ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
Hata mimi sijasema kwa miezi miwili lakini dalili zimeanza kujionyesha hasa miezi hii miwili. Hivyo ina maana serikali ilianza zamani sana kuyumba kiuchumi lakini hatuwahi kunotes dalili mapema.
Ok, nashukuru mkuu kwa kuongeza mawe ya ukweli kabisa katika tetesi hizi tunazozijadili.
Ukweli ni kwamba hali itaendelea kuwa mbaya kwa sababu mali zetu ambazo zingetusaidia kujitegemea kiuchumi zimeshamilikishwa kwa wawekezaji ambao wameingia mikataba ya kijinga na kuondoka na mali zote!!!
Na hili ndiyo kilio cha upinzani kilichowapa umaarufu kwa wananchi.
Mwisho, ubarikiwe kwa hoja iliyoenda shule.
Kuna watumishi wa umma wameshiriki mafunzo Botiswana. Wanasema kule mtumishi wa umma wa chini anapata tsh. 1,800,000/- Na hapo ana uhakika wa mkopo wa kujenga nyumba ya kisasa ambapo serikali haikupi mkopo mpaka uoneshe nyumbani kwenu ambako ni sharti ujenge nyumba ya maana.
Wana maslahi mazuri kwa kuwa, gold na diamond yao wamewakabidhi wawekezaji kwa kugawana 50% wakati mwekezaji anatakiwa kufuata matakwa mengine kama kulipa kodi, kulipia lesseni ya biashara na sheria nyingine. Waliowekeza pale ni makaburu wa SA, watu wanakula bata kiivyo.
Sasa kama watumishi wa umma wanaolalamika leo, waungane kwa pamoja wapinge unyanyasaji unaofanywa na serikali haiwezekani? Polisi na JWTZ ndo wajinga kabisa, sitaki hata kuwaona. Walimu na maisha yo duni nao bado hawajabadilika. Eti mtu anajivunia kupewa tsh. 200,000/= atumie mwezi mzima? kwa vijijini inawezekana, kwa hawa wanoishi mijini tena nyumba za kupanga, si wanaishia kuwa wajasiria mali na kuwatelekeza watoto ili watafute hela ya kula na kulipia pango la nyumba?
Ama kweli we are controlled by false Consciousness.