Elections 2010 Hali si shwari CHADEMA...!?

kanda2

JF-Expert Member
Apr 22, 2007
1,318
72
Chadema leaders in Tarime move to CUF

By DAILY NEWS Reporter,
13th August 2010

Political wind has hit hard Chadema in Tarime District, Mara Region where hundreds of its members returned their membership cards in protest of what has been described as prejudice.

Speaking on behalf of others, the former Chadema District Secretary, Mr Joseph Anthony said the party supporters decided to join the Civic United Front (CUF) as the best way to express their grievances.

"We (former Chadema members) are terribly disappointed by the higher party authorities that have decided to nominate wrong candidates for parliamentary and councillorship seats. We are not ready to work with leaders imposed on us," Joseph explained.

Other party leaders in the district who defected to CUF include the party's district chairman, Mr Stephen Gesengewa (Sanifu), personal secretary to the former legislator, Mr Charles Mwera, the district youth chairman, Mr Jumanne Mroni, the youth commander, Waiboga Waryoba and others.

The fact that the former legislator for Tarime Mr Charles Mwera was not nominated in the party's preferential votes, was also expected to join the CUF and vie for the seat through CUF.

According to CUF district secretary, Ms Theresia Mkami and the party's district chairman, Mr Charles Nyamuriba, more than 200 former Chadema members joined CUF. She said for the last three weeks CUF had received nearly 600 new party members from other parties in the area.

"Any moment from now we expect to receive Mr Charles Mwera, the former legislator on the ticket of Chadema," Theresia revealed.

Mnalo hilo limewaganda!
 
Hii sio habari nzuri kwa CUF na kwa Chadema pia, watakaonufaika na mgawanyiko huu ni CCM, ni vyema viogozi wa Chadema wakakaa na watu hawa ili waumalize huo mfarakano kwa faida ya upinzani.
 
Hii sio habari nzuri kwa CUF na kwa Chadema pia, watakaonufaika na mgawanyiko huu ni CCM, ni vyema viogozi wa Chadema wakakaa na watu hawa ili waumalize huo mfarakano kwa faida ya upinzani.

Ni kweli sio habai nzuri ,hata mimi sikupendelea kuona mass exodus wanaihama Chadema katika dakika za mwisho ,ila hapa inaonekana kuna jambo haiwezekani watu wahame tu hivihivi ni lazima wameanza watu wameanza kuzinduka,kwa upande mwengine watu kuhama chama kimoja kwenda kingine sio hatari kubwa,ingelikuwa tishio kama ingekuwa wanarudi kulekule tulikotoka yaana wanarudi CCM,ila vyama vinahitaji kuweka mambu yao sawa kama CUF kwani hatukusikia malalamiko ,Mi nilijua tu kama Chadema amna kitu ,sasa mambo hayo yanakuja juu.
 
Acha wahame kwani hatutaki siasa za personality kama huko CCM.Sasa kama kura za huyo Mwera hazikutosha bado hao wababaishaji walitaka apitishwe hivyohivyo?Utiifu kwa mtu badala ya chama ni mithili ya umwinyi.Kwani Chadema walishinda by-election kwa kura 200 au maelfu?Good riddance.

By the way,magazeti ya CCM yamekuwa busy kweli kusaka habari za kuwavunja moyo Chadema.
 
Ni kweli sio habai nzuri ,hata mimi sikupendelea kuona mass exodus wanaihama Chadema katika dakika za mwisho ,ila hapa inaonekana kuna jambo haiwezekani watu wahame tu hivihivi ni lazima wameanza watu wameanza kuzinduka,kwa upande mwengine watu kuhama chama kimoja kwenda kingine sio hatari kubwa,ingelikuwa tishio kama ingekuwa wanarudi kulekule tulikotoka yaana wanarudi CCM,ila vyama vinahitaji kuweka mambu yao sawa kama CUF kwani hatukusikia malalamiko ,Mi nilijua tu kama Chadema amna kitu ,sasa mambo hayo yanakuja juu.

Very strange, learning from experience; i thought that we shared the same feelings; these names, Mwiba, MS, Kanda, Junius would rather see their fellow opposition parties demise so as to leave them as a sole opposition party. Go and fight CCM then you will be stronger than fighting CHADEMA; Chadema I am seeing has taken a very diiferent path, they don't fight CUF, they are fighting the party in power which has made things worse for the people.

CUF wakeup, you have nothing to gain by fighting CHADEMA, overall CHADEMA is supporting you!!
 
Chadema u just move on. Msibabaishwe na hisia za watu. Fanyeni lile lililo bora kwa jamii na si kiongozi mmoja mmoja
 
Go Mwera, Go...... CHADEMA sio yako pekee ni yetu sote.........pamoja na wewe.
 
DAiLY NEWS IN ACTION

Jimbo la Tarime lina matatizo siku zote. Sioni kama kuna chama kina advantage kwenye huu mgawanyiko wa wapiga kura. CCM wenyewe wameshindwa kutangaza mshindi wa kura za maoni kwa kuhofia vurugu, wanasubiri kwenda kutangazia matokeo Dodoma ambako wapiga kura hawawezi kwenda kufanya fujo.

Pengo la hao wanaotoka CHADEMA kwenda CUF litazibwa na kura za chuki za wana CCM ambao mgombea wao atakatwa jina lake. Mwisho wa siku bado CHADEMA watashinda.

Daily News (Daily Noise) naona wako kazini kuisaidia CCM, lakini CCM ina kibarua kipevu.
 
Hilo litatokea tu kama mgombea wa CCM atakayetoswa atajitoa kwenye chama na kugombea kwa chama kingine, lakini vinginevyo atakayetoswa ataingia kwenye kampeni kama mpambe mkuu wa atakayepitishwa akipalilia "nafasi yake ya kupoozwa" baada ya uchaguzi.
 
Ndugu zangu wanachadema, salaam ziwafikie hapo mlipo, Nazungumza toka hapa nyumbani , Nashangaa uvumi unaoenezwa na wasiopenda mabadiliko, Ni kweli kuwa kura za ndugu yetu mwera hazikutosha, na hii imefanyika tuu kwa sababu 2

Ndg Mwera alipopata fursa kuingia pale mjengoni hakuweza kuvivaa viatu vya mpiganaji wetu(Chacha) viatu vilimpwaya.

Uwezo wa kujenga hoja nao umeonekana kuwa mdogo, ama ni kwa sababu hakujijenga vema hilo siwezi kulisemea

Ndipo kwa maslahi yetu wanatarime tukaona tuje na mbadala wa Chacha Wangwe(Mwita Mwikwabe)

Hatakuna aliyerudisha Kadi na sisi tunajua CHADEMA waliyoyafanya hapa, wanafunzi kusomeshwa si jambo dogo, Tunajua wala hatudanganyiki hata kidogo

Kama kaka yetu atakihama chama na kuelekea anapajua sisi hatuna cha kusema ila tunamjali na pia yeye ni sehemu ya CHADEMA, mchango wake tunauheshimu sana

Ni yeye aliyeweza kuisimamia halmashauri yetu na tukafanya vyema.na jambo la kuanguka kura za maoni ni jambo la kawaida

CCM hata kama wangekuja na pipi, pelemende hapa hawapati kitu, uwelewa ni mkubwa kwa Dada zetu, mama zetu, Baba zetu na hata wake zetu

Kazi kwenu huko mliko waelimisheni Mama zenu, baba zenu na hata waume zenu nchi ipone

Mwisho, sisi hatuongozwi na fikra za mtu, tunaamini ukweli na si habari za Bi Kilembwe
 
acha wahame kwani hatutaki siasa za personality kama huko ccm.sasa kama kura za huyo mwera hazikutosha bado hao wababaishaji walitaka apitishwe hivyohivyo?utiifu kwa mtu badala ya chama ni mithili ya umwinyi.kwani chadema walishinda by-election kwa kura 200 au maelfu?good riddance.

By the way,magazeti ya ccm yamekuwa busy kweli kusaka habari za kuwavunja moyo chadema.
kaka mwera hakushindwa isipokuwa kura zake hazikutosha,hapo ndipo mtihani unapokuja chadema.angalia mambo ya ukonga utaona ubinafsi na u.....unatawala chadema,hicho sio chama cha kisiasa ni cha burudani tuu.ondokeni huko!
 
Mjumbe mwingine ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema uamuzi wa Mbowe ni wa ‘funika kombe mwanaharamu apite', kwani alijua watu wake wameanguka kwenye uchaguzi huo. "Uchaguzi haukuwa na rushwa bali ni kubwagwa kwa wabunge, Halima Mdee, Susan Lyimo, Anna Komu na Grace Kihwelu, huku Lucy Owenya pekee akipitishwa kutokana na heshima ya mdhamini wa chama, Philemon Ndesamburo,'' alisema mjumbe huyo.

Talk about nepotism....
 
SULEIMAN JONGO NA HAMIS SHIMYE

HALI ya hewa ndani ya CHADEMA imechafuka kutokana na baadhi ya wanachama kusema watapinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa viti maalumu, endapo utakaorudiwa utaendelea kuwa na mwelekeo wa upendeleo.

Kauli hiyo imetolewa siku chache baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe na Msimamizi wa uchaguzi huo, Dk. Kitila Mkumbo, kuuahirisha kutokana na rushwa na ukiukwaji wa taratibu.

Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya chama hicho kilisema wajumbe wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) hawajaridhishwa na uamuzi wa Mbowe.

Wajumbe hao walisema uamuzi wa kuahirisha uchaguzi ulilenga kuwabeba wabunge waliomaliza muda wao, ambao waliangushwa kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Kiramuu, mjini Dar es Salaam.

"Wajumbe hatujaridhika, katika uchaguzi ule tuliamua kufanya mabadiliko na kuleta chama chenye sura mpya, lakini Mwenyekiti amekataa uamuzi wetu na kufuta uchaguzi,'' kilisema chanzo hicho cha habari. Chanzo hicho kiliongeza: "Ukabila tumepania kuumaliza kwa kuanza kubadilisha taswira ya wabunge wote wa viti maalumu kutoka kanda ya kaskazini ili uwepo usawa.''

Mjumbe mwingine ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema uamuzi wa Mbowe ni wa ‘funika kombe mwanaharamu apite', kwani alijua watu wake wameanguka kwenye uchaguzi huo. "Uchaguzi haukuwa na rushwa bali ni kubwagwa kwa wabunge, Halima Mdee, Susan Lyimo, Anna Komu na Grace Kihwelu, huku Lucy Owenya pekee akipitishwa kutokana na heshima ya mdhamini wa chama, Philemon Ndesamburo,'' alisema mjumbe huyo.

Chanzo kingine ndani ya CHADEMA kilisema Kamati Kuu ya chama hicho imeamua mfumo wa kuwapata wabunge viti maalumu usiwe wa kupigiwa kura, badala yake watateuliwa na chama. "Tunayajua aliyoamua Mbowe kwenye Kamati Kuu, kwani hakutakuwa na uchaguzi wa wabunge wa viti maalumu na badala yake watateuliwa na Kamati Maalumu,'' alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Erasto Tumbo, alisema viongozi wa juu walifanya mkutano na leo au kesho watatoa uamuzi wa hatima ya nafasi hizo. "Kikao cha juu ndicho kitaamua. Sijui ni njia ipi itatumika kuwapata wagombea hao kwa kuwa mimi si msemaji wa mambo hayo. Viongozi ndio wenye jukumu la kutoa ufafanuzi na leo au kesho taarifa itatolewa," alisema Tumbo.

Katika siku za hivi karibuni chama hicho kimekuwa kwenye migogoro ya uchaguzi mara kwa mara, hususan kutokana na kuwepo makundi miongoni mwa viongozi wakuu wa chama hicho. Mwaka jana matokeo ya uchaguzi wa Baraza la Vijana la chama hicho (BAVICHA) yalifutwa na uchaguzi kuahirishwa, ambapo aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, David Kafulila, aliamua kukihama chama hicho na kujiunga na NCCR-Mageuzi. Uchaguzi wa BAWACHA pia uliahirishwa kutokana na kuibuka madai ya upendeleo.

Katika hatua nyingine, aliyekuwa mbunge wa Tarime kupitia chama hicho, Charles Mwera, amekihama na kujiunga na CUF, akidai kuwepo kwa ubabaishaji na rushwa.

Jimbo la Segerea pia hali si shwari kutokana na mwanachama aliyebwagwa kwenye kura za maoni katika chama hicho, Fred Mpendazoe kurudishwa kinyemela na kuondolewa mshindi Rachel Mashishanga. Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanachama wamesema wanakihama chama hicho, huku wengine wakisema wataipigia kura CCM

Tusisahau source ya habari hii ni gazeti la Uhuru.
 
mkakati wa ccm wa kununua watz masikini umeeshaanza.................wameanza kuwagawa wenye hekima wanajua na wanachukua hatua.........kazi kwenu mnnunliwao kwa bei chee kiasi hicho
 
Hilo gazeti la daily news hawtaki hata siku moja kwenda vijijini na kuripoti juu ya upungufu wa madawti,walimu,miundombinu mibovu,limekaa kushabikia chama tawala,siku zenu zinahesabika
 
Back
Top Bottom