Hali kama hii unaweza kumkubalia mkeo awe muigizaji?

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
leo-9.jpg
 
arghhhhh..kwani nini cha ajabu hapo??....acha wivu kwa mkeo kaka...kazi hiyo inaleta kipato cha familia....

NI MAONI TU WADAU ILA YAMEJAA MTAZAMO WA KUWAWEZESHA WANAWAKE WASIENDELEE KUWA JINSIA TEGEMEZI
 
Thubutuuuuuuuu! Mimi hata kama mkisema nina wivu sikatai, ila SIWEZI KUMRUHUSU!
 
Kwani kuna tatizo inabidi mjenge mazingira ya kuamiana ....hehehe inaonekana mwenzetu unaweza kupasua TV
 
vipato vingine ni vya laana wandugu. hapa kiukweli hakuna kuaminiana kama mnavyotaka tuamini. ndoa ya tyson na monalisa iko wapi? ndoa ya hale beri iko wapi? mahusiano ya mastaa wengi kila siku tunasikia yako kikaangoni. ukweli wa nafsi wanawake wengi waigizaji huangukia mapenzini na wale wanaoigiza nao. kama utavumilia hilo hapo sawa, ila si kuamini kuwa mkeo hafanyi kufuru nje ya mahusiano yenu. asilimia 90 ya mabinti wenye majina bongo wana kashfa nyingi za ngono. ukimruhusu mke/mume kufanya scene kama hizo is at your own risk!
 
Mhuu,Yaani hapo sijuhi!tatizo hawa waigizaji wetu wa bongo,pia sio wavumilivu.akiona kitu kimenoga hata km cha mtu,atakukuruka nacho.kwani hamjasikia mtu mmoja alitoa nyumba yake warekodie movie,akakuta zilizotumika zimesahaurika hapo...achana kabisa na mwanamme wa kibongo.Kumwachia mke wako tena katika mazingira hatarishi ni sawa na kumwachia panya paka amchunge.
 
Kwani kuna tatizo inabidi mjenge mazingira ya kuamiana ....hehehe inaonekana mwenzetu unaweza kupasua TV

Kuna sanaa nyingine hmmmmm!Nadhani inakuwa vigumu sana kwa mtu yeyote ambaye siye msanii kumwacha mkewe/mmewe awe muigizaji.Binadamu ameumbwa na some elements za wivu(huu ni ukweli usiopingika), labda iwe hampendani.

Ni vyema basi watu ndani ya sanaa moja(kwa sababu wanaelewa nini maana ya sanaa yao) wakaoana - hapa itakuwa rahisi kutokupata any doubts kuwa mmeo/mkeo "si hali".Ni mtazamo tu, am open to critics!

Nawasilisha!
 
vipato vingine ni vya laana wandugu. hapa kiukweli hakuna kuaminiana kama mnavyotaka tuamini. ndoa ya tyson na monalisa iko wapi? ndoa ya hale beri iko wapi? mahusiano ya mastaa wengi kila siku tunasikia yako kikaangoni. ukweli wa nafsi wanawake wengi waigizaji huangukia mapenzini na wale wanaoigiza nao. kama utavumilia hilo hapo sawa, ila si kuamini kuwa mkeo hafanyi kufuru nje ya mahusiano yenu. asilimia 90 ya mabinti wenye majina bongo wana kashfa nyingi za ngono. ukimruhusu mke/mume kufanya scene kama hizo is at your own risk!
Ray aliigiza na binti mmoja nimemsahau, mwishowe alimgeuza hawala, Kanumba aliigiza na miss TZ pia yakawa yale yale nk, hii inaonesha kama hatomuoa kwa vile ni mke wa mtu, ni lazima atamlamba tu, na utegemee kulea watoto wasio wako.
 
Kuna movie iliyochezwa na Ray akiwa amevunjika miguu yote kwa ajali, halafu mkewe akawa anamleta mwanaume ndani akiwepo, wanafunga chumba na kufanya mambo...! Je, nina uhakika gani kuwa sio kweli? Kacheki hiyo movie halafu utoe commend. Kwanza nikimuoa msanii, nampiga stop mara moja. Kwaya tu sikubali, sembuse uigizaji, Thubutu...! Kama ni wivu sawa....
 
Uigizaji kama huu mara nyingi husababisha kuanza kwa mausiano ya mapenzi baina ya hao waigizaji.
Sio tu Tanzania hata huko 'duniani' wasanii wengi wameanzisha uhusiano wa kimapenzi baada ya kuigiza kama wapenzi.
Mfano, Brad Pit na Angelina Jolie walianzia kwenye filamu ya Mr & Mrs Smith.
Sio wacheza filamu tu bali hata wasanii wa muziki wa kike na wa kiume wanapofanya video moja ya kimapenzi.
 
Kwani kuna tatizo inabidi mjenge mazingira ya kuamiana ....hehehe inaonekana mwenzetu unaweza kupasua TV
Ni vyema tuwe wakweli, we dada chukulia kuwa aliyelaliwa (kwenye picha hii) ni mmeo, utaridhika tu???? Si utasema ``kama mambo yenyewe ni haya acha tu tufe masikini!!!``
 
Kwa mkao huo kwenye picha hata kama kama unamumini mkeo asilimia zote hapo ilipofikia .................mmmmh hakuna kuigiza kabisa mie nasema bora akae home maana hiyo picha hapo lazima kupimana imani kuwepo wakimaliza movies wanaenda kudunguana tuuuu
 
Kwa wabongo wanadhani kuigiza namna hiyo ndiyo kuongeza uzuri wa filam, wasichojua ni kwamba unaweza kutengeneza picha nzuuri tu bila kutiatia aibu za namna hiyo....ujinga tu
 
hapo mamsapu atanisamehe! Uigizaji gani kama huo? Thubutu!
 
Kwani kuna tatizo inabidi mjenge mazingira ya kuamiana ....hehehe inaonekana mwenzetu unaweza kupasua TV

Assume Kanumba angekuwa mumeo..........usingejisikia wivu kwa mumeo?

Wakati mwingine tunakuwa emotionless kwenye matatizo ya wenzetu na kujifanya washauri wema huku tunaignore baadhi ya vitu basic, likikutokea wewe tatizo hilo hilo unadondoka kwenye depression ya kufa mtu!!
 
Kwani kuna tatizo inabidi mjenge mazingira ya kuamiana ....hehehe inaonekana mwenzetu unaweza kupasua TV

arghhhhh..kwani nini cha ajabu hapo??....acha wivu kwa mkeo kaka...kazi hiyo inaleta kipato cha familia....

NI MAONI TU WADAU ILA YAMEJAA MTAZAMO WA KUWAWEZESHA WANAWAKE WASIENDELEE KUWA JINSIA TEGEMEZI

hapo mamsapu atanisamehe! Uigizaji gani kama huo? Thubutu!
Pape naamini amejibu yote, First Lady na wenzako mnaweza kubadili mtazamo wenu. au ni ngangali.
 
hao wanaeneza uchafu tu,wanaigiza nini kwanza hawa? kila siku wako tu palepale na hawana lolote wanacontribute kwenye society kutokana na maigizo yao, zaidi sana ni kuiga mambo ya ulaya na kuchafua jamii tu.
 
Back
Top Bottom