hali ya uchumi serikalini ni mbaya sana

carmel

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,836
262
Hali ya uchumi imekuwa mbaya sana katika idara zote za serikali kuliko hata ile iliyowahi kuripotiwa wakati wa uchaguzi. Chanzo cha kuaminika kutoka idara moja nyeti kinasema wamepelekewa waraka mzito wa kuwaamuru kurudisha hazina OC walizokuwa wamepelekewa kwa ajili ya matumizi ya kazi za serikali. Kwa ufupi hata OC zenyewe kuna wizara yenye idara kama kumi inapelekewa sh miliion kumi which means kila idara ipewe million moja kwa mwezi na bado wanataka pesa hizo zirudishwe kwa kisingizio kuna watu hawajalipwa mishahara kwa hiyo bora kazi zote zisimame mishahara ilipwe. hali inatisha especially kwa sukari kufikia 2000 kwa kilo. Tunaenda wapi?
My Take: huu ni mkakati maalumu wa kutafuta fungu la kuilipa dowans.
Amueni wananchi wakati ni huu wa kufanya kama Tunisia.
 
Hivi ule mkutano wa Bunge letu ''tukufu'' wa mwezi wa pili bado upo pale pale?

Nadhani wangeanza kwa kuuahirisha huo kwanza.

Wananchi wafanye kama Tunisia? - ile sumu tuliyopuliziwa ya ''amani, utulivu na mshikamno'' itachukua muda mrefu saaana ku-expire.
 
Bunge liahirishwe? I dont think so, wanajua sana kulinda maslahi yao hawa, mi ningewasifu kama wangepunguza posho za wabunge kulipa dowans
 
Bunge liahirishwe? I dont think so, wanajua sana kulinda maslahi yao hawa, mi ningewasifu kama wangepunguza posho za wabunge kulipa dowans

Kuliko kuwanyang'anya idara nyeti let say ya afya hako ka-milioni moja, si bora bunge lisubiri kwanza kuepusha yale mamilioni wanayojilipa posho?

But again, vipaumbele vyetu vipo tumboni
 
Hazina hakuna fedha siyo kuwa wanataka kuwalipa Dowans. Makusanyo ni madogo ni 60% tu ya mahitaji ya nchi vilevile Mkwere alitumia fedha nyingi sana kwenye kampeni akifikiria kuwa anaweza kuzirejesha kwa mizunguko mingine kama ya Dowans n.k Akina ankle Michuzi na wengine walikuwa wanapata posho ya laki moja kwa siku. Kampeni ilikuwa nchi nzima .... leo ndo tunalipa gharama hiyo. Nakumbuka kabla sijatoroka Bongo baada ya kuona akili za wengi ni finyu kwenye uchaguzi uliopita tulitakiwa kurejesha OC hazina mwezi Septemba ambapo ofisi niliyokuwepo ilitakiwa kurejesha nusu ya fedha zote zilizokuwa zimeletwa. Nasikitika kuona kama bado inaendelea .......... "" Mwenye macho na aone..... mwenye masikio na asikie..... """
 
carmel -

Naomba kuuliza tu - OC ndiyo nini vile? Maana wengine hatujawahi kufanya kazi serikalini tangia kutoka tumboni mwa Mama zetu!

It sounds like "salary advance"? right?
 
carmel -

Naomba kuuliza tu - OC ndiyo nini vile? Maana wengine hatujawahi kufanya kazi serikalini tangia kutoka tumboni mwa Mama zetu!

It sounds like "salary advance"? right?

I think it's OTHER CHARGES. Fungu linalopelekwa ofisi za serikali to cover operational costs, I guess.
 
magafu, nimekusoma, hata mi kilichoniondoa bongo, ni unafiki na ufisadi wa serikali. Poleni ndugu zangu mliopo tz, iliniuma sana kikwete alivyochakachua kwa mara ya pili.
 
carmel -

Naomba kuuliza tu - OC ndiyo nini vile? Maana wengine hatujawahi kufanya kazi serikalini tangia kutoka tumboni mwa Mama zetu!

It sounds like "salary advance"? right?
OC maana yake "Other Charges" apart from mshahara huwa kuna hela inatoka Hazina inaitwa OC kwa ajili ya ku-run office. Kununulia karatasi, wino, kulipia internet, umeme,fax,simu, chai asubuhi, kulipa vibarua, kununua vifaa kama computer, printers, photocopier, posho za vikao,mafuta ya gari,vifaa vya usafi na mengine mengi kama hayo. Huwa kwa idara moja ya wizara ina matumizi ya bilioni 5-10 kwa mwaka.
 
Yote mliyoyanena ni kweli hakika.Kila Idara na Sekta ya Umma sasa hivi wanahaha jinsi ya kuwalipa wafanya kazi posho zao za mwezi acha mishahara.Mtakumbuka majuzi Polisi wakilalamika wamekatwa posho zao,Ile ilikuwa ni hatua ya makusudi kabisa wala haikuwa bahati mbaya kama yule bwana mdogo wa Zenji alivyojitetea!!!Kwa ujumla Hazina kuna hali mbaya isiyoelezeka katika historia ya nchi hii miaka 50 Baada ya uhuru.
 
carmel -

Naomba kuuliza tu - OC ndiyo nini vile? Maana wengine hatujawahi kufanya kazi serikalini tangia kutoka tumboni mwa Mama zetu!

It sounds like "salary advance"? right?

ni matumizi ya kila mwezi yanayotolewa kwa kila idara ya serikali
 
Nilijua hali itakuwa hiyohiyo. Kama rais anaingia madarakani tena kwa forgeries, tutarajie nini? Usanii kila kona. kwenye wizara kama za nishati usiseme. Hata watanzania tutegemee kula mikenge. Mpaka akili zitakapo tuingia tukaingia barabarani kuandamana.
 
kuna idara toka mwaka huu wa fedha uanze hazijapata mafungu ya miradi...wanaripoti na kuondoka ofcn wakisubiri mishahara.idara zina madeni kila pahali
wakulima waliahidiwa ruzuku ya pembejeo wakaandaa mashamba makuuubwa lakini mpaka sasa bilabila
Lakini kama watendaji wanaendelea kufyata mkia mwisho wake itakuwaje
 
Hapo kwenye RED panatia simanzi! Tunakoelekea tutalishwa unga wa mbao!
 
Hazina hakuna fedha siyo kuwa wanataka kuwalipa Dowans. Makusanyo ni madogo ni 60% tu ya mahitaji ya nchi vilevile Mkwere alitumia fedha nyingi sana kwenye kampeni akifikiria kuwa anaweza kuzirejesha kwa mizunguko mingine kama ya Dowans n.k Akina ankle Michuzi na wengine walikuwa wanapata posho ya laki moja kwa siku. Kampeni ilikuwa nchi nzima .... leo ndo tunalipa gharama hiyo. Nakumbuka kabla sijatoroka Bongo baada ya kuona akili za wengi ni finyu kwenye uchaguzi uliopita tulitakiwa kurejesha OC hazina mwezi Septemba ambapo ofisi niliyokuwepo ilitakiwa kurejesha nusu ya fedha zote zilizokuwa zimeletwa. Nasikitika kuona kama bado inaendelea .......... "" Mwenye macho na aone..... mwenye masikio na asikie..... """

Hapo kwenye bold ni mchango pia kwenye ukata wa serikali, haswa mgao ulioanza mara nyingi tu ofisi za TRA zinakuwa off-line ikiimanisha kwa saa kadhaa au siku nzima kodi zinakuwa hazikusanywi. Walipa kodi wanasubiri mpaka uvumilivu unawashinda.
 
Kwa kweli hali ni mbaya katika idara za serikali,pesa za maendeleo hakuna ni pesa za mishahara tu ndio zinatoka nazo zatolewa kila mwezi.Kwa mwenendo huu hakuna ahadi hata moja aliyotoa JK itatekelezwa mwaka huu wa fedha.Swali la kujiuliza hizo hela zilikwenda wapi wakati uchaguzi uligharamiwa na wafadhili?au ndio EPA nyingine?
 
na mtaani napo hali mbaya leo mfuko wa sukari kg50, sh 90000 bei ya jumla wakati jk anaingia madarakani ilikua sh 35 000
 
na mtaani napo hali mbaya leo mfuko wa sukari kg50, sh 90000 bei ya jumla wakati jk anaingia madarakani ilikua sh 35 000

Hili ndo linaniuma haswaa. mimi mwananchi wa kawaida kununua kilo ya sukari sh 2000.
 
hebu achaneni na bubge hivi mmeshajiuliza hiyo semina ya wiki mbili kwa wabunge wote hao ya kumsikiliza fisadi hosea mtu ambaye wao wanatakiwa kum discipline inatumia zaidi ya milion 20 kwa siku bila kujumlisha mafuta yao na perdiem kulikua na umuhimu kweli? Kweli kuna seminar gani ndefu kiasi hicho ya one size fits them all, wabunge wapya na wa zamani wanafundishwa sane thing na same instructo, sawa na wanafunzi wa darasa la kwanza na la saba kusoma somo moja kwa mwalimu mmoja
 
Back
Top Bottom