Hali ya serikali ni tete? Mpaka sasa mishahara kitendawili

sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,204
4,208
wanajf salaam!
hivi ni kweli kwamba hali ya serikali ni tete kiasi cha kuchelewesha mishahara ya wafanyakazi mpaka sasa?
nikiwa miongoni mwa wafanyakazi wa umma,nimepata salary slip yapata 4 days now ila hundi ya mshahara haijapelekwa bank,nimemuuliza mhusika w kwa hapa ofisini kwetu anasema serikali haijaleta pesa wao wametoa slip in advance tu.

mwezi uliopita kuna mjumbe wa jf alitoa mada hii mimi sikutilia maanani kwa kuwa mwezi ulopita sisi tulipata mishahara mapema ila sasa nadhani ndio zamu yetu....

duuu napata hofu na muelekeo wa serikali yetu.au ndo ule msemo kuwa 'nchi imeshauzwa?'

nawasilisha.
 
Mwezi uliopita walichukua pesa toka TCRA, hawakuwa na namna! Mwezi huu haitawezekana kwa kuwa wakichukua tena TCRA wameonywa kuwa wataiuwa taasisi hiyo, labda wataelekea NSSF au GEPF.

Ambaye atanibishia kuhusu hili la serikali kukopa TCRA na kufilisika naye atakuwa amefilisika kimawazo
 
Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!
 
izo sekta binafsi,labda kwa vibarua sio waajiriwa,tar ya mshahara ni kuanzia 21-25,mpaka apo esabu maumivu,serikal kushney...
 
Tunarudi enzi za Mwinyi, mashule yamefungwa kabla ya muda, serikali imefilisika

Serikali corrupt hazikusanyi kodi - Mwalimu Nyerere !!!!
 
Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!
hujui na hujui kuwa hujui
 
Lisemwalo lipo, kuna watu walimtukana sana yule mleta uzi! sasa mnaanza kuuona ukweli eeeeh!!!!
 
wanajf salaam!
hivi ni kweli kwamba hali ya serikali ni tete kiasi cha kuchelewesha mishahara ya wafanyakazi mpaka sasa?
nikiwa miongoni mwa wafanyakazi wa umma,nimepata salary slip yapata 4 days now ila hundi ya mshahara haijapelekwa bank,nimemuuliza mhusika w kwa hapa ofisini kwetu anasema serikali haijaleta pesa wao wametoa slip in advance tu.
mwezi uliopita kuna mjumbe wa jf alitoa mada hii mimi sikutilia maanani kwa kuwa mwezi ulopita sisi tulipata mishahara mapema ila sasa nadhani ndio zamu yetu....
duuu napata hofu na muelekeo wa serikali yetu.au ndo ule msemo kuwa 'nchi imeshauzwa?'

nawasilisha.

Kama wafanyakazi wa serikalini kutolipwa mshahara by tar.25 ndo kusema imeshauzwa basi nchi ilishauzwa tangu zama za Nyerere!! Hivi ni lini nchi hii haijapata kuwa na ucheleweshaji wa mishahara kwa muda wote?! Mie nilishawahi kufanyakazi kazi NMB, na mara kibao tu mishahara ilikuwa inachelewa.....na ilikuwa ni kawaida kabisa, hususani kwa halmashauri, ku-debit account zao kulipia mishahara na kisha kurejesha cheki za mishahara zinapowafikia. nakumbuka niliwahi hata kuwashauri wenye benki yao tuanzishe product ya salary advance for gvt employees ambayo tungeweka some interest.
 
izo sekta binafsi,labda kwa vibarua sio waajiriwa,tar ya mshahara ni kuanzia 21-25,mpaka apo esabu maumivu,serikal kushney...

Hapa ndipo ninapopata taste ya ile wanayoilalamikia CDM...."CCM wasijifanye wasemaji wa vyama vingine!" Je, nikuletee mkataba wangu wa kazi ili uone kama sijaajiriwa?! salary yangu ya October 2011 nilipata November 03; na hii ni kwa wenzangu wote na hakuna kibarua hapo!
 
Alichokililia na kutumia pesa nyingi vile.....amekipata....!!!anajuta!!
 
izo sekta binafsi,labda kwa vibarua sio waajiriwa,tar ya mshahara ni kuanzia 21-25,mpaka apo esabu maumivu,serikal kushney...
Sekta binafsi kwa Wahindi ni noumer mkuu....ngoma inaweza kusubiri mpaka mwezi unaofuata! teh teh...!
 
Wanaokudai waambie wasubiri mwisho wa mwezi. Leo ni tar 25, bado siku tano.
 
wanajf salaam!
hivi ni kweli kwamba hali ya serikali ni tete kiasi cha kuchelewesha mishahara ya wafanyakazi mpaka sasa?
nikiwa miongoni mwa wafanyakazi wa umma,nimepata salary slip yapata 4 days now ila hundi ya mshahara haijapelekwa bank,nimemuuliza mhusika w kwa hapa ofisini kwetu anasema serikali haijaleta pesa wao wametoa slip in advance tu.
mwezi uliopita kuna mjumbe wa jf alitoa mada hii mimi sikutilia maanani kwa kuwa mwezi ulopita sisi tulipata mishahara mapema ila sasa nadhani ndio zamu yetu....
duuu napata hofu na muelekeo wa serikali yetu.au ndo ule msemo kuwa 'nchi imeshauzwa?'

nawasilisha.

Mliimchagua wenyewe huyo JK last year, subirini mnae huyo hadi 2015. Mtavuna mlichopanda
 
Back
Top Bottom