Hali ni tete mkoani Manyara; mwekezaji achinjwa!

Polisi nchini Tanzania inapeleleza mauaji ya meneja na muwekezaji nchini humo Sifael Jackson. Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara kaskazini, Parmena Sumari ameiambia BBC kuwa maofisa wake wanaendelea kuwasaka wauaji wa mfanyabiashara huyo. Mwandishi wa habari Benny Mwaipaja ameiambia BBC kuwa marehemu alivamiwa na kuuawa na genge lililokuwa na mikuki, magongo na mapanga akiwa ndani ya gari lake. Mauaji haya yanatokea wakati kukiwa na upinzani mkubwa wa raia dhidi ya mpango wa serikali wa kupigia debe uwekezaji wa kilimo kwa kiwango kikubwa.

Uvamizi

Mwandishi huyo aliendelea kusema kuwa "Bw Jackson aliuawa kinyama na kukatwa kichwa na genge la hadi watu 15 siku ya Jumanne jioni. Baadhi ya wakaazi wa mkoa huo wa Manyara wanaishutumu serikali kwa kutishia hali yao ya maisha kwa kugawa ardhi yao vipande vikubwa kwa wakulima wa kibiashara wa mashamba makubwa, wakiwemo wakulima wa kigeni. Lakini serikali inasema kuwa lengo la sera hiyo ni kujaribu kuimarisha uzalishaji wa chakula na kuhakikisha kwamba ardhi inatumiwa kikamilifu.

Kwa uchache mashamba manne yamevamiwa mwaka huu karibu na mji wa Babati huko Manyara, ambako mazao yalichomwa na mali kuteketezwa kwa moto. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alituma ujumbe mkubwa wa Mawaziri wa serikali kwenda kupeleleza kuhusu mzozo huo. Ujumbe huo uliwaonya wananchi katika maeneo walioyazuru dhidi ya vitendo vyao vya kuvamia na kuteketeza mali za watu la sivyo watakamatwa na kuhukumiwa.

Mwandishi huyu Mwaipaja alisema kuwa serikali ina wasiwasi kuwa ghasia hizo sasa zinaweza kuikosesha Tanzania wawekezaji ambao ina imani wangeweza kusaidia mpango wake wa kijani.Kampeni ya serikali ya kutaka kilimo cha kiwango kikubwa kibiashara ni mabadiliko makubwa ukizingatia sera zilizokuwepo baada ya Uhuru zilizokuza na kupendelea Usoshalisti.

BBC Swahili - Habari - Mkulima auawa kinyama Tanzania
 
Polisi nchini Tanzania inapeleleza mauaji ya meneja na muwekezaji nchini humo Sifael Jackson.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara kaskazini, Parmena Sumari ameiambia BBC kuwa maofisa wake wanaendelea kuwasaka wauaji wa mfanyabiashara huyo.

Mwandishi wa habari Benny Mwaipaja ameiambia BBC kuwa marehemu alivamiwa na kuuawa na genge lililokuwa na mikuki, magongo na mapanga akiwa ndani ya gari lake.

Mauaji haya yanatokea wakati kukiwa na upinzani mkubwa wa raia dhidi ya mpango wa serikali wa kupigia debe uwekezaji wa kilimo kwa kiwango kikubwa.

Uvamizi

Mwandishi huyo aliendelea kusema kuwa "Bw Jackson aliuawa kinyama na kukatwa kichwa na genge la hadi watu 15 siku ya Jumanne jioni.

Baadhi ya wakaazi wa mkoa huo wa Manyara wanaishutumu serikali kwa kutishia hali yao ya maisha kwa kugawa ardhi yao vipande vikubwa kwa wakulima wa kibiashara wa mashamba makubwa, wakiwemo wakulima wa kigeni.
Lakini serikali inasema kuwa lengo la sera hiyo ni kujaribu kuimarisha uzalishaji wa chakula na kuhakikisha kwamba ardhi inatumiwa kikamilifu.

Kwa uchache mashamba manne yamevamiwa mwaka huu karibu na mji wa Babati huko Manyara, ambako mazao yalichomwa na mali kuteketezwa kwa moto.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alituma ujumbe mkubwa wa Mawaziri wa serikali kwenda kupeleleza kuhusu mzozo huo.

Ujumbe huo uliwaonya wananchi katika maeneo walioyazuru dhidi ya vitendo vyao vya kuvamia na kuteketeza mali za watu la sivyo watakamatwa na kuhukumiwa.

Mwandishi huyu Mwaipaja alisema kuwa serikali ina wasiwasi kuwa ghasia hizo sasa zinaweza kuikosesha Tanzania wawekezaji ambao ina imani wangeweza kusaidia mpango wake wa kijani.

Kampeni ya serikali ya kutaka kilimo cha kiwango kikubwa kibiashara ni mabadiliko makubwa ukizingatia sera zilizokuwepo baada ya Uhuru zilizokuza na kupendelea Usoshalisti.
 
sasa viongozi wetu badala ya kutafuta ufumbuzi wa kumaliza tatizo utasikia wamechochewa na chama fulani
 
Problem ni kwamba matunda ya uwekezaji hayagawanywi sawasawa.wananchi hawaoni utamu wa uwekezaji,wanahitaji direct impact na sio kuambiwa pato la taifa linakua bila kuona maendeleo.mfano shule wanajijengea wenyewe,maji wanachimba wenyewe,umeme gharama ya kuweka nguzo ni juu n.k
ni ngumu mwananchi huyu kumuambia mwekezaji ana faida kwake.
 
mkulima wa tanzania anachotaka ni kuwezeshwa alime mwenyewe sio kumdidimiza kwa kumnyang'anya ardhi! Nakumbuka kuna makala ndefu ilichapishwa gazeti la raia mwema ikishutumu sera ya kilimo kwanza kuwa ni ukoloni hakuna aliesikia! Kwa nini hatujifunzi zimbabwe, kenya na africa ya kusini?, wakulima wakubwa wakiwa wageni ni hatari kwa usalama na uhuru wa mwananchi! Mi naona kama mabilioni ya kikwete wangepewa wakulima watanzania ingefaa zaidi kuliko ilivyo sasa! MAKUBWA ZAIDI YANAKUJA
 
labda yeye ndiyo alikuwa na kiherehere. Wazungu wakifia wanatoa post kubwa kwa wabongo ili waweze kutumia ubongo wao kurubuni watu au hata kuwalaliia haki zao. Sasa imefika mwisho. Huo mgogoro nakumbuka sasa kama na vifo vimetokea kazi imeanza.
 
wabaya ni sisi wenyewe, tuna-colude na wageni kudhuru ndugu zetu, usishangae jina kuwa la kitanzania, waliotenda jambo hilo inaelekea wanajua mbaya wao nani.
 
Wana JF,

Nadhani huwa mwakumbuka Mwl.JK Nyerere alisha wahi kuhoji swala la wawekezaji ni watu gani hawa au ni wana rudisha utumwa na akatoa mfano wa boxing umchukue mtu wa Heavy Weight na middle weight uwagombanishe inakuja kweli. sasa ndio hayo mambo ya serikali yetu ilikubali uwekezaji kumbe wao viongozi walikuwa na lao jambo kuwatumia hao wawekezaji wao walio waleta ili kuwanyonya wananchi na leo hii wanac=shindwa ni jinsi gani ya kutatua matatizo yao na wananchi na ndio maana serikali haiko makini na wanannchi wake sasa huko wamechinjana na bado huko viwandani mahotelini na makampuni ya hao wawekezaji kuta mwagika damu nchi hii na hili litakuwa juu ya hawa viongozi wetu wasio soma alama za nyakati kila waambiwalo wao ni kudhani upinzani yani wanakuwa na mawazo finyo sana. Ubinafsishaji umeiteka Serikali,TRA,PCCB,POLICE,MIGRATION yaani wewe mwananchi uka report kwa hivyo vyombo hapo ni kazi bure tuuu ni kama watwanga maji kwa kinu ati.
 
Tatizo la serikali yetu ni kukosa ubunifu, uzalendo na kuendekeza tamaa! Anakuja anayejiita mwekezaji, badala ya kutafuta/kutafutiwa eneo jipya, wanampa eneo ambalo wana wa nchi wamekuwa wakijipatia riziki zao kila siku. Tena unakuta ni mali ya kijiji na hawashirikishwi! Wanafukuzwa kama wavamizi bila kujali kesho yao. Mvamizi anafanywa mfalme/mungu mtu na wenyeji ni kama matonya! Mvamizi anapewa ulinzi na dola na wananchi wanakuwa ndio wahalifu! Huu ugomvi hauwezi kwisha! Labda aje masia...
 
tutajie mwekezaji basi!

Wawekezaji ni wahindi mmojawapo ni huyo mbunge wa babati vijijini, na kwa msaada wa hao wafanyakazi wao weusi hunyanyasa sana raia hadi wengine hulawitiwa ila polisi wanapiga kimya so kuuliwa kwa huyo meneja ni funzo kwa viherehere wao ambao husaliti raia wenzao afu hao maponjoro wana kiburi saana sijui nani anawalinda hawaheshimu
Raiaa hata kidogo
 
Wawekezaji ni wahindi mmojawapo ni huyo mbunge wa babati vijijini, na kwa msaada wa hao wafanyakazi wao weusi hunyanyasa sana raia hadi wengine hulawitiwa ila polisi wanapiga kimya so kuuliwa kwa huyo meneja ni funzo kwa viherehere wao ambao husaliti raia wenzao afu hao maponjoro wana kiburi saana sijui nani anawalinda hawaheshimu
Raiaa hata kidogo

hivi serikali haiwezi kabisa kuingilia haya mambo na kuyamaliza?????watanzania jifunzeni gharama ya
kukabidhi wahuni serikali!!!!!!naomba isirudiwe tena
 
hivi serikali haiwezi kabisa kuingilia haya mambo na kuyamaliza?????watanzania jifunzeni gharama ya
kukabidhi wahuni serikali!!!!!!naomba isirudiwe tena

Serikali hii ya ccm!? Tena ccm ya JK!? Haiwezi hata kidogo! Wala hawathubutu hata kuuliza! Tunachoweza kusikia kutoka kwao ni "mgogoro huu unachochewa na mbunge wachama flani (cdm?), ametoka kwenye jimbo lake amekwenda kuchochea mgogoro kule. Tunamfahamu, jana nilimsema na leo nasema tena". Hii unaweza kuisikia kutoka kwa waziri kwa niaba ya serikali!
 
watu wana hasira na kile kinachofanywa na serikali. ingawaje jambo walilofanya kujichukulia sheria mikononi hilo ni kosa la jinai. wawekezaji ni njia moja wapo kwa baadhi ya viongozi walio serikalini kujitafutia utajiri wa haramu. Kilimo kwa tanzania si kitu cha kuwawekeza watu kutoka nje. ikiwa 70% ya hao viongozi imetoka katika familia za wakulima. mfumo ni kuwawezesha watanzania wenyewe kwenye kilimo cha kisasa haswa kwa kutumia mashine. tanzania sio maskini bali mfumo wa watu wachache na ubinafsi ndio unaoleta njaa. Kwa mapesa yote hayo yaliyoibiwa mfano pesa za rada ikiwa zitawekweza kwa wakulima wazwawa hamsini tu kwa vifaa vyote vya kilimo kwa mkopo basi baada ya miaka miwili tu tanzania kutakuwa hakuna njaa. Hamna familia tanzania ambayo aigusi ukulima. sasa kitendo cha kusema wanawekeza katika kilimo huo ni unyanyasaji kwa watanzania.
 
Back
Top Bottom