Hali ya sintofahamu Bungeni: Polisi waingilia kati, Wabunge wa Upinzani watolewa nje

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Hali ndani ya bunge ni kutokuelewana muda huu, wabunge upande wa upinzani, wamesimama muda huu kushinikiza bunge kurushwa live na TBC, mwenyekiti anayeendesha bunge muda huu ni Andrew Chenge amesema uamuzi wa Serikali kuzuia bunge kurushwa live ni sahihi.

TV zilizokuwa hewani jioni hii nazo zimeondoka hewani live baada ya wabunge wa upinzani kusimama wakitaka mjadala wa bunge urushwe live na TBC.

Hali ndani ya bunge ni sintofahamu!.



Updates;

=Polisi waingia ndani ya Ukumbi wa bunge kudumisha usalama, baadhi ya Wabunge wameumia Mbunge wa Arumeru Magharibi na wabunge wawili wa CUF toka Zanzibar

=Baadhi ya wabunge(Lissu, Bulaya, Lema na Pauline Gekul) wametolewa nje sababu walikua wanashinikiza kujadiliwa kwa hoja ya Zitto juu ya kusimamishwa bunge kurushwa moja kwa moja na TV.

=Wabunge wote wa UKAWA na Mbunge wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe, Watolewa nje.

=Bunge linaendelea na mjadala wa kujadili Hotuba ya Rais.

= Zitto Kabwe ameungana na UKAWA na kwa sasa wapo kwenye kikao cha pamoja kujadili hatua za kuchukua baada ya tukio.

20160127070616.jpg

20160127070618.jpg
 

Attachments

  • 20160127070617.jpg
    20160127070617.jpg
    67.6 KB · Views: 117
Tatizo Ni Nini?, TBC1 na Serikali ya JPM Inajiandaa Kuficha Nini?, Kama TBC1 Ni Chombo Cha Taifa Kwa Nini

Tuwekewe Figisufigisu za KutokukifaidiChombo Chetu. Kama Wasiporusha Live Basi TBC1 Ni Chombo Cha

CCM Kama Ilivyo Gazeti la Uhuru na Mzalendo. Ulimwengu wa Sasa Wanasema Ni Black and White, Koleo

Linahitwa Koleo na sio Kijiko, Mjusi anahitwa Mjuzi Na wala Sio Mamba. Kama Serikali Imecreate Majipu

katika Maamuzi na Matendo yake basi Waache Wabunge ambao ni Wawakilishi wetu Wayatumbue

Majipu hayo Mbele ya Macho ya Watanzania through TBC1.
 
Ninaona ccm safari hii wamejizatiti kuyapa uongozi wa bunge mafisadi na makatili kama chenge, ndungai na yule mwanamke ili kuendeleza ubabe wa kuvunja katiba. Na hapa ni ishara tosha kwamba sasa Tanzania hakuna katiba wala sheria ila kinachoongoza ni mabavu.

Mwenendo wa bunge ninaona viongozi wanatumia ubabe ili kulinda maslahi ya ccm. Hivi ndivyo wenye nchi wanataka?

Ninaona hatari inakuja kwa kasi. Ikumbukwe watu hawajapona majerha ya kugeuzwa kwa matokeo ya uchaguzi, suala la Zanzibar ndiyo kwanza halijaanza hata kufuka moshi, bado wanahamishia ubabe bungeni. Nini kinafuata?
 
Saa hizi ni wakati wa kilimo,hizo Tv zitutembelee wakulima huku ili waonyeshe live ukulima wa kisasa,kuliko kuonyesha kina sugu wakirusha makonde bungeni live
 
Hapa ni ccm Ikubali, imeteleza Kumtuma Nape, Kuminya Uhuru wa Habari Kwa watanzania, kupata Habari za Bunge Lao Kutoka Kwa Wa wakilishi Wao.

Hiki Chombo Siyo Mali ya Chama Cha Mapinduzi, ni Chombo Cha Uma Tofauti na Itv, Star Tv, Azam Tv Au Chanel 10.

Kila Mtanzania Anakilipia Kodi Chombo Hiki, Hivyo Basi ni Haki kwa TBC Kuwajibika Kwa Wananchi, Kwa Kuwapa Habari Muhumu Ziusuzo Maendeleo ya Wananchi.

Ni Haibu Kusikia Mh Nauye Akisema Hati TBC Imekosa Kiasi cha Sh Bl 4 za Kumudu Kuwapatia Matangazo ya Bunge Wananchi wake!

Basi Serikali Itangaze Kwamba TBC imefilisika Na Ikifunge Kabisa, Kuliko Kuja kutuletea Hadithi za Uongo, wakati Chombo Serikali inawajibika Kuhakikisha Shirika Hili Linawapatia Wananchi Habari Kwa Mujibu wa Katiba Ya Nchi.

Ccm inaogopa nini? Kama inajiamini? Waache Hofu, wananchi waachwe Wapime pumba na Mchele. Kwani Hawataki Mh Magufuli Aonyeshwe Majipu yaliyojificha na Wabunge wa UKAWA? Au Ndani ya ccm Majipu Ni Karibia Yote?
 
Ni heri kuonesha vijana wakiwa mashambani wanalima live kuliko kuonesha mahoka ya wenye elimu za hapa na pale



wakati mwingine jaribu kuficha ujinga wako hata kidogo tu! huna akili,hata mwenye mtindio wa ubongo anaweza kupost kitu cha maana kuliko wewe! sio kila uzi lazima uchangie! imefika kipindi sasa UONGOZI WA JF UANZISHE JUKWAA LA WATOTO! KAMA NYIE IKIBIDI NA LA MATAAHIRA PIA!
 
Back
Top Bottom