Hali botswana si shwari... Vurugu zasababisha shule kufungwa kwa muda usiojulikana

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Lile vuguvugu la mageuzi lililoanzia Kaskazini mwa Afrika na ukanda wa nchi za Arabuni huenda limevuka Afrika ya Magharibi, Kati na Mashariki hadi kufika Kusini.

Baada ya vuguvugu kuanzishwa nchini Lesotho, sasa Botswana i halijojo kufuatia mgomo wa wafanyakazi uliosambaa hadi kusababisha wanafunzi kugoma, kuharibu majengo na hatimaye kulazimu shule kufungwa. Unaweza kuisoma taarifa hiyo ya kufungwa shule kufuatia vurugu kwa kubofya hapa.

Lakini mmoja wa rafiki aliyepo huko anaandika hivi:

Ugomvi ni "Mjeshi Mkuu" wa Serikali na Wafanyikazi.

Wanataka nyongeza ya asilimia 16, sababu hawajaongezwa tangu 2004, na maisha yamepanda sana.

"Mjeshi" akakataa, hakuna hela, mwishowe akasema atatoa asilimia 5.

Wafanyakazi wakaamua kugoma kwa wiki 2, Serikali ikapeleka "ishu" mahakamani wale wote walio katika huduma muhimu wasigome kulingana na mkataba. Mahakama ikapitisha, walio hospitali, maji, umeme nk., wakaambiwa warudi kwa amri ya mahakama.

Wakagoma.

Zilipoisha wiki 2 wakaendeleza mgomo... "indefinitely".

"Mjeshi" anapiga propaganda mgomo hauathiri chochote na hata wakigoma kwa miaka 5 haongezi kitu ng'o!

huduma zikazorota, Alhamis ikachukua sura mpya, shule moja ya high level ikalianzisha, "kwanini hatufundishwi?", Serikali inasema walimu wapo... wakati hawapo...

Wanafunzi "wakawapa kibano" walimu waliokuwa wanafundisha... "kwanini hawajajiunga na mgomo.

Waziri wa elimu akaenda.

Wakamkimbiza kwa mawe

Kasheshe ikaanzia hapo.

Ijumaa shule nyingine 2 zikaendeleza.

Leo, nchi nzima babake! Wanafunzi Sekondari hadi Primary wote wameingia kitaani... vurugu noma. Wana mawe, visu fimbo na chepeo.... Vunja ofisi za Serikali na gari za Serikali hata binafsi. Pora maduka.

Watu wakafunga kazi saa 3 asbhi kuogopa vurugu. Ikaletwa "FFU". Wakapiga watoto, vita ikaanza, bahati mbaya wakakamata askari mmoja... wakapiga wakaua, wakakamata mwalimu aliyekataa kugoma, wakapiga wakaua. Mwanafunzi mmoja pia kafa.
Wanapiga walimu na wanafunzi wanaoenda madarasani na yoyote anayetetea.

"Mjeshi akatuma helikopta kutawanya. Wakawapiga "tear gas", noma, wakachochea moto, ni noma.
wakatuma wajeshi sasa convoy kubwa, watoto wamefunga barabara zote, kali zaidi wengine ni std 1 wapo humo!!!

Waziiri wa elimu katangaza kufunga shule zote... indefinitely.

"Mjeshi" katangaza kufukuza kazi wote walio mgomoni as soon as possible.

Kesho sijui itakuwaje!!

source: Hali Botswana si shwari... vurugu zasababisha shule kufungwa kwa muda usiojulikana - Wavuti
 
... strange enough Western Media ziko kimyaaaaa! pure manifestation of Western Double Standards and Imperialistic Agenda.
 
... strange enough Western Media ziko kimyaaaaa! pure manifestation of Western Double Standards and Imperialistic Agenda.

kwani kila kitu lazima kiripitiwe na western media? wasiporipoti ni double standards? so tunakaa chini tunasubiri west waripoti. halafu kwingine tunalalamika western imperialism! strange us people. kweli we must emancipate ourselves from within manake now tunachekesha
 
Kweli jana asubuhi baada ya kumpeleka mtoto shule,hazikupita hata dakika 05 nikapigiwa simu nikamchukue mtoto kwani wanafunga shule hali ya kiusalama sio nzuri.Pia mtoto mwingine alirudishwa saa 6 wakati anatakiwa kurudi nyumbani saa 11.30 jioni.Hali sio nzuri kabisa,mji mchafu.Takataka zimezagaa barabarani,maana wazoaji taka wamegoma,sasa watu wanachofanya ni kwenda kuzitelekeza barabarani na unakuta mbwa wanachana ile mifuko na uchafu unatawanyika hovyohovyo,ni kama mwezi na kitu takataka hazijazolewa.
 
Kweli jana asubuhi baada ya kumpeleka mtoto shule,hazikupita hata dakika 05 nikapigiwa simu nikamchukue mtoto kwani wanafunga shule hali ya kiusalama sio nzuri.Pia mtoto mwingine alirudishwa saa 6 wakati anatakiwa kurudi nyumbani saa 11.30 jioni.Hali sio nzuri kabisa,mji mchafu.Takataka zimezagaa barabarani,maana wazoaji taka wamegoma,sasa watu wanachofanya ni kwenda kuzitelekeza barabarani na unakuta mbwa wanachana ile mifuko na uchafu unatawanyika hovyohovyo,ni kama mwezi na kitu takataka hazijazolewa.

Poleni broda!
I cant figure out mahala kama Botswana vurugu zinaanzia wapi, wakati at least kila Mtswana ameonja Maisha Bora.

Waambie wale jamaa zetu wa MAKHIRIKHIRI wakae mbali na vurugu hizo!
Wabongo wanampenda sana 'Shumba Ratshega'!
 
Back
Top Bottom