Hali ni mbaya Muhimbili

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
Sijasimuliwa nimetoka sasa hivi muhimbili, hali ni ya kuhuzunisha sana wagojwa ambao wanahitaji msaada wa daktari hawana la kufanya hakuna Daktari yeyote zaidi ya manesi ambao wapo wodini tu nafikiri kulinda usalama wa mashuka. Viongozi wanaohusika wakae na hawa madaktari ili kuokoa maisha ya watu wasio na hatia, hakuna sababu kabisa ya kuvutana, suluhu ni kufikia muafaka. inasikitisha sana. Uuungwana ni kusikiliza na kufanya maelewano kuokoa maisha ya watanzania wasio na hatia. hii ni laana kwa taifa damu hii itakuwa juu ya wahusika!!!
 
Yuko wapi Profesor Sarungi? huwa huyu mzee ana moyo wakujitolea mno!
 
Acha wafe wakome waliambiwa serikali hii ya mapungwani wakabisha..ma dokta hasa wewe dokta chichi gomeni milele..tena ikibidi mpasue hata na thermometer na darubini kabisa
 
Ki ukweli ni busara ya hali ya juu sana inahitajika katika kufikia maamuzi na muafaka wa suala hili,vinginevyo hali itakuwa mbaya sana.
 
watu wanakufa,yeye analipua milioni 300 kwa safari ya siku 4 ambayo haina faida!!kweli madaktari kuna kichwa walikiwekea nazi..
 
Acha wafe wakome waliambiwa serikali hii ya mapungwani wakabisha..ma dokta hasa wewe dokta chichi gomeni milele..tena ikibidi mpasue hata na thermometer na darubini kabisa

Mkuu, wa kukoma hapo nani sasa...wanaokufa ni raia wasio na hatia, wenye makosa au labda wanaotakiwa kukoma ni serikali ambao wao hawatakufa kwasababu Agha khan, regency nk zinafanya kazi na ndiko wanapotibiwa wao.
 
Nadhani anasema hivyo kwa sababu wao ndio walimchagua huyu muuza sura kuingia ni magogo.
 
Kama ingeliwakuwa Apollo Hospital ungeona Mafisadi wakikaa meza moja na Madaktari, Lakini ni wa Muhimbili ambako wao hawakujali na wala hawana mpango kwa kuwa ni hospital za walalahoi. Subirini mpaka siku za uchaguzi ndio mtaonekana thamani zenu walalahoi
 
alafu wewe muanzisha mada ni MWALIMU maana wao ndo wanafanywa misukule,kwani madaktari ni mungu kuzuia vifo!? Hacha kuchanganya watu,waliambiwa wasichague huu mzimu wakauchagu. sasa waache wanaojua kupigania haki waipiganie.nyie walimu endelea kunyamaza msituletee mambo ya ajabu!! Shwaini!!
 
HIZO MIL300 ZA SAFARI Ya kikwete zingeongezewa kwenye bajeti ya MADAKTARI WAKATI WANASUBIri maKUBaliNO RAsmi,jambo moja ambalo tunatakiwa kujua ni kwamba serikali ya ccm wana dharau sana,tatizo letu watanzania hatujui haki zetu za kuwawajibisha hawa wapumbavu!
 
Am not ashamed to be Tanzanian, but to have this Governance in my Lovely Country.
Mungu atatulipia one day, tena hapa hapa duniani
 
Sijasimuliwa nimetoka sasa hivi muhimbili, hali ni ya kuhuzunisha sana wagojwa ambao wanahitaji msaada wa daktari hawana la kufanya hakuna Daktari yeyote zaidi ya manesi ambao wapo wodini tu nafikiri kulinda usalama wa mashuka. Viongozi wanaohusika wakae na hawa madaktari ili kuokoa maisha ya watu wasio na hatia, hakuna sababu kabisa ya kuvutana, suluhu ni kufikia muafaka. inasikitisha sana. Uuungwana ni kusikiliza na kufanya maelewano kuokoa maisha ya watanzania wasio na hatia. hii ni laana kwa taifa damu hii itakuwa juu ya wahusika!!!

Utasikia Radio one baadaye ikitangaza kwamba hakuna Daktari aliyegoma, nachukia sana vyombo vya habari kutumika katika propaganda
 
hapa media nazo zinaleta propaganda na kuwa emotionally moved wakati hapa kuna hoja za msingi, kweli siasa zinatumaliza maana kila mtu ni siasa tu lakini sote tukumbuke jamani: madaktari sehemu kubwa ya professional yao ni kazi na sio siasa kama tunavyotaka kuaminishwa!
Utasikia Radio one baadaye ikitangaza kwamba hakuna Daktari aliyegoma, nachukia sana vyombo vya habari kutumika katika propaganda
 
Mkuu, wa kukoma hapo nani sasa...wanaokufa ni raia wasio na hatia, wenye makosa au labda wanaotakiwa kukoma ni serikali ambao wao hawatakufa kwasababu Agha khan, regency nk zinafanya kazi na ndiko wanapotibiwa wao.

kwani kumchagua ****** sio hatia??
 
Mbona kamati za binge hazikosi hela maana wanaenda mpaka nje ya nchi?
 
Hatuwezi kufanikiwa kwa porojo, tukitanguliza utu mbele wakati viongozi wetu hawana huo utu. Labda tutafute njia nzuri ya kutatua hilo tatizo.

1) Pengine hapa kuna haja ya kuanza kuangalia namna ambavyo serikali inashughulikia masuala yanayogusa moja kwa moja maisha ya watu wake. Hapa ikiwezekana watu wapewe demo kwa kuwarudisha madaktari kazini, lakini game iendelee mtaani kwa maandamano yasiyo na kikomo.
2) Kuna haja ya kuwa na wasemaji wa jamii zetu wasio wanasiasa wala wa mlengo fulani ili kukomesha hii tabia ya viongozi wetu kujiona miungu watu, kiongozi akifanya madudu lazima awajibike. Na hili lazima liwekwe kwenye katiba mpya.

3) Jeshi la wananchi kazi yake ni kulinda usalama wa raia na mali zao, wachukue nafasi wakati mazungumzo yakisubiriwa, sijui ni lini. Lakini nalo liko hoi! wataalaamu wa jeshi wamebaki kula vitimoto migombani.
 
Back
Top Bottom