Halima Mdee: Bold and Beautiful!

She is extremely beautiful kwa kweli mbunge wetu wa Kawe mtarajiwa...

IMG00162-20101005-1910.jpg
 
Nivizuri mleta hoja angeeleza pia elimu yake, anastahili kupewa jimbo la kawe miye pia nampa Big Thump kwa ujasiri wake alioouonyesha mjengo wa vijana wapya wajao, naamini mwaka huu sisi emuuuuuuuuu! be ready to be blusted even with your members as Ionic lady which she deserved to be in Chadema mama Malecela,
Naamini hata muungano utapata upepo mkali sn labda hata marehem anaweza kuitwa kwenye kupokea Nishani au tuzo hapo ndipo ndugu hufaidi, maana yangu nikuwa labda marehem Tanganyika aweza kumbukwa na kuongelewa hata kupewa nafasi na watoto na wajukuu ambao hatukumuona tutapata habari zake naikiwezekana muungano utapata matofari kama si kuziba ukuta, kwani Zenji wameamua kivyao vyao je kunako hakuna bahari watasemaje baada ya uchaguzi? je watanyamaza?Mdee najua ataongelea sn twamjua ni chapa ya mamba.
 
Halima Mdee, Mbatia hakuna amani

  • Posted on October 4, 2010 at 10:30am

Na Mwandishi Wetu

Joto la kisiasa limezidi kupanda, Jimbo la Kawe wagombea wawili wenye nguvu lakini wote wakiwa na tiketi za vyama vya upinzani, Halima Mdee (CHADEMA) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi), hawapatani na katika mapambano yao ya kisiasa hakuna amani.

Habari zisizo na shaka zinasema kuwa kila upande umekuwa ukimshutumu mwenzake kwamba unamhujumu kisiasa, hivyo kukuza mtifuano kati yao huku wakimsahau mpinzani wao mkubwa, Angela Kizigha (CCM).

Wiki iliyopita, gazeti hili lilizungumza na msaidizi wa Mbatia, Hamis Athuman ambaye alisema kuwa wanasheria wa NCCR chini Mhadhiri, Sengondo Mvungi wanafuatilia kauli za Halima kabla ya kuamua cha kufanya baadaye.

Alhamisi iliyopita, gazeti hili lilipewa taarifa na chanzo chake cha kuaminika kuhusu Halima kumpigia simu Mbatia na kumshutumu kwamba amekuwa akiendesha kampeni chafu dhidi yake, ikiwemo kumtangazia kuwa amejitoa kinyang’anyiro cha kuwania Ubunge Kawe.

“Amempigia simu na hawakuongea vizuri, unaweza kuona jinsi hali ilivyo. Ni siasa lakini hakuna aliye tayari kuona mwenzake anakuwa na mtaji mkubwa wa kisiasa kuliko yeye, kwahiyo hakuna maelewano hasa pale inapoonekana kuna mtu amezungumza kitu cha kumuathiri mwingine,” alisema mtoa habari wetu.

Halima, alipoulizwa na gazeti hili kuhusu kumpigia simu Mbatia, alikiri na kusisitiza kwamba alifanya hivyo kumuonya kwa sababu amekuwa akizungumza maneno ya kumchonganisha na wapigakura wake.

“Kwenye mkutano wao Tegeta Jumatano iliyopita, walitangaza nimejitoa kugombea Ubunge Kawe kwa sababu nimeshinda Viti Maalum CHADEMA kitu ambacho si cha kweli. Ilikuwa ni kunichonganisha na wapigakura wangu, kwahiyo Mbatia na chama chake hawakunitendea haki ndiyo maana nilimpigia simu.

“Nilimwambia aache, mimi shida yangu si Ubunge, lengo langu ni kuwatetea wananchi. Kusema nimeshinda Viti Maalum wakati si kweli ni kuniharibia. Nagombea jimbo na lengo langu la Kawe ili niwatetee wananchi,” alisema Halima.

Mbatia alipotafutwa, simu yake ilipokelewa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Jimbo la Kawe, Hemed Msabaha ambaye alisema kuwa kama Halima alipiga simu, basi alifanya hivyo kirafiki kwa sababu sheria hazitamki alivyofanya.

“Iweje Halima ampigie simu mtuhumiwa wake? Angekwenda kushtaki, kitu kingine siku hiyo inasemwa ni gazeti liliandika Halima ameshinda Viti Maalum lakini Mbatia hakuzungumza hayo maneno na vizuri ni kwamba sisi huwa tunajadili hoja badala ya watu,” alisema Hemed.

Source: GPL
 
anafaa sana kuwa mke wa slaa kwakuwa hana mke angemuoa huyo ta kuliko kuvamia wake za watu:tonguez:
 
http://www.globalpublishers.info/profile/UWAZI
Waathirika wa mikopo wamvamia Halima Mdee Kawe

Na Mwandishi Wetu

Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA, Halima James Mdee amevamiwa na kundi la wananchi wa Bunju, waliodai kuchangishwa pesa ili wapewe mikopo lakini matokeo yake kuambulia hasi.

Halima, alivamiwa na wakazi saba wa Bunju katika eneo la Tegeta, Dar es Salaam Jumatatu wiki hii na kumuweka kati, wakitaka asikilize kilio chao kwamba walichangishwa fedha na chama kimoja cha upinzani (siyo CHADEMA) kwa ahadi ya mikopo lakini hawajaambulia chochote.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Halima alikuwa akipita Barabara ya New Bagamoyo akitokea usawa wa Mwenge Dar es Salaam akiwa kwenye gari lake aina ya Toyota Land Cruiser Prado, alisimamishwa na wananchi hao eneo la Tegeta Kibaoni.

Akiwa anaendesha mwenyewe, Halima kwa uelewa kwamba waliomsimamisha ni wapigakura wake, aliweka gari kando na aliposhusha kioo tu, alivamiwa na wananchi saba ambao walianza kumsimulia kilio chake.

Wakieleza kinachowasibu, wananchi hao walisema kuwa wao ni wakazi wa Bunju na kilio chao ni kwa chama kimoja cha siasa ambacho kiliwachangisha pesa kwa ahadi ya kupewa mikopo lakini hawajapewa.

"Tulichangishwa pesa za kujisajili na ada ya kupewa mikopo. Jumla shilingi 10,000. Hicho chama kilituambia tujiunge ili tupewe mikopo na kwamba wao wana dira ya kutukomboa.

"Lakini tangu tumechangishwa hatujapewa hiyo mikopo na zaidi mambo yanazidi kuwa magumu na elfu kumi kumi zetu zimepotea, tunaomba utusaidie mheshimiwa, tunakutegemea," kilisema chanzo chetu kwa kumkariri mmoja wa waliotoa kilio chao kwa Halima.

Chanzo chetu kiliendelea kusema kuwa wananchi hao pia walimkabidhi baadhi nyaraka zinazoonesha ukweli wa madai yao, pamoja na mchakato mzima wa kuchangishwa.

Jumatano ya wiki hii, gazeti hili lilimuendea hewani Halima ambaye alikiri kukumbwa na mkasa huo lakini akafafanua kwamba haoni kama ni geni kwenye shughuli za siasa.

"Ni mambo ya kawaida, wale walinifuata kunifikishia kilio chao kwa imani kwamba naweza kupaza sauti kwa kilio chao. Maelezo yao nimeyapokea, kwahiyo naangalia jinsi ya kuwasaidia kwa sababu ni wapigakura wangu," alisema Halima.

Source: GPL
 
Waathirika wa mikopo wamvamia Halima Mdee Kawe

Na Mwandishi Wetu

Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA, Halima James Mdee amevamiwa na kundi la wananchi wa Bunju, waliodai kuchangishwa pesa ili wapewe mikopo lakini matokeo yake kuambulia hasi.

Halima, alivamiwa na wakazi saba wa Bunju katika eneo la Tegeta, Dar es Salaam Jumatatu wiki hii na kumuweka kati, wakitaka asikilize kilio chao kwamba walichangishwa fedha na chama kimoja cha upinzani (siyo CHADEMA) kwa ahadi ya mikopo lakini hawajaambulia chochote.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Halima alikuwa akipita Barabara ya New Bagamoyo akitokea usawa wa Mwenge Dar es Salaam akiwa kwenye gari lake aina ya Toyota Land Cruiser Prado, alisimamishwa na wananchi hao eneo la Tegeta Kibaoni.

Akiwa anaendesha mwenyewe, Halima kwa uelewa kwamba waliomsimamisha ni wapigakura wake, aliweka gari kando na aliposhusha kioo tu, alivamiwa na wananchi saba ambao walianza kumsimulia kilio chake.

Wakieleza kinachowasibu, wananchi hao walisema kuwa wao ni wakazi wa Bunju na kilio chao ni kwa chama kimoja cha siasa ambacho kiliwachangisha pesa kwa ahadi ya kupewa mikopo lakini hawajapewa.

“Tulichangishwa pesa za kujisajili na ada ya kupewa mikopo. Jumla shilingi 10,000. Hicho chama kilituambia tujiunge ili tupewe mikopo na kwamba wao wana dira ya kutukomboa.

“Lakini tangu tumechangishwa hatujapewa hiyo mikopo na zaidi mambo yanazidi kuwa magumu na elfu kumi kumi zetu zimepotea, tunaomba utusaidie mheshimiwa, tunakutegemea,” kilisema chanzo chetu kwa kumkariri mmoja wa waliotoa kilio chao kwa Halima.

Chanzo chetu kiliendelea kusema kuwa wananchi hao pia walimkabidhi baadhi nyaraka zinazoonesha ukweli wa madai yao, pamoja na mchakato mzima wa kuchangishwa.

Jumatano ya wiki hii, gazeti hili lilimuendea hewani Halima ambaye alikiri kukumbwa na mkasa huo lakini akafafanua kwamba haoni kama ni geni kwenye shughuli za siasa.

“Ni mambo ya kawaida, wale walinifuata kunifikishia kilio chao kwa imani kwamba naweza kupaza sauti kwa kilio chao. Maelezo yao nimeyapokea, kwahiyo naangalia jinsi ya kuwasaidia kwa sababu ni wapigakura wangu,” alisema Halima.

Source: GPL
 
I support her. Yes Bold. Yuko kwa maslahi ya taifa na automatically maslahi yake Mungu anamlipa.
 
mjengoni si mara yake ya kwanza kufika na kufanya kazi!!!
 
kazi ipo kwani anapambana na mbatia ambaye ni maarufu kama yeye.
 
Back
Top Bottom