Elections 2010 Hali halisi vituoni siku ya kupiga kura

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
Nipo kwenye kituo cha kupigia kura hapa shule ya Nkuhungu, waliojitokeza ni wengi lakini vijana wametia fora! Taratibu zinakwenda vizuri na majina yapo yanaonekana vizuri. Wengine mtueleze kinachoendelea kwenye vituo vyenu.
 
Tangia alfajiri nimekuwa nikifanya "shunting" kutoka Bunju B hadi Tegeta kwa ndevu ::: Watu wamejitokeza na inaonekana utaratibu so far ni mzuri
 
Kata ya Sinza B kuna uzembe wa wasimamizi wa uchaguzi ambao leo nimewaona ni watoto wa makada wa CCM wametuchelewesha kdogo.
 
Nipo hapa mapambano Sinza!

Hali ni shwari watu ni wengi na vijana wapo its amazing pia middle class wametia fora. Pia watu waliofika na magari yamejaa nje ya wapiga kura hii inatia moyo!

Mungu ameibariki Tanzania (viva Jubilee!!)
 
Nimepata habari sasa hivi kutoka Tarime kwamba kunaweza kutokea vurugu pengine kuzidi ya zile za uchaguzi mdogo mwaka juzi, kwani CCM wanataka kupenyeza makada wao katika usimamizi wa uchaguzi. Lakini jamaa kanihakikishia kwamba vijana wako macho na niwatangazia Watz kwamba zikitokea vurugu nchi hii basi ni CCM ambao huwa hawataki kushindwa!

INATIA MOYO SANA HABARI HII
 
nipo kawe changanyikeni. Watu wamejitokeza kwa wingi, wa rika na jinsia zote. utaratibu ni mzuri. Kuna jamaa amefiwa na nduguye lakini kaja kupiga kura kwanza ndo waanze safari. Mwamko wa vijana ni mkubwa sana
 
Nimemaliza kupiga kura yangu hapa Ilkiurei nje kidogo ya mji wa Arusha, watu ni wengi sana, kuna utata wa baadhi ya majina ya watu kutoonekana lakini waangalizi wako makini sana kuwaelekeza wapiga kura namna wanavyoweza kutambua vituo vyao kwani wengine majina yao yamehamishiwa vituo vingine tofauti na walipojiandikishia. Inatia moyo sana jinsi upigaji kura unavyosimamiwa hapa.
Nimejaribu kudodosa kidogo kujua msomamo wa watanzania, kwa kweli CCM mnakazi kwani kila niliemuuliza nini hasa kilimsukuma kuwahi kiasi hicho kuja kupiga kura, jibu lilikuja tofauti na nilivyotegemea. Mzee mmoja kaniambia amechoshwa na uongozi usio na maslahi kwa wananchi na sasa kawahi ili aitumie haki yake vizuri kumchagua Dr. Slaa kwa mabadiliko ya kweli, anasema "pamoja na uzee wangu naamini Dr. Slaa ataniwezesha kufanikisha ujenzi wa kibanda changu" inatia moyo sana!
 
wanachosisitiza niliowahoji hapa ni kua kura yao ni muhimu sana uchaguzi huu, wengine wanasema hawana mzaha na uongozi. Nimeshuhudia vijana walosema hawatapiga kura wakiwa vituoni.
 
niko hapa kituoni,ubungo kisiwani.Mambo bado jamaa wasimamizi wako slooo.Ila watu ni wengi na mambo ni shwari.
 
Ni asubuhi tu nimefika kituoni kupiga kura. Wengi waliosimama mstarini ni vijana wenye nyuso za matumaini na tabasamu. Sijawahi kuona mwamko wa namna hii tangu nilipopiga kura yangu ya kwanza mwaka 1975.

Naamini kabisa watanzania wanahitaji mabadiliko kwa nilichokiona hapa Mwanza, nitawajulisha kinachoendelea ila kwa masikio yangu CHADEMA juu
 
ahsante kwa taarifa...niko mkoa wa pwani, kisarawe. vijana pia wamenishangaza, japo eneo sio la wakazi wengi, ila inatia moyo sana..
 
Nimesafiri kati ya Moro na Dar asubuhi hii. Nimeona watu wamepanga misururu vituo mbalimbali. Maeneo ya Mlandizi na Kibaha FFU ndani ya magari yao wanarandaranda barabarani. Kwa haraka inaonyesha wamama ni wengi zaidi vituoni. Baadhi ya makanisa yenye shamrashamra kila jumapili yamepigwa kufuli. Uchaguzi mwema
 
Nimetoka kupiga kura maeneo ya mbezi beach na kuna vituo 6. Kituoni nimeona kasoro hizi
  • Vituo vimefunguliwa saa 12 asubuhi lakini kupiga kura tumeanza saa 1 asubuhi tumeambiwa mtu wa mwisho kuruhusiwa kupiga kura ni atakae fika saa 10 jioni, na kila kituo kitahudumia watu 500, hesabu za haraka kila saa moja watu 55. Lakini kwa saa moja kituo kimoja kimehidumia watu 9 tu. Kuna uwezekano watu wengi wasiweze kupiga kura
  • Kuna watu watano ambao nimeshuhudia majina yao hayapo kwenye orodha ya wapiga kura wakati daftari lina majina na picha zao.
  • Mtu mmoja kakuta majina yake yamekosewa ingawa namba ya mpiga kura kwenye kitambulisho ni sawa daftari
  • Vituo vina mawakala wachache watatu hadi wanne, baadhi ya vyama havina mawakala
  • Kati ya mawakala hao waliopo wa vyama wengine wamekuja baada ya upigaji kura kuanza
  • Mawakala wa nec wako slow na hii ni asubuhi, ikifika mchana jua kali itakuwaje?
Tungepata na vituo vingine hali ilivyo
 
Namshuru mungu nimemaliza kupiga kura, cjawahi pata msukumo wakupiga kura kiasi hiki, safari hii watu wamehamasika sana kwa kweli, naimekua tofauti na miaka mingine watu hawafichi mtu yuko huru kumtaja anae mpigia kura, hapa kituoni kwetu ukiona line imejaa vijana unajua wanampigia nani. Kweli inatia moyo sana.
 
wadauuuu,mi nawakubari kwani napata habari kama nipo home tz,mapinduzi daima,endeleeni kutupa habari
 
tuna shukuru mkuu,kweli mawasiliano ni muhimu sana napata habari kama nipo tz vile hongereni,
mapinduzi daima
 
Back
Top Bottom