Halima Mdee: Jumba la Mch. Rwakatare nalo libomolewe ili Kuepuka Double Standard!

Huyo ana vibali vyote vya kujenga hiyo nyumba, kwahiyo kabla ya kubomoa Serikali iwashughulikie kwanza waliompa ruhusa ya kujenga, na kwanini hawakusimamisha ujenzi wakati unaanza wanasubiri mpaka mtu anahamia?

....ignorance ya sheria isiwe na haiwezi kuwa excuse ya kuliacha hilo jengo..........
...pili....pamoja na kubomolewa huko....waliotowa vibali eneo husika wawajibishwe.....ili iwe fundisho kwa wengine.....
 
Labda Lwakatare ahamie chadema ndo litabomolewa
Nakubaliana nawe mkuu!.. Ndiyo maana Sumaye alipokuwa waziri mkuu aliwaambia watu wa kilimanjaro, "mkitaka biashara ziwaendee vizuri hamia CCM!" Kwa msingi huu hata biashara haramu au shughuli maeneo yasiyoruhusiwa yakisindikizwa na bendera ni salama 100%.
 
Halima Mdee? Kwanini Usilalamikie UFISADI na Uende kumshurutisha RAIS na WAZIRI MKUU ?Hapo tutaona Umefanya kazi ya HAKI na kweli Unapenda NCHI YAKO... SIO KIJENGO KIMOJA unaona Walaaaaaaaaa
Huu wenyewe ni ufisadi. Unataka azungumzie nini mkuu?
 
Halima mdee acha wivu usiyo na maana, politics is not played in that way.You are still very young to fight for such a nice house, kwa nini usiseme jengo tanesco lililotangazwa na Magufiri kuvunjwa ambalo ni dhahiri limevunja sheria livunjwe?Wananchi wa madale waliovunjiwa nyumba zao ukaenda kuwadanganya kuwa ungewasaidia, hadi leo ni miaka miwili hujatoa msaada wowote wa mali au kisheria wapate haki zao.Leo unataka kuongeza umaskini kwa kushauri pia nyumba wa Mch. Rwakatale ivunjwe!! What kind of a politician are U?Wanasiasa wa bongo kweli vimeo, kweli Kawe tumejifunza, nadhani hatutarudia kufanya makosa
Kwa hiyo wewe unataka viongozi waendelee kuwa juu ya sheria? Kwa nini nyumba za eneo moja zibomolewe lakini ya mtu mmoja ilindwe? Hapa utetezi unatakiwa kutolenga kulinda uzuri wa nyumba. Kwani wanaobomolewa si watu? Ila akibomolewa Rwakatare umaskini unaingia!. Umejaribu kujipima wewe na mdee nani kimeo? Kwa hiyo mwanasiasa ili akufurahishe ni lazima apiganie jengo la Tanesco libomolewe?
 
kwanini yeye kama mbunge aliyechaguliwa na waatu anaogopa kushikilia msimamo na kuomb jumba libomolewe? kwanini amekaa kimya muda wote? kwa nini anaogopa kutaja jina la huyo mtu kama ni kweli?na yeyy ni cdm akichaguliwa tena au kuingia serikalini watabeba watu hivyo hivyo.nikiona ameshikilia haswaaaaaaaaaa basi nitajua kweli yeye anapenda watu wa kawe.Shame kwa viongozi wote na yeye aliyekaa na kuona jengo linakamilika ndio anakuja kuongea, nakerwa nikiwa kama mwanachi. eti sasa ndio anaongea na hakuna hata msimamo wa yeye kuomba serikali ibomoe anakuwa kama anaogopa eti inaonekana hivi au vile...
Kwa hiyo jimbo hilo ungepewa wewe, ungeweza kujua nyumba zooote zinazojengwa kinyume na sheria?. Ni miaka mingapi imepita tangu Mdee awe mbunge wa kawe? Mamlaka zinazohusika zilikuwa wapi?
 
Kwani waliobomolewa walikuwa walala hoi? au hatujui maana ya mlalahoi........!

Waambie mkuu. Mlalahoi hawamjui kabisa. Ukiwa na uwezo wa kujenga nyumba wewe si mlalahoi. Labda kama ni kibanda cha maboksi na magunia . Lakini nyumba zilizokuwa pale hazikuwa za namna hiyo. Tafuteni maana sahihi ya mlala hoi.
 
Lwakatare-na-Halima-Mdee.jpg

Serikali imetakiwa kumdhibiti na kumuondoa, kisha kuibomoa nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mchungaji Getrude Lwakatare.

Rai hiyo imetolewa na Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.

Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa, wakati raia wengine wakibomolewa nyumba ambazo kama ilivyo ya Mchungaji Lwakatare, zilijengwa kinyume cha sheria, Mbunge huyo amehamia na kuishi kwenye nyumba yake.

Julai mwaka huu, nyumba za wananchi waliojenga katika maeneo tengefu ya ufukwe wa Jangwani, mto Ndumbwi na mto Mbezi, zilibomolewa katika operesheni iliyoendeshwa na Baraza la Mazingira la Taifa (Nemc).

Operesheni hiyo ilihusisha takriban nyumba 15 na kuta nane. Lakini cha kushangaza nyumba ya Mchungaji Lwakatare ambayo imejengwa kinyume cha sheria haikuguswa[/QUOTE

Double standards!!
 
The business of God, nimeapa hakuna mchungaji atakaepokea sadaka yangu, unless it is under unavoidable circumstances.
 
ndio maana kakobe kajiendea kujitafutia makazi marekani kwa obama! kakusanya dhahabu za watu weeeeeee, sasa kawaacha wanasikiliza cd, mwenye we yuko kwa obama anakula good-tym bila hofu ya kubomolewa nyumba, lol!
 
KWA MUJIBU WA KAZI YANGU NA MAADILI NILIYONAYO 'double std' ni uchafu usiovumilika. Wote, anayetoa kibali fake na anayepokea au kutafuta kibali fake kwa kujua au kutojua wako hatiani.

Verdict:

APEWE NOTISI YA KUBOMOA NYUMBA, MUDA ALIOPEWA UKIISHA, IBOMOLEWE NA ALIPE GHARAMA HUSIKA ZA KUBOMOWA NA KUSAWAZISHA ENEO. WALIOTOA VIBALI WOTE WAWAJIBISHWE KWA MUJIBU WA MIKATABA YA AJIRA ZAO.
 
Heee!arooooo,tutafika kwa style hii?hawa wachungaji hawa


ndio maana kakobe kajiendea kujitafutia makazi marekani kwa obama! kakusanya dhahabu za watu weeeeeee, sasa kawaacha wanasikiliza cd, mwenye we yuko kwa obama anakula good-tym bila hofu ya kubomolewa nyumba, lol!
 
who will speak if u wont? who will speak 4 the voiceless 4 their voice to be heard? Halima has exercised her freedom of speech. She should be taken as a brave among thousands who knew the scandal but haven't spoken anything. I meritoriously concur with her.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI VIONGOZI AINA YA MCHUNGAJI GETRUDE LWAKATARE NI AIBU KWA TAIFA Hivi karibuni Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa walitoa tamko kwamba nyumba zote zilizojengwa kando kando ya fukwe za bahari na mito zitabomolewa, bila wamiliki kulipwa fidia kutokana na kukiuka Sheria za Ardhi na Mazingira za mwaka 1992, 1995 na 2004.

Kauli hiyo ilitokana na ukweli kwamba imekuwa ni jambo la kawaida kwa watu wenye nguvu ya fedha kuharibu mazingira kwa makusudi pasipo kujali athari ambazo zinaweza kutokea sasa na baadae kwa wakazi wa maeneo husika, jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla! Kwa watu wengi, kauli ya mawaziri hao ilionekana kama ni hatua muhimu sana katika kulinda mazingira ya fukwe zetu na jamii nzima hasa kutokana na umuhimu wa kulinda mazingira katika wakati huu wa athari za mabadiliko ya tabianchi.

Lakini baadhi yetu tuliona kama ni mwendelezo wa kauli za Serikali ambazo utekelezaji wake ama huwa ni wa mashaka au ukitekelezwa basi utekelezaji wake hutawaliwa na upendeleo wa hali ya juu kwa watu wenye fedha na nafasi kubwa serikalini (vigogo).

Moja kati ya nyumba iliyotakiwa kubomolewa imejengwa kwenye viwanja namba 2019-2020 Kawe Beach, katika fukwe za Bahari ya Hindi.

Viwanja ambavyo vilipatikana kwa ushirikiano wa Mchungaji Lwakatare na tapeli maarufu wa Ardhi jijini Dar es salaam, anayejulikana kwa jina la Frank Mushi.

Ikumbukwe kwamba katikati ya mwezi Julai, 2012 wananchi waliojenga nyumba katika maeneo yanayosemekana ni tengefu ya Jangwani Beach, Mto Ndumbwi na Mto Mbezi walivunjiwa nyumba katika operesheni iliyoendeshwa na Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC).

Operesheni ambayo ilihusisha takriban nyumba 15 na kuta ( fences) 8. Katika nyumba hizo, mojawapo iliyotakiwa kuvunjwa ni ya Mchungaji Getruda Lwakatare.

Lakini kwa sababu ambazo wahusika, akiwemo yeye mwenyewe na serikali, wanazifahamu, nyumba yake haikuguswa! Wakati wananchi wanaofahamu ukweli wa mambo, wakiwa bado wanahoji chinichini juu ya upendeleo wa kitabaka ulio wazi, hivi karibuni wameshuhudia kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari, ikiripotiwa kuwa Mchungaji Lwakatare (Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God na Mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ) amehamia kwenye nyumba yake mpya.

Nyumba ambayo ilipaswa kuwa imebomolewa kwa sababu imejengwa kwenye viwanja ambavyo ni kinyume cha sheria kujenga katika maeneo hayo.

Kuvunja sheria kwa uwazi namna hii, huku wengine wakichukuliwa hatua kwa kuvunja sheria hiyo hiyo, si tu ni 'double standards', bali kunaweza kutafsiriwa ni kuitia serikali mfukoni.

Kitu kibaya zaidi ni kwamba kiongozi huyo alishataarifiwa tangu mapema juu ya ubatili wa kujenga katika eneo hilo, kupitia kwa huyo Frank Mushi kabla hata ujenzi wa nyumba hiyo haujaanza.

Ikumbukwe pia kuwa viwanja hivyo vilipatikana na ujenzi huo kuwezekana baada ya eneo la bahari na mto kujazwa kifusi na mawe! Kwa kutambua kuwa kuendelea na ujenzi katika eneo hilo ni kuvunja sheria za nchi zinazohusu utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya jamii nzima, Mchungaji Lwakatare aliendelea kwa kujiificha nyuma ya mgongo wa huyo Mushi, akijifanya hahusiki kabisa na kilichokuwa kikiendelea katika eneo husika.

Uthibitisho wa ubatili wa kujenga katika viwanja husika: 1) Tarehe 4/1/2011 Wizara ya Ardhi kupitia barua yenye Kum. Namba LD/297571/18 waliandika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuhusiana na uvamizi wa kiwanja nana 2019 na 2020 Mbezi Kawe.

Barua husika pamoja na mambo mengine ilibainisha kwamba wizara imefanya ukaguzi katika viwanja tajwa, baada ya kupata malalamiko juu ya uharibifu wa mazingira unaoendelea katika eneo hilo.

Na kwamba ukaguzi walioufanya umeonesha kuwa ujenzi unaofanyika katika eneo husika hauruhusiwi na unakiuka Tangazo la Serikali (GN) No. 76 ya mwaka 1992.

Kupitia barua hiyo, wizara ilimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuchukua hatua za kubomoa/kuondoa uendelezaji batili uliokuwa ukifanyika katika viwanja Na 2019 na 2020 Mbezi Kawe.

Barua hiyo ilisainiwa na Bwana Sadoth K. Kyaruzi, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara. 2) Uthibitisho mwingine ni barua ya tarehe 30/9/2011 kutoka NEMC kwenda kwa Bwana Frank Mushi.

Barua husika, ilitoa maelekezo kwa Mushi kuvirudisha katika hali yake ya kawaida, viwanja namba 2019-2020 kwa mujibu wa vifungu 55(2) (a) (e), (3) na 151 (1) ,(2) (a), (b), (3) ,(4) (b) na (f) vya Sheria ya Mazingira, sura 191 ya mwaka 2004.

Barua husika inabainisha kwamba timu ya wataalam toka Baraza la Mazingira (NEMC), Wizara ya Maji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam na Manispaa ya Kinondoni ilitembelea eneo husika kufuatia malalamiko kutoka kwa viongozi na wakazi wa Kawe Beach.

Timu hiyo ilibaini kwamba eneo la Mto Ndumbwi, pamoja na bahari lilikuwa linajazwa mawe na vifusi hali iliyosababisha kupatikana kwa viwanja na 2019 na 2020.

Ambapo ndani ya viwanja hivyo lilikuwa linajengwa jumba kubwa kinyume kabisa na vifungu 55(2)(a) , 55(2) (b) , 55(2)(d) na 55(2)(e) vya Sheria ya Mazingira. Ilibainika pia kuwa mikoko ilikatwa kinyume na s.63(1) ya Sheria ya Mazingira.

Kwa mujibu wa nyaraka nilizonazo, yafuatayo yalijitokeza i) Timu ya wataalam ilibaini kwamba, tayari Wizara ya Maliasili na Utalii ilishatoa zuio la ujenzi katika eneo husika. ii) Manispaa ya Kinondoni, mara kadhaa iliweka zuio la uendelezaji na kutoa amri kwa 'mmiliki' wa eneo husika kubomoa, lakini mmiliki huyo alipuuza amri hiyo na kuendelea na ujenzi! iii) Ilitolewa amri ya Mahakama, tarehe 5/4/2011 kumtaka Bwana Mushi asiendelee na ujenzi.


Amri hiyo ilipuuzwa na ujenzi ukaendelea. Baraza la Mazingira lilimwagiza tena, Bwana Mushi:- 2) Kuvunja majengo yote yaliyoko kwenye viwanja vyenye mgogoro. 3) Ndani ya siku saba, tokea amri husika kutolewa (amri ilitolewa 30/9/2011) awe ametoa mawe na vifusi vyote vilivyoharibu mkondo wa maji na bahari na kuurudisha mto na bahari katika hali yake ya kawaida. 4) Ndani ya siku 30 chini ya usimamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha kwamba mikoko yote iliyokatwa imerudishwa katika hali iliyokuwa awali.

Kwa gharama za Bwana Mushi. Licha ya amri zote hizo, mazuio yote hayo, matamko ya mawaziri yaliyotawaliwa na mbwembwe nyingi, ujenzi uliendelea, nyumba imekamilika. Sasa inatumika.

Wakati kigogo huyo amehamia kwenye nyumba yake kwa matangazo na mbwembwe, Mto Ndumbwi, bahari na mazingira kwa ujumla yameharibiwa vibaya! Bila kusahau kuwa wananchi wengine wamebomolewa nyumba zao kwa kutumia sheria hizo hizo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira, Sura 191 ya mwaka 2004, Fungu 57(1) hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za kudumu za kibinadamu ndani ya mita 60 ambazo kwa asili yake zinaweza kuhatarisha au kuathiri vibaya ulinzi na utunzaji wa mazingira, utunzaji wa bahari, kingo za mto, bwawa au mwambao wa asili wa ziwa. Halikadhalika,

Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 ( Sura 113) Fungu 7 (1) (d) inabainisha kwamba eneo lolote lililo ndani ya mita 60 kutoka kingo ya mto na bahari linatakiwa kutangazwa kama ardhi hatari au kuhifadhiwa.

Na pale inapotokea kuwa masharti ya sheria moja yanapingana na masharti ya Sheria ya Mazingira, kuhusu mambo yanayohusu usimamizi wa mazingira, Sheria ya Mazingira ndiyo hutumika, kwa mujibu wa Fungu 232 la sheria ya mazingira sura Kutokana na hali hii serikali inatakiwa kujinasua katika mwendelezo wa tafsiri wanayoipata wananchi kuwa imetekwa na kuwekwa mfukoni na watu wachache wenye uwezo.

Maana wanaona kuwa huu ni mwendelezo wa serikali kuwa na kigugumizi pale sheria zinapovunjwa na vigogo serikalini au watu wenye fedha wanaoshirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali na chama tawala kufanya ufisadi.

Wameona mambo ya namna hii mara kadhaa, ikiwemo serikali kushindwa kuwachukulia hatua waliohusika na kashfa kubwa za ufisadi kama 'akina' Kagoda na wenzake (EPA), Richmond na kashfa nyingine nyingi.

Kwamba sasa inazidi kuonekana dhahiri kuwa kuna watu wako juu ya sheria za nchi, huku wanyonge wakishughulikiwa.

Ni wakati mwafaka sasa kwa mawaziri wanaohusika na masuala ya ardhi na mazingira kuwaeleza Watanzania kulikoni wananchi wa hali ya chini kuvunjiwa nyumba zao kwa kigezo cha kuvunja sheria wakati huo huo Mchungaji Lwakatare (kigogo) ambaye uharibifu wake ni wa hatari kuliko hata hao waliovunjiwa akitamba mtaani kwamba yeye yuko juu ya sheria na hakuna mamlaka yoyote yenye uwezo wa kumzuia kufanya alichofanya! Ni aibu kwa Taifa kuwa na viongozi wa aina hii! Viongozi ambao wako tayari kutumia fedha, hila, mamlaka na dhamana za uongozi walizopewa, kuhalalisha haramu, ni janga kwa mstakabali wa taifa letu! Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi


Imetolewa Dar es Salaam na;
Halima Mdee (MB)

Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi

 
Ibomolewe tu mchungaji alale nje!

Fanya editing uweke paragraphs na vituo ili msomaji akupate vizuri.
 
Back
Top Bottom