Hali ya umeme nchini: Tanesco yakata tamaa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
[h=3]Tanesco yakata tamaa [/h]

*Yasema hali tete, ratiba ya mgawo yatupwa

Na Benjamin Masese
Majira

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kuwa hali ya mgawo wa umeme nchini kwa sasa ni tete kutokana na uzalishaji wa nishati hiyo kuzidi kupungua na kufikia hatua za mwisho za kuzimwa kwa mitambo.

Vile vile limesema kwamba halitaweza kufuata ratiba iliyotolewa awali ya mgawo wa umeme na hivyo kuwataka wananchi kukubaliana na hali iliyopo sasa hadi serikali itakapofanikisha mipango yake kuhusu suala hilo.

Hayo yalisemwa na Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Badra Masoud wakati wa mahojiano na gazeti hili kwa njia ya simu kuhusu kutofuatwa kwa ratiba ya mgawo wa umeme iliyotolewa awali ambayo imesababisha malalamiko kwa wananchi.

Bi. Masoud alisema kuwa ratiba hiyo imeshindikana kufuatwa kutokana na kiwango kidogo cha umeme kinachozalishwa ambacho kwa muda mwingine kipanda na kushuka, hivyo kuwapa wakati mgumu wa kuwahudumia wateja wake.

Alisema kuwa hakuna njia mbadala ya kuepusha tatizo hilo, kwa kuwa tayari limeshakuwa kubwa.

Kinachotakiwa sasa, alisema ni uvumilivu na subira wakati serikali ikiwa katika mchakato wa kuepusha nchi isiingie katika giza.

"...kwa hilo ni kweli hatuwezi kufuata ratiba tuliyoitoa awali kwa sababu ya kiwango cha uzalishaji kupungua kila wakati, yaani kinapanda na kushuka...sasa ukisema unafuata ratiba utasababisha migogoro, naomba wananchi watambue kwamba hali ni tete na tukubaliane na hali hii," alisema.

Hivi karibuni, vyombo vya habari vilisema makali ya mgawo wa umeme yameongezeka kutoka saa nane hadi 18 kwa siku katika mikoa mbalimbali ikiwemo Tabora, Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam.
 
Kwanini serikali haiko wazi kukubali kua hili ni janga la kitaifa?
 
Huyo mama wa tanesco hajui lolote wala asituambie tukubaliane na hali, hizi kazi za kupewa kwa kuangaliwa usoni bwana.....
 
Kwanini serikali haiko wazi kukubali kua hili ni janga la kitaifa?

Mkuu wa nchi si kishaongea kwamba yeye si mawingu anyeshe mvua na pia matatizo haya ya umeme yeye kayakuta hivyo hastahili lawama zozote!! Hivyo nchi ndio inaelekea gizani sijui kwa kipindi gani...labda mpaka October kama kutakuwa na mvua za kutosha ya kuweza kuyajaza yale mabwawa ya Mtera na Kidatu, vinginevyo kama ukame utaendelea giza ndio hiloooooo linajivuta taratibu.
 
Yatatimia muda si mrefu,ccm wapo kwa ajili ya kuvuna raslimali zetu.wanashindwa kuuza mashangingi then wanunue mitambo ili watupe umeme?
 
Pamoja na kwamba JK kakuta tatizo yeye akisaidiwa na aliowateuwa kishkaji wakaendelea kuitafuna kwa kuandaa mikataba mibovu na kujilimbikizia fedha nje na ndani ya nchi, akifikiri na yeye ataicha TANESCO kama alivyoikuta kumbe speed ya jamaa zake ya kuitafuna ikatriple(x 3) sasa inamuumbua, anaulizwa swali anajibu kama mtoto ambaye hajaenda hata darasa la kindagatern bana inaudhi sana!
 
Huyo mama wa tanesco hajui lolote wala asituambie tukubaliane na hali, hizi kazi za kupewa kwa kuangaliwa usoni bwana.....

yani imebidi nichekek tu kwa sentensi yako...
wazime tu tuingie gizani labda tutapata akili sasa.
 
Lakini Taarifa zilizopo nikuwa Tatizo la umeme ni la muda tu kufikia mwezi wa Disemba mwaka huu litatatuliwa....taarifa zaidi fuatilia vyombo vya habari kuanzia sasa
 
Back
Top Bottom