Hali kama hii itaweza kufika bongo miaka ijayo ya bunge ninatabiri mimi.......

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
VIDEO - Mwanasiasa Atoa Bunduki Baada ya Kuzidiwa na Maswali
6508930.jpg

Mbunge wa Jordan alitoa bastola baada ya kuzidiwa na maswali

Baada ya kuzidiwa na maswali kwenye kipindi cha televisheni LIVE, mbunge wa bunge la Jordan kwanza alivua kiatu na kumtandika mpinzani wake kabla ya kutoa bastola yake na kutishia kumpiga risasi jamaa aliyekuwa akimbana sana kwa maswali.
Mbunge wa bunge la nchini Jordan alishindwa kuvumilia maswali ya mpinzani wake na kuamua kutoa bunduki kwenye kipindi cha televisheni kilichokuwa kikirushwa LIVE na televisheni ya Jordan.

Mbunge huyo aliyetajwa kwa jina la Mohammed Shawabka alikuwa kwenye kipindi cha mjadala wa mambo ya kisiasa kilichokuwa kikirushwa LIVE na televisheni ya Jordan.

Mjadala huo ulipamba moto pale mbunge huyo alipotupiwa maneno na mwanaharakati wa masuala ya kisiasa, Mansour Sayf al-Din Murad akituhumiwa kuchakachua uchumi wa Jordan huku mbunge huyo pia akimtuhumu mwanaharakati huyo kuwa ni jasusi wa Israel.

Mbunge huyo baada ya kuzidiwa na maswali ya mwanaharakati huyo alianza kumrushia maneno makali.

Haikuchukua muda mrefu, mbunge huyo aliinama chini na kuvua kiatu chake na kumrushia Mansour ambaye alifanikiwa kukikwepa kwa kubonyea chini.

Mbunge huyo aliona haitoshi ndipo alipoamua kutoa bastola yake ndogo na kutishia kumpiga risasi mwanaharakati huyo.

Ugomvi huo ulizidi kuwa mkubwa lakini pamoja na harakati za muandaaji wa kipindi hicho kujaribu kusuluhisha, ugomvi huo uliendelea na kupelekea kipindi hicho kukatwa.

Mwisho wa ugomvi mbunge huyo hakuitumia bastola yake.






<tbody>
</tbody>


VIDEO - Mwanasiasa Atoa Bunduki Baada ya Kuzidiwa na Maswali

Wallah Nabaa Ushungu badala ya kutoa Jamvia kaamuwa isiwe tabu katoa Pistol kasheshe kweli Mambo ya bungeni.......
 
VIDEO - Mwanasiasa Atoa Bunduki Baada ya Kuzidiwa na Maswali
6508930.jpg
Mbunge wa Jordan alitoa bastola baada ya kuzidiwa na maswali
Baada ya kuzidiwa na maswali kwenye kipindi cha televisheni LIVE, mbunge wa bunge la Jordan kwanza alivua kiatu na kumtandika mpinzani wake kabla ya kutoa bastola yake na kutishia kumpiga risasi jamaa aliyekuwa akimbana sana kwa maswali.
Mbunge wa bunge la nchini Jordan alishindwa kuvumilia maswali ya mpinzani wake na kuamua kutoa bunduki kwenye kipindi cha televisheni kilichokuwa kikirushwa LIVE na televisheni ya Jordan.Mbunge huyo aliyetajwa kwa jina la Mohammed Shawabka alikuwa kwenye kipindi cha mjadala wa mambo ya kisiasa kilichokuwa kikirushwa LIVE na televisheni ya Jordan.Mjadala huo ulipamba moto pale mbunge huyo alipotupiwa maneno na mwanaharakati wa masuala ya kisiasa, Mansour Sayf al-Din Murad akituhumiwa kuchakachua uchumi wa Jordan huku mbunge huyo pia akimtuhumu mwanaharakati huyo kuwa ni jasusi wa Israel.Mbunge huyo baada ya kuzidiwa na maswali ya mwanaharakati huyo alianza kumrushia maneno makali.Haikuchukua muda mrefu, mbunge huyo aliinama chini na kuvua kiatu chake na kumrushia Mansour ambaye alifanikiwa kukikwepa kwa kubonyea chini.Mbunge huyo aliona haitoshi ndipo alipoamua kutoa bastola yake ndogo na kutishia kumpiga risasi mwanaharakati huyo.Ugomvi huo ulizidi kuwa mkubwa lakini pamoja na harakati za muandaaji wa kipindi hicho kujaribu kusuluhisha, ugomvi huo uliendelea na kupelekea kipindi hicho kukatwa. Mwisho wa ugomvi mbunge huyo hakuitumia bastola yake.
<tbody> </tbody>
VIDEO - Mwanasiasa Atoa Bunduki Baada ya Kuzidiwa na MaswaliWallah Nabaa Ushungu badala ya kutoa Jamvia kaamuwa isiwe tabu katoa Pistol kasheshe kweli Mambo ya bungeni.......
Tanzania yameshafika hayo, Pale Igunga kila siku tulikua tunasikia risasi zinarindima kutoka kwa wana kampeni wa CCM , na mwisho wa Yote Rage akapanda nayo na akaiweka adharani, sasa unafiri wangemuuzi ingekuwaje? umesahau ya Bro Dito
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom