na upendeleo wa hali ya juu kwa watu wenye fedha na nafasi kubwa serikalini (vigogo). Moja kati ya nyumba iliyotakiwa kubomolewa imejengwa kwenye viwanja namba 2019-2020 Kawe Beach, katika fukwe za Bahari ya Hindi. Viwanja ambavyo vilipatikana kwa ushirikiano wa Mchungaji Lwakatare na tapeli maarufu wa Ardhi jijini Dar es salaam, anayejulikana kwa jina la Frank Mushi. Ikumbukwe kwamba katikati ya mwezi Julai, 2012 wananchi waliojenga nyumba katika maeneo yanayosemekana ni tengefu ya Jangwani Beach, Mto Ndumbwi na Mto Mbezi walivunjiwa nyumba katika operesheni iliyoendeshwa na Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC). Operesheni ambayo ilihusisha takriban nyumba 15 na kuta ( fences) 8. Katika nyumba hizo, mojawapo iliyotakiwa kuvunjwa ni ya Mchungaji Getruda Lwakatare. Lakini kwa sababu ambazo wahusika, akiwemo yeye mwenyewe na serikali, wanazifahamu, nyumba yake haikuguswa! Wakati wananchi wanaofahamu ukweli wa mambo, wakiwa bado wanahoji chinichini juu ya upendeleo wa kitabaka ulio wazi, hivi karibuni wameshuhudia kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari, ikiripotiwa kuwa Mchungaji Lwakatare (Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God na Mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ) amehamia kwenye nyumba yake mpya. Nyumba ambayo ilipaswa kuwa imebomolewa kwa sababu imejengwa kwenye viwanja ambavyo ni kinyume cha sheria kujenga katika maeneo hayo. Kuvunja sheria kwa uwazi namna hii, huku wengine wakichukuliwa hatua kwa kuvunja sheria hiyo hiyo, si tu ni ’double standards’, bali kunaweza kutafsiriwa ni kuitia serikali mfukoni. Kitu kibaya zaidi ni kwamba kiongozi huyo alishataarifiwa tangu mapema juu ya ubatili wa kujenga katika eneo hilo, kupitia kwa huyo Frank Mushi kabla hata ujenzi wa nyumba hiyo haujaanza. Ikumbukwe pia kuwa viwanja hivyo vilipatikana na ujenzi huo kuwezekana baada ya eneo la bahari na mto kujazwa kifusi na mawe! Kwa kutambua kuwa kuendelea na ujenzi katika eneo hilo ni kuvunja sheria za nchi zinazohusu utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya jamii nzima, Mchungaji Lwakatare aliendelea kwa kujiificha nyuma ya mgongo wa huyo Mushi, akijifanya hahusiki kabisa na kilichokuwa kikiendelea katika eneo husika. Uthibitisho wa ubatili wa kujenga katika viwanja husika: 1) Tarehe 4/1/2011 Wizara ya Ardhi kupitia barua yenye Kum. Namba LD/297571/18 waliandika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuhusiana na uvamizi wa kiwanja nana 2019 na 2020 Mbezi Kawe. Barua husika pamoja na mambo mengine ilibainisha kwamba wizara imefanya ukaguzi katika viwanja tajwa, baada ya kupata malalamiko juu ya uharibifu wa mazingira unaoendelea katika eneo hilo. Na kwamba ukaguzi walioufanya umeonesha kuwa ujenzi unaofanyika katika eneo husika hauruhusiwi na unakiuka Tangazo la Serikali (GN) No. 76 ya mwaka 1992. Kupitia barua hiyo, wizara ilimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuchukua hatua za kubomoa/kuondoa uendelezaji batili uliokuwa ukifanyika katika viwanja Na 2019 na 2020 Mbezi Kawe. Barua hiyo ilisainiwa na Bwana Sadoth K. Kyaruzi, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara. 2) Uthibitisho mwingine ni barua ya tarehe 30/9/2011 kutoka NEMC kwenda kwa Bwana Frank Mushi. Barua husika, ilitoa maelekezo kwa Mushi kuvirudisha katika hali yake ya kawaida, viwanja namba 2019-2020 kwa mujibu wa vifungu 55(2) (a) (e), (3) na 151 (1) ,(2) (a), (b), (3) ,(4) (b) na (f) vya Sheria ya Mazingira, sura 191 ya mwaka 2004. Barua husika inabainisha kwamba timu ya wataalam toka Baraza la Mazingira (NEMC), Wizara ya Maji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam na Manispaa ya Kinondoni ilitembelea eneo husika kufuatia malalamiko kutoka kwa viongozi na wakazi wa Kawe Beach. Timu hiyo ilibaini kwamba eneo la Mto Ndumbwi, pamoja na bahari lilikuwa linajazwa mawe na vifusi hali iliyosababisha kupatikana kwa viwanja na 2019 na 2020. Ambapo ndani ya viwanja hivyo lilikuwa linajengwa jumba kubwa kinyume kabisa na vifungu 55(2)(a) , 55(2) (b) , 55(2)(d) na 55(2)(e) vya Sheria ya Mazingira. Ilibainika pia kuwa mikoko ilikatwa kinyume na s.63(1) ya Sheria ya Mazingira. Kwa mujibu wa nyaraka nilizonazo, yafuatayo yalijitokeza i) Timu ya wataalam ilibaini kwamba, tayari Wizara ya Maliasili na Utalii ilishatoa zuio la ujenzi katika eneo husika. ii) Manispaa ya Kinondoni, mara kadhaa iliweka zuio la uendelezaji na kutoa amri kwa ’mmiliki’ wa eneo husika kubomoa, lakini mmiliki huyo alipuuza amri hiyo na kuendelea na ujenzi! iii) Ilitolewa amri ya Mahakama, tarehe 5/4/2011 kumtaka Bwana Mushi asiendelee na ujenzi. Amri hiyo ilipuuzwa na ujenzi ukaendelea. Baraza la Mazingira lilimwagiza tena, Bwana Mushi:-2) Kuvunja majengo yote yaliyoko kwenye viwanja vyenye mgogoro. 3) Ndani ya siku saba, tokea amri husika kutolewa (amri ilitolewa 30/9/2011) awe ametoa mawe na vifusi vyote vilivyoharibu mkondo wa maji na bahari na kuurudisha mto na bahari katika hali yake ya kawaida. 4) Ndani ya siku 30 chini ya usimamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha kwamba mikoko yote iliyokatwa imerudishwa katika hali iliyokuwa awali. Kwa gharama za Bwana Mushi. Licha ya amri zote hizo, mazuio yote hayo, matamko ya mawaziri yaliyotawaliwa na mbwembwe nyingi, ujenzi uliendelea, nyumba imekamilika. Sasa inatumika. Wakati kigogo huyo amehamia kwenye nyumba yake kwa matangazo na mbwembwe, Mto Ndumbwi, bahari na mazingira kwa ujumla yameharibiwa vibaya! Bila kusahau kuwa wananchi wengine wamebomolewa nyumba zao kwa kutumia sheria hizo hizo. Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira, Sura 191 ya mwaka 2004, Fungu 57(1) hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za kudumu za kibinadamu ndani ya mita 60 ambazo kwa asili yake zinaweza kuhatarisha au kuathiri vibaya ulinzi na utunzaji wa mazingira, utunzaji wa bahari, kingo za mto, bwawa au mwambao wa asili wa ziwa. Halikadhalika, Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 ( Sura 113) Fungu 7 (1) (d) inabainisha kwamba eneo lolote lililo ndani ya mita 60 kutoka kingo ya mto na bahari linatakiwa kutangazwa kama ardhi hatari au kuhifadhiwa. Na pale inapotokea kuwa masharti ya sheria moja yanapingana na masharti ya Sheria ya Mazingira, kuhusu mambo yanayohusu usimamizi wa mazingira, Sheria ya Mazingira ndiyo hutumika, kwa mujibu wa Fungu 232 la sheria ya mazingira sura Kutokana na hali hii serikali inatakiwa kujinasua katika mwendelezo wa tafsiri wanayoipata wananchi kuwa imetekwa na kuwekwa mfukoni na watu wachache wenye uwezo. Maana wanaona kuwa huu ni mwendelezo wa serikali kuwa na kigugumizi pale sheria zinapovunjwa na vigogo serikalini au watu wenye fedha wanaoshirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali na chama tawala kufanya ufisadi. Wameona mambo ya namna hii mara kadhaa, ikiwemo serikali kushindwa kuwachukulia hatua waliohusika na kashfa kubwa za ufisadi kama ’akina’ Kagoda na wenzake (EPA), Richmond na kashfa nyingine nyingi. Kwamba sasa inazidi kuonekana dhahiri kuwa kuna watu wako juu ya sheria za nchi, huku wanyonge wakishughulikiwa. Ni wakati mwafaka sasa kwa mawaziri wanaohusika na masuala ya ardhi na mazingira kuwaeleza Watanzania kulikoni wananchi wa hali ya chini kuvunjiwa nyumba zao kwa kigezo cha kuvunja sheria wakati huo huo Mchungaji Lwakatare (kigogo) ambaye uharibifu wake ni wa hatari kuliko hata hao waliovunjiwa akitamba mtaani kwamba yeye yuko juu ya sheria na hakuna mamlaka yoyote yenye uwezo wa kumzuia kufanya alichofanya! Ni aibu kwa Taifa kuwa na viongozi wa aina hii! Viongozi ambao wako tayari kutumia fedha, hila, mamlaka na dhamana za uongozi walizopewa, kuhalalisha haramu, ni janga kwa mstakabali wa taifa letu! Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Imetolewa Dar es Salaam na; Halima Mdee (MB)

Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi
 
Back
Top Bottom