Halima Mdee: Hatujaja Bungeni kuuza sura

kwani alikuwa anamaanisha nini?navyojuwa njuka manake ni form one kipindi kile tulikuwa tukiitwa,then na sisi tukajapata njuka wetu mwaka uliofuata!
Dah! Umenikumbusha mbali na ishu ya Njuka. Hujakosea kabisa. Ina maana wabunge wapya ni Njuka pia?
 
Halima Mdee kambiwa afute kauli ya kuuza sura na njuka ingawa Spika aliwaambia wabunge kuwa muongozo wa Spika unatolewa mwisho wa mada ila CCM wao wanavunja hizo kanununi yaani ni vurugu tu.

Nilifikiri Anne Makinda angemsifia kwa kuchangia Kiswahili kukua huyu mama wa Njombe vipi au kwa sababu anaongea kilugha basi kila mmoja aongee kama yeye?. Nani asiyejua maana ya kuuza sura kama siyo visa vya Makinda. Ila ajue pale saigoni wanamsubiri na sijui kama shopping ataenda tena Kariakoo.
 
Halima mdee ni kichwa,yeye peke yake sawasawa na wabunge 100 wa CCM,kaza buti halima mpaka magamba yapukutike yote.ANGUKO LA CCM LIMETIMIA
 
Bro Zitto,Sister Halima ,new kids in in block endeleza juhudi until transformed Tanzania under 'occupation' is transformed into true democracy.
 
Huyu dada kila anachotema ni madin..yan ccm wenyewe wanamuadmire akianza kuongea wote wanakuwa mguu sawa..raha sana..long liv dada
 
Then akamchana msamba JK,
Kuwa amesainishwa kitabu alichokitoa ofisini kwa Lukuvi kinachoonyesha jk akisema ili kuinua kilimo anataka kufikia mwaka huu na ujao bajeti itenge asilimia 10 ya bajeti kwa ajili ya kilimo...lkn cha kushangaza kumetengwa chini ya asimia nane! Akasema Ccm inamtia aibu raisi! Yaani wanamsainisha mambo ambayo hayatekelezeki!!

Big up Halima...wenye akili tunakukubali mno!
 
Bahati mbaya hatupati rekodi kamili ya alichosema Mdee. Tunapewa vi snippets vya neno moja moja halafu tunategemewa tujadili na tunarukia kujadili.

Ametamka "njuka," kasema nani njuka? Kafanya nini "njuka"? Kuuza sura, nani kaambiwa anauza sura?
 
Bahati mbaya hatupati rekodi kamili ya alichosema Mdee. Tunapewa vi snippets vya neno moja moja halafu tunategemewa tujadili na tunarukia kujadili.Ametamka "njuka," kasema nani njuka? Kafanya nini "njuka"? Kuuza sura, nani kaambiwa anauza sura?
njuka ni wale wasiojua kanuni za Bunge.wauza sura ni wale wasiochangia bajeti kazi yao kupiga makofi tu!
 
wabunge wa CCM wanaona wivu kwa kuwa wao hawana ujasiri na uwezo wa kupembua mambo outside the box....good job done Mdee, keep on.....
 
Njuka ni njuka na kama hatakubali basi hatakomaa atabaki kuwa njuka. Je UDOM Vipi, si inaonyesha unjuka. Mlichotaka ni kumkatisha tu Halima Asiongee, kwa sababu hoja zake zinawaumbua, Wasaliti wakubwa wa wananchi. Mimi kura yangu hampati tena.

Mbunge kijana wa jinsia ya kike ambaya anachukua nafasi ya anne kilango. CDM moto wa kuotea mbali.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom