Hali ya Uusalama wa taifa letu ni ya hatari

Ukosefu wa mafuta (sio uhaba), ukosefu wa umeme, ukosefu wa ajira, tofauti kubwa ya kipato kati masikini na matajiri na ugumu wa maisha kwa ujumla ni vitu vinavyopelekea hali ya usalama wa taifa letu kuwa hatarini.
Naona kabisa kuna siku watu wataingia mitaani, machafuko makubwa yatatokea na huenda yakamn'goa raisi na serikali yake madarakani.
Kwakweli hali ya usalama wa taifa letu ni mbaya na inatisha.

Mvunja nchi ni mwana nchi!! serikali hii ikitoka itakuja nyingine ye watanzania wala usihofu! CCM ikitoka kitakuja chama kingine cha watanzania wala si watu kutoka nje! so usihofu unless you have something to loose!
 
daladala na taxi zimegeuka sheli, galoni la lita tano linauzwa kwa 15,000/= ambayo ni sawa na sh. 3,000/= kwa lita. Kweli hali yetu ya taifa ni mbaya sana
 
Panapofuka moshi hapakosi moto na huu moto kama utalipuka sijui kama utazimwa kirahisi bila kuwepo mabadiliko makubwa ya uongozi nchini.

Ukosefu wa mafuta (sio uhaba), ukosefu wa umeme, ukosefu wa ajira, tofauti kubwa ya kipato kati masikini na matajiri na ugumu wa maisha kwa ujumla ni vitu vinavyopelekea hali ya usalama wa taifa letu kuwa hatarini.
Naona kabisa kuna siku watu wataingia mitaani, machafuko makubwa yatatokea na huenda yakamn'goa raisi na serikali yake madarakani.
Kwakweli hali ya usalama wa taifa letu ni mbaya na inatisha.
 
Wenzetu wakiwa
wanasonga mbele kwenye nyanja za sayansi
na teknolojia, sisi tunazidi kurudi nyuma na
kudorora. Rasmi tunaacha kutumia magari na
kuanza kutumia magari ya kukokotwa na
wanyama.
 
Nadhani tunahitaji ku-define neno Taifa lina maana gani kabla ya kuangalia usalama wake. kiujumla Taifa kijiografia ni nchi yenye kutambulika kwa mipaka yake kadha wa kadha. kwa maana hiyo taifa letu la tz linatambulika kwa mipaka yake ya kiramani. Lakini neno/jina Taifa ni nchi yenye utawala hususan wake. na hapo ndo tunapoanza kupata shida na hili tulisemalo taifa letu.

Manake ukiacha maana ya kijiografia, hakuna maana nyingine ya taifa iliyo in existence. nadhani falsafa ya taifa kama sehemu ya nchi yenye utawala (uwe wake yenyewe kama taifa huru au wa kutawaliwa na nchi nyingine - koloni) vyote hatunavyo. sisi hatujitawali wala hatutawaliwi. kwa ufupi hatuna uongozi.

Na kwa hali hii, sioni kama tuna chochote cha kusema usalama wa taifa...manake hilo taifa lenye huo usalama halipo. labda umaanishe tunatishiwa kuvamiwa na nchi firani...ambayo kwa sasa haipo na haitegemewi kutokea. kwa kuwa hatuna tatizo la usalama wa taifa, kitu pekee kilicho hatarini kiusalama ni hao wajionao viongozi wa taifa hili...wao ndo usalama wao uko hatarini...na wanastahili kuwa katika hali hiyo
 
Usalama wa Taifa wapo Baa za Kijitonyama na Sinza wanakula BIA na kubadilisha "plate number" za magari!

BTW: Hivi walinzi wa Kikwete na wasindikizaji wa msafara wake nao ni "State Security Agents" or "Operatives"?[/QUOTE]unaweza kuwaita wauza sura.ila wa kwa sasa watoto wa mjini wamewapachika jina jingine wanaitwa WAVIMBA MACHO et kisa raisi au waziri mkuu anapoenda sehem katika mishemishe za kiserikali wao kazi yao ni kutazama usalama(sijui usalama gani?).ila nawapendea jambo moja.wanajua sana kupangilia kaunda suti pia kuuchuna bila kuzungumza na mtu.kwa hilo wapo juu.oops nimesahau na sunglasses.jamaa wana mbwembwe wale.lol
 
Chanzo cha matatizo yote wa kuilaumu ni serikali ambayo madarakani kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa kuwa letea wananchi maisha bora,maisha bora hayaji midomoni huja kwa vitendo..
 
Back
Top Bottom