Hali ya SIASA nchini ni TETE

ni kweli wanajamii, tujiepushe sana na alama ya vyama kwenye magari hasa chama tawala!!!
Mimi mwenyewe kwenye mkoko wangu siweki alama ya chama, ila waosha magari woooote wanajua fika kuwa chama tawala sikipendi na hunilindia gari na kuosha tena kwa uaminifu.
NGULI...jiepushe na alama ya chama hasaaaaaaa chama tawala utaumizwa kaka hasa katika majiji makubwa yote hapa nchini i.e. Dar, Mwanza & Arusha
 
Ni bahati mbaya sana CCM inaonekana kama chama cha madhalimu, japo kuna wanachama wengi sana waaminifu ambao wanatamani sana wajisikie vizuri wanaposema wao ni wanachama wa chama hicho,
Ile hisia ya ushujaa, ushupavu, mshikamani, pride imepungua sana kwa wanaCCM.
Ni kama kuwa mshabiki wa timu inayofungwa, unajisikia aibu kusema mbele za watu, uanachama wako.
Hii ni hatua nyingine Tanzania tumepiga,
Asante Kikwete kwa kutufanya tupigane wenyewe
 
Kuna mtu alisema bungeni kuwa mtake msitake mimi ndoo rais wenu.
tunajinonea how them tempered with our votes.
Seem asilimia kubwa ya wananchi bado wana hasira na yaliyotokea.....
tungoje kesho itakuwaje
 
Nguli pole kwa mkasa huu na hasa ukichukulia halikuwa gari lako.

Niliposoma kuwa POLISI wanazuia mikutano ya Slaa kwenye miji mikubwa kwa sababu hali ya Taifa ni tete, nilidhani ni utani. Sasa naanza kuamini kuwa kweli hali si shwari sana kwa Taifa. Kama kweli angeliruhusiwa kuhutuia au angelisema twendeni tukadai haki, hali ingelikuwa mbaya sana.

Wengi waliliona hili hata kabla ya uchaguzi. Kuna jamaa yangu alitua kutoka UK na kusema siku anaondoka kwamba "hali ya mwamko wa kisiasa Tanzania ni kubwa sana hajawahi kuona............" Upande mmoja inafurahisha na upande mwingine, inatisha. Tuombe Mungu mabadiliko yaje salama.

CCM itabidi wawape tu watu wanachokitaka ili kupungza tensions zilizopo:

1. Mgombea binafsi Tanzania katika ngazi zote.
2. Kubadili katiba ya Nchi ili iende na wakati.
3. Tume huru ya uchaguzi (mahakama ziwe huru pia).
4. Kupunguza madaraka ya Rais na hasa katika kuteuwa.
 
Hao ni wapole kama ingekuwa huku kwetu wangelichoma moto kabisa hilo gari na wewe mwenyewe wangekumwagia tidikali, huku kwetu CCM ni sawa shetani inachukiwa na kila mtu mpaka watoto. ILAANIWE CCM, WALAANIWE VIONGOZI WOOOOTE WA CCM, I HATE CCM.
 
Nguli pole kwa mkasa huu na hasa ukichukulia halikuwa gari lako.

Niliposoma kuwa POLISI wanazuia mikutano ya Slaa kwenye miji mikubwa kwa sababu hali ya Taifa ni tete, nilidhani ni utani. Sasa naanza kuamini kuwa kweli hali si shwari sana kwa Taifa. Kama kweli angeliruhusiwa kuhutuia au angelisema twendeni tukadai haki, hali ingelikuwa mbaya sana.

Wengi waliliona hili hata kabla ya uchaguzi. Kuna jamaa yangu alitua kutoka UK na kusema siku anaondoka kwamba "hali ya mwamko wa kisiasa Tanzania ni kubwa sana hajawahi kuona............" Upande mmoja inafurahisha na upande mwingine, inatisha. Tuombe Mungu mabadiliko yaje salama.

CCM itabidi wawape tu watu wanachokitaka ili kupungza tensions zilizopo:

1. Mgombea binafsi Tanzania katika ngazi zote.
2. Kubadili katiba ya Nchi ili iende na wakati.
3. Tume huru ya uchaguzi (mahakama ziwe huru pia).
4. Kupunguza madaraka ya Rais na hasa katika kuteuwa.

Sikonge umeniacha hoi na sgnature yako....NEC ni tawi la CCM, kibaya zaidi wanachakachua kwa KASI ZAIDI (ELNINO)
Nguruwe pita leo sina mkuki
 
mbona mi ninaweka bendera ya CHADEMA watu wananishangilia mwanzo mwisho
 
Kuna mtu alisema bungeni kuwa mtake msitake mimi ndoo rais wenu.
tunajinonea how them tempered with our votes.
Seem asilimia kubwa ya wananchi bado wana hasira na yaliyotokea.....
tungoje kesho itakuwaje

yaani nikikumbuka ile kauli natamani nipasue TV..yaani jitu jizi halafu linajisifia eti mi ndo raisi mtake msitake
 
Unaacha kumhubiri Kristo unahubiri siasa.
Kweli Nguli ndugu yangu kazi unayo, wacha wakuite fisadi.
Wakuu nimesikitika sana na mpasuko wa KISIASA ulioko nchini hivi sasa nilidhani wanayozungumza watu ni ushabiki ila leo yamenikuta, gari niliyokuja nayo kazini kwenye kioo kikubwa, kwenye kioo cha kutazama nyuma kuna benendera ya CCM. Nilivyokuja kupaki walinizuia wale vijana pamoja na waalinzi nikawasalimia wakakataa na kuambulia matusi kuwa mimi ni kijana naoneka mstaarabu kumbe mwizi na tena fisadi papa nilicheka nikizani labda ni mzaha, ndio wakaanza ya nguoni.

Kwa hasira nikapiga simu kwa manager anayehusika na parking na kwa haraka akafika alishuhudia matusi ya waosha magari wale pamoja na mlinzi pembeni na hata anisaaidii karibu nipigwe na mawe kwa hasira. Akawahoji wakasema kama nataka kupaki na gari waioshe basi nitoe bendera ya CCM haraka kwani maisha yamekuwa magumu na kuweka bendera ina maanisha mimi nachangia kwani nai support kuwepo madarakani. Cha kushangaza manager nae akawa support ndio nikaishiwa nguvu ikabidi niitoe bendera/kitambaa cha CCM ndio nika park gari.

Nime report kwenye uongozi wa ofisi nao wamenigeuka wakaniambia nisiwaletee ushabiki wa kisiasa na nikiendelea kujihusisha na siasa nitafukuzwa kazi. Imebidi niombe msamaha yasifike mbali lakini hata hivyo gari sio yangu niliazima yangu ni lizee halikosi siku 2 bila kwenda garage.

Wito wangu elimu ya mpasuko wa kisiasa itolewe ipasavyo si ajabu magari ya watu yakaanza kuchomwa na baadae kuhamia kwenye nyumba za watu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom