Hali ni tete Mtwara Leo, Sakata ya Gesi

MAKOSHNELI

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
930
1,552
Wakuu,

leo ntwara tangu asubuhi kila huduma imefungwa watu wapo kimakundi makundi wanasikiliza bunge hasa bajeti ya wizara ya nishati na madini,ni magari ya ffu tu ndio yapo barabarani nayo hupata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo yaliyowekwa na vijana,baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari eti kwakuwa walipita jirani na gari yao,askari wengi waliokuja si wa hapa ntwara wengi wametoka Masasi na Lindi.


Kauli mbiu ya huku kwa sasa - "gesi haitoki hata kwa bomba la peni"

attachment.php


=======

attachment.php


MORE UPDATES
MATAIRI KILA KONA YA MJI YAMECHOMWA BARABARANI POLISI NA ZIMA MOTO NDIO WANAKAZI YA KUZIMA NA KUFUKUZA RAIA

TAYARI NYUMBA KADHAA ZA WATUMISHI WA SERIKARI ZIMETIWA KIBERITI MAENEO YA SHANGANI
NTWARA2.JPG

 

Attachments

  • IMG_20130522_100503.jpg
    IMG_20130522_100503.jpg
    194.3 KB · Views: 2,044
  • IMG_20130522_102259.jpg
    IMG_20130522_102259.jpg
    242.2 KB · Views: 35,479
  • IMG_20130522_102325.jpg
    IMG_20130522_102325.jpg
    227.1 KB · Views: 24,272
  • IMG_20130522_102338.jpg
    IMG_20130522_102338.jpg
    260.2 KB · Views: 25,945
  • IMG_20130522_102603.jpg
    IMG_20130522_102603.jpg
    305.6 KB · Views: 39,055
  • NTWARA.JPG
    NTWARA.JPG
    85.2 KB · Views: 718
Hahahahaha ndo kazi iliyobakia kwa hawa polisi wetu,ila nadhani kuwalaumu pia sio sawa kwani waliapa kuilinda katiba ya tanzania na pia kutii amri za wakuu,so wako sawa kabisa nadhani sio sahihii kabisa kuwalaumu hawa watu
 
Yaani hapo ndiyo Ccm inachukiwa sana
badala ya kusikiliza matatizo wao wana
peleka Polisi.
Wanaandaa vipindi eti Lindi&Mtwara
itakuwa kama Ulaya.

Huku Prof wa Wizara anasema gesi ndiyo
engine ya Nchi hii.
Liwalo naliwe

Kauli Mbiu ni nzuri sana
"'Gesi Haitoki hata kwa Bomba la Pen""
 
Wana Mtwara komaeni tupo pamoja; Siyo kila kitu Dar es Salaam, kwani nyie wana wa Mtwara hamtakiwi kufaidika na raslimali zenu ?.
 
"'Gesi Haitoki hata kwa Bomba la Pen""

Tuko pamoja wana mtwara na wanakusini kwa ujumla, na hiyo kauli mbiu idumu.
 
Kudaadeki magamba mpaka ya=nye blood!! Ntwara citizens have been pushed to the wall till they have found they have nothing to loose! Kufa ni kupumzika kwa watu walioteswa na mashetani ya CCM kihivyo!!
 
Nimesikia wamekata matangazo ya Radio na TV huko Ntwara ili wasisikilize kinachoendelea Bungeni.
mlioko huko tupeni habari kamili.
 
Ni baada ya kukunwa na hotuba ya waziri wa nishati wakati anawasilisha hotuba yake kuwa gesi itawanufaisha kwanza wanamtwara na mikoa ya jirani kabla ya maeneo mengine ya nchi..vijana wanasherehekea mitaani na kumpongeza muhongo
 
baada ya kutoridhishwa na bajeti ya nishati na madini vurugu zimeshaanza mitaa ya Magomeni, Soko kuu na Coco beach Pande za mtwara ....
nimetulia ndani naskizia mabomu yanavurumishwa ...
for more updates stay tuned ....
 
By MAKOSHNELI 11:20 Today

Wakuu,
leo ntwara tangu asubuhi kila
huduma imefungwa watu wapo
kimakundi makundi wanasikiliza
bunge hasa bajeti ya wizara ya
nishati na madini,ni magari ya ffu
tu ndio yapo barabarani nayo
hupata wakati mgumu kupita
kwasababu ya mawe na magogo
yaliyowekwa na vijana,baadhi ya
watu kadhaa wamechukuliwa na
askari eti kwakuwa walipita jirani
na gari yao,askari wengi waliokuja
si wa hapa ntwara wengi wametoka
Masasi na Lindi.

Kauli mbiu ya huku kwa sasa -
"gesi haitoki hata kwa bomba la
peni"
 
Wadau,niko maeneo ya magomeni mtwara muda huu polisi wanarusha mabomu na risasi kila pembe,ni mtafaruku huduma zote zimesitishwa,wananchi wanataka kujua hatma ya gesi kusafirishwa kwenda Dar.Hali si shwari kabisa na ikumbukwe huu ni muendelezo wa tukio kama hili siku ya ijumaa iliyopita!
 
Back
Top Bottom