Hali ya kiafya ya mama mzazi wa mbunge Chiku Abwao si nzuri

Jun 9, 2011
16
7
[h=3][/h]
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mhe.Chiku Abwao akimuuguza mama yake mzazi Tatu Abdallahman (79) ambaye amerejeshwa hospitali na kutibiwa nyumbani kwake Gangilonga mjini Iringa mgonjwa huyo anasumbuliwa na matatizo ya mshtuko wa moyo na kupelekea kupooza mguu wa kushoto na mkono hali iliyomlazimu mbunge Abwao kusitisha kuhudhuria kikao cha bunge Dodoma na kurudi kuuuguza mzazi wake huyo MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha Demokrasi na maendeleo (CHADEMA) Chiku Abwao amelazimika kuomba ruhusa bungeni na kurudi nyumbani Iringa kumuuguza mama yake mzazi Tatu Abdallahman (79) ambaye hali yake kiafya ni mbaya zaidi.

Akizungumza na mtandao huu leo nyumbani kwa mbunge huyo eneo la Gangilonga ambako kwa sasa mama yake yupo baada ya kutolewa Hospital ,Abwao alisema hali ya mgonjwa wake si nzuri sana hali ilkiyomlazimu kurudi kutoka bungeni na kuja kumuuguza .

Alisema kuwa mama yake ambaye wiki moja kabla alikuwa amezidiwa kupitia kiasi anasumbuliwa na tatizo la mshtuko wa moyo ambalo limepelekea kwa sasa baadhi ya viungo kupooza .

Abwao alisema kuwa kabla ya kulazwa katika Hospital hali yake ilikuwa ni mbaya zaidi na kuwa kwa sasa hali yake japo imeendelea kuwa nzuri ila tayari amepooza mkono wa kushoto na mguu na kuwa amekuwa ni mtu wa kushinda amelala na akijitahidi sana amekuwa akiishia kukaa juu ya kitanda chake.

Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa daktari wake amekuwa akifika kumtibu nyumbani japo bado kupona kwake tatizo hilo anamtegemea zaidi mwenyezi Mungu.
 
What do you want to potray???!!!!, Jaribu jukwaa la afya
 
Mungu awatie nguvu nyote mnaouguza na Mungu atawalipa. Mungu kwa majaliwa yake atamponya na kurudi tena kufanya kazi zake.
 
What do you want to potray???!!!!, Jaribu jukwaa la afya
We kweli kilaza! siku nyingine uwe unajipanga kabla ya kucomment. Chiku ni mpiganaji mwenzetu so taarifa kama hii lazima iwepo hapa ili tumtie nguvu mwenzetu katika kipindi hiki kigumu.
 
Back
Top Bottom