Kiraka
JF-Expert Member
- Feb 1, 2010
- 3,834
- 3,076
Nimefika Mapambano A Sinza, kuna tatizo la upungufu wa wasimamizi waelekezaji wa wapiga kura. Walibandika huko siku za nyuma list ya wapiga kura, leo wametoa pale yalipokuwa na kuyahamishia kwenye madarasa mbali mbali, lakini hakuna mtu wa kuelekeza wapiga kura hili jambo, hivyo watu wanafika na kusumbuka kutafuta majina yao, na wengine kukata tamaa, nimefanikiwa kujaribu kuelekeza watu kama kumi hivi, lakini sioni msimamizi wa kituo, askari na hao wasimamizi wa tume hawana usaidizi wowote wamekaa, kwa sasa watu ni wachache sijui itakuwaje pale kutakapokuwa na watu wengi.
Kama kuna mtu anamjua mtu wa tume anayeweza kusaidia hili ataarifiwe.
Kama kuna mtu anamjua mtu wa tume anayeweza kusaidia hili ataarifiwe.