Hali ya maisha katika Jiji la DSM

O-man

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
323
65
Katika hali ya kusikitisha na kukatisha tamaa, maisha, ambayo nayaita ya kawaida, katika jiji letu, yameota mbawa. Hata bamia limekuwa ni anasa - kilo moja ni shilingi 3,000. Najiuliza maswali lakini nachelea kutoa majibu. Hivi wapo viongozi ambao wanaguswa na hali hii? Huyu mtu ambaye katika kukuru kakara zake amefanikiwa kupata unga kwa ajili ya ugali, mboga ya rahisi na ambayo wengi wetu imetutoa mbali imekuwa tunu? Nyama, maharage na samaki ni mboga za siku za mshiko tu. Mtu huyu ana akili timamu na siku akisema hii inatosha, sikubali, lazima hali ibadilike, lolote na liwe. . . Atalaumiwa kweli? Najuwa fika likitokea hili vipo vyama vitabebeshwa mzigo wa lawama. Ukweli utabakia pale pale - viongozi wetu, kwa sababu wameshiba, wamesahau waliowaweka madarakani. Kama kipo kidogo basi tugawane ili atakayelalamika tumuone mlafi. Inauma sana.
 
ccm oyeee!
 
Chama cha wamiliki daladala nao wamecharuka wametuma maombi SUMATRA kuomba nauli zipande..
 
Ni kweli ccm oyee! Naona mboga ishamwagwa, huo ugali sijui itakuwaje.
 
Chama cha wamiliki daladala nao wamecharuka wametuma maombi SUMATRA kuomba nauli zipande..

Ilianza TANESCO, wakafuata watengeneza vinjwaji, sasa daladala, who is next..........? na siku malji akigoma aingie barabarani kupinga?
 
Hayo ndiyo maisha ya bora kwa kila mtanzaniaaaa..............Acha kuhoji si ulipewa furana na kofia??
 
sio huko tu dar hata huku Arusha balaa uzuri wa dar vidagaa vya baharini vipo huku hakuna japo mbogamboga kibao yote Tumwachie MUNGU tu ipo cku
 
Back
Top Bottom