Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 264
Bunge likiwa hovyo, Rai akiwa hovyo, Waziri Mkuu akiwa hovyo, Upinzani ukiwa wa hovyo matokeo yake ni wananchi wanajichukulia hatua mikononi na kufanya maamuzi magumu. Huu ni Mwanzo tu, Hongera mama Hellen Kijo Bisimba kwa Kuwasha moto, picha yako ina ujumbe mzito kwa kizazi chetu na vizazi vijavyo. Wewe ni shujaa wetu. Heshima mbele mama, umeanza leo, kesho tutamalizia kazi yako. Wasomi wa JF, usomi wenu hauna mana ikiwa hamuwezi kuchukua maamuzi magumu. Nadiriki kuwaiteni wanafiki kwani hamna machungu na nchi yenu zaidi ya porojo.
Hamna uzalendo, mngekuwa na uzalendo, mngetumia elimu zenu kupigania mageuzi na serikali ya kidhalimu tuliyonayo leo. Nadiriki kuwaita wasaliti, kwa maana raia masikini wanaandamani nyie mpo kwenye mitandao. Tulifuzwa leo na polisi, kesho tunarudi..... nyie endeleeni kuandika, kwani huu siyo muda wa kuandika bali muda wa ukombozi dhidi ya udhalimu wa Serikali mbvu ya kishikaji. Tunamuomba Mungu awalete wanaye 5 tu kama mama Bisimba ili tuikomboe taifa letu !