Elections 2010 Hali halisi vituoni siku ya kupiga kura

Wagombea wa chadema ngazi ya jimbo na kata hawakuwa serious na mawakala, tumeshalizwa tayari. Chadema makao makuu walijipanga kuratibu na kushughulikia haya matatizo?
 
Mungu wetu ndiye msimamizi wa kura leo, yaani mimi nimepigia hapa TSJ- Makumbusho, mawakala naona kama ni under 18 jamani, ila tusali tuuuuuu
 
...nimechanganyikiwa!! nimepiga kura ila naondoka kituoni kwa hofu kubwa, mawakala nimemwona mmoja wa ccm, mwingine mchafu mchafu hv sijui ni wa chama gani... hv kweli jamani kura yangu itapona?
 
Tayari, nimetoka!!! asante watu wa arusha, vipi moshi mbeya mbona kimya? hata nyie shinyanga jamani


Moshi kupo quiet, si unajua ndugu zetu huwa wanaacha mji na kupanda mlimani? Ila mie nimepiga kura yangu ya mafiga matatu ya CHADEMA na sasa nasikilizia tu.
 
Nami nimepiga tayari nikiwa Morogoro. Mambo ni shwari kabisa. Tuendelee kumwomba Mungu akamilishe ukombozi wa watoto wake.
 
Nimetoka kumfukuza kazi rasmi ya urais jakaya mrisho kikwete kupitia kwenye kura yangu.
Nilimuangaria kwanza usoni jk halafu nikamkemea asinichekee kabla ya kwenda kumtilia alama ya vyema
dr. Wilbroad slaa kumkaribisha rasmi ikulu.
 
Nimeshapiga kura. Naangalia tv watu wanavyopiga kura. Watu walio kwenye foleni ya kupiga kura wanaonekana wana uchungu na hasira. Sijaelewa tatizo. Au ndio wanaenda kumsulubu JK!!! Kweli kazi ipo. Kumbe watu ukiwaangalia usoni tu utajua wanapigia chama gani. Kwa hali hii JK ajiandae kukabidhi tu, na akiangalia tv ndio presha itapanda. Maana watu wana hasira utadhani wanaenda ulingoni

Kama uchaguzi utakuwa wa haki, thithiem hawana lao. Watanzania tumewachoka katika kila kona ya nchi.
 
By this time tomorrow, habari zitakuwa zingine kabisa! Ni VILIO everywhere! Kwi kwi kwi!!!!!! :smile-big:

Kwa mwanamapinduzi wa kweli hakuna kulia, safari ya mapambano ndo kwanza inaanza upya. Mna kazi kubwa sana ya kuongoza nchi ambayo three quarters hawaridhiki na uongozi wenu.
 
Kwa wale mliokwisha kupiga kura endeleeni kuhamasisha wale ambao wanaonekana kukata ya kupiga kura wakapige kura.
 
Kwenye kituo changu leo ilikuwa hivi..

IMG00407-20101031-0912.jpg IMG00406-20101031-0912.jpg IMG00404-20101031-0758.jpg IMG00405-20101031-0806.jpg

Vijana wengi na hata watu wa makamo wamejitokeza kwa wingi na wanataka mabadiliko na maendeleo

Tembelea Uchaguzi Tanzania kupata taarifa mbalimbali LIVE za uchaguzi 2010.
 
Wagombea wa chadema ngazi ya jimbo na kata hawakuwa serious na mawakala, tumeshalizwa tayari. Chadema makao makuu walijipanga kuratibu na kushughulikia haya matatizo?

Jamani kwa kuwaangalia watu usoni tu mnaona hawafai, labda watu wa ndani ya CHADEMA watujuze.

Kwangu mie wakati napiga kura niLIona akina mama na wazee wazee wengi, i was a bit scared cos kidogo akina mama wapo attached sana na SisiM (Sorry dada zangu). Hata hivyo ni rural kidogo so its more likely that young people have moved to town.

I was encouraged by one old man as i was leaving the voting premises who told me that he is so disappointed that students are not going to vote but he still believes that Dr. Slaa will win.

I went, wow, how did you know that i am anti-CCM?
 
Ni asubuhi tu nimefika kituoni kupiga kura. Wengi waliosimama mstarini ni vijana wenye nyuso za matumaini na tabasamu. Sijawahi kuona mwamko wa namna hii tangu nilipopiga kura yangu ya kwanza mwaka 1975.

Naamini kabisa watanzania wanahitaji mabadiliko kwa nilichokiona hapa Mwanza, nitawajulisha kinachoendelea ila kwa masikio yangu CHADEMA juu

Shukrani kwa taarifa
 
Jamani nimfanyeje m2 huyu?(jk)?
Nimsulibishe nisimsulibishe?
Bila shaka jibu ni cmpo,
ASULIBISHWE . . . . !
HADI MDA HUU,KWA MTAZAMO DR.SLAA ANA KURA KAMA 10Milion,2jiandae kuenda kumshuhudia akila kiapo. . . . !
Pipo o o o o o o z. . . . . . ? ? ?
 
Jamani mliokwisha piga kura hebu tuelezeni iwapo kuna ukweli wa habari kwamba tiki ya kwa Dr (phD) inaweza kuhamia kwa 'Dr' (wa kuchota). Hii hasa ni katika maeneo ambayo Dr(PhD) ana ufuasi mkubwa kama vile Mbeya, Mwanza, Bklb, Musoma, Arusha, kili, Manyara, Iringa, Rukwa.
 
Wakuu mpaka sasa katika zunguka zunguka ya hapa na pale..nikiwa katika manispaa ya iringa nimeona maeneo mengi yakiwa shwaari kabisa huku watu wengi wakiwa wamejitokeza kwa wingi vituoni kupiga kura..maeneo ya mji yametulia..huku wengine wakiwa wameanzia katika nyumba za ibada (makanisani) lakini bado kuna misururu mirefu ya wapiga kura katika maeneo mbalimbali waliojitokeza tangu alfajiri na mapema!!

Matatizo katika vituo ni yaleyale m-yajuayo..mara majina hayaonekani..mara nenda kule ..nk lakini walau mji umetulia!! Ntaendelea kuwahabarisha kwa lolote litakalotokea!!

2ufu1dv.jpg

rc6a86.jpg


9acutu.jpg

picha kwa hisani ya: Mzee wa matukio daima!
 
Mimi nimetoka kupiga kura pale NIT MABIBO, hali hairidhishi, foleni inakwenda taratibu sana, watu ni wengi, hasa kundi la vijana ambao walikua ni wenye furaha sana. Mpaka saa mbili bado zoezi la kupiga kura lilikua halijaanza katika kituo cha kupigia kura "G"

Pia watu walikua wanahangaika kujua majina yao yalipo, utakuta mtu kapanga foleni akifika karibia na mlangoni anaambiwa jina lako halipo hapa kapange mstari ule pale, hiyo ilikua ni kero kubwa sana kwa watu, kwa maana ilibidi waanze tena upya foleni zao.
 
..Wajumbe kuna taarifa toka kanda ya ziwa zinazosema mwamko ni wa kufa mtu..Masha anavuliwa ubunge na uwaziri rasmi leo..bila aibu ameenda kupiga kura kituo cha nyegezi bila kujua kituo kizima kura yake ndo ya kwanza na ya mwisho kujipigia..
Lakini wananchi wanamsanifu,maana wanajua mbwa akikaribia kufa huwa hajui harufu...KWAHERI MASHA!! Buriani..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom