Hali ya hewa Qatar yazua mzozo Fifa

Ehud

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
2,685
337
Tuesday, 23 November 2010 20:46
0
digg

LONDON, Uingereza

KAULI kuhusu hali ya hewa ya joto na jinsi inavyoweza kuikosesha nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 imezua mzozo baina ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya Fifa.

Mzozo wa sasa ni baina ya Mohamed Bin Hammam, raia wa Qatar ambaye amehoji kauli ya mwenzake wa Marekani, Chuck Blazer aliyesema hali ya Qatar ni ya joto mno kiasi kwamba haifai kuwa mwenyeji wa fianali hizo za 2022.

Blazer alisema wiki jana kwamba Bin Hammam na nchi yake, Qatar wanaweza kuweka vipoza hewa katika viwanja vyote, lakini hawawezi kupoza hewa ya nchi nzima.

Kauli hiyo ya Blazer iliungwa mkono na kamati ya ufundi ya Fifa katika ripoti iliyoeleza kuwa kuipa nchi hiyo uenyeji wa fainali hizo kutakuwa na athari kiafya.

Wastani wa joto katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati inafikia nyuzi joto 106 Fahrenheit.

Lakini, Bin Hammam amemnyooshea kidole Blazer akieleza kuwa joto kali pia ni suala ambalo linayakumba baadhi ya maeneo ya Marekani, lakini mwaka 1994 ilipewa uenyeji huo.

“Mwenzangu aliponiuliza nitoe maoni kuhusu joto kule kwetu kwamba ingewaathiri wachezaji na maofisa , nilimkumbusha mambo mawili ” alieleza Bin Hammam.

“Kwanza : Mabadiliko ya teknolojia na suluhisho ambalo Qatar inaweza kutumia katika viwanja vyake ili kukabiliana na changamoto zote zinatokana na joto.

Pili : Sijui kama anakumbuka au la mambo yalivyokuwa kule kwao (Marekani) mwaka1994 , ambako baadhi ya mechi zilichezwa saa 6 mchana huku joto likuwa kali hadi kufikia nyuzi joto 50 Celsius (nyuzi 122 Fahrenheit).”

Bin Hammam alieleza kuwa mashabiki wa Marekani walisahau joto na ndiyo maana wanaomba tena uenyeji wa fainali za 2022, ikiwa ni miaka 16 tangu walipopewa naasi hiyo.

Maombi ya Marekani yaliongezwa nguvu wiki jana baada ya Chama cha Ligi Kuu (MLS) kueleza utayari wake wa kubadili ratiba za mechi zake wakati wote wa fainali hizo ili kwenda sambamba na mapendekezo ya Rais wa Fifa, Sepp Blatter.

Blatter ameeleza kuwa mfumo wa sasa wa ligi hiyo inayofanyika Machi-Novemba itaikosesha nafasi Marekani ikilinganishwa ligi nyingine zikiwamo za Ulaya ambazo wakati huo huo zipo likizo.
Qatar, Marekani zinachuana na Australia, Japan na Korea Kusini kuwania uenyeji wa fainali za 2022.

Bin Hammam, Blazer and Blatter are on the FIFA executive committee that will vote on the 2018 and 2022 hosts in Zurich on Dec. 2.

Idadi ya wapigakura wa kuchagua mwenyeji huyo imebakia 22 baada ya mjumbe wake kutoka Nigeria, Amos Adamu na mwenzake wa Tahiti, Reynald Temarii wamefungiwa kati ya mwaka na mitatu kwa tuhuma za kupokea hongo.

Wawili hao walifungiwa na kamati ya maadili ya Fifa, ambako Adamu amezuiwa kujishirikisha na soka kwa miaka mitatu na Temarii mwaka mmoja. Temarii, ndiye Rais wa Soka wa Oceania.

Juzi, makamu rais wa Fifa, Chung Mong-joon alisema wajumbe wamepewa adhabu kali mno.
 
Back
Top Bottom