Hali bado tete jijini Mbeya

Hili nililiona, jana wenzao wameuwawa kwa risasi unategemea leo wangelala tu?
Hakuna kiongozi hata mmoja aleamua kutoa taarifa na kuuomba umma wa Mbeya japo msamaha, lazima warudi njiani tena

Mabomu ya machozi na risasi za moto havijawahi kuwa suluhisho la matatizo ya wananchi na kwahiyo hata kama polisi watayavurumisha wiki nzima haitakuwa suluhu.

Muhimu ni uongozi wa mkoa kuyatazama matatizo ya wamachinga kwa busara na kama wajibu wao wa lazima, wakae nao mezani, wawasikilize madai yao na hatimaye watafikia suluhisho. Hii hali ikiendelea hivi ninapata wasiwasi na mustakabali wa askari na familia za askari polisi wanaoishi uraiani! Katika hili waziri nahodha anatakiwa kuwa mbeya hadi muda huu ninapoandika post hii.
 
Yatakuwa yameletwa usiku toka Iringa, Songea, Rukwa n.k.

Yataisha tena na askari watachoka, watashindwa hasa pale familiua zao zinazoishi uswahilini na raia zitakapoanza kulipizwa kisasi. Hapo hali itazidi kuwa mbaya.

JK na Serikali yako muyatizame haya, Diplomasia ni kitu muhimu sana kuliko mtutu wa bunduki.
 
Viongozo wa Magamba watumie busara, hasira ya umma haiwezi kutulizwa na mabomu, risasi. Na wasidhubutu kufanya kosa waue watu.
 
mbeya walisema kitawaka mpaka kieleweke! Sikujua kama ndugu zangu hao wanamsimamo ya kiivi kwa kweli!
 
amani ya nchi hailindwi kwa mabomu! nahisi hili litakuwa somo zuri saana kwa watawala wetu.
 
nasikia jana walifanya hivyo hivyo kuwaomba wananchi wayamalize hayo masuala kwa majadiliano lakini wananchi walipojaribu kukusanyika walizingirwa wakapigwa na wengine kukamatwa hivyo leo sidhani if people will buy that crap of table reconciliation...
 
itabidi serikali imwombe kiongozi wao/Mbunge sugu akatulize hali lasivyo mafisadi watatumia risasi mpaka zitaisha na huu ukata sijui watazinunua wapi.

Peoples power inafanya kazi.
 
jamani huku sasa ni vita wakati najiandaa kwenda ofisini mana nipo kikazi huku ttcl kutoka hotelini mabomu yanapigwa sio mchezo watu wamejifungia kazi imeanza upya huu mgogoro utaweka historia ktk hii nchi naona magari ya matangazo yanapita kutangazia watu kwamba mapambano yasitishwe watu wakae mezani hali ni mbaya hivi hapa nafanya maarifa nitafte gari linalokuja dar nirud hata kazi cwez fanya vzur

wewe subiri hukohuko
uwe na experience,cku si nyng uyazoea tu
 
Askari kumbukein hamuishi vituo vya polisi ila mnaishi uswahili na raia, mna familia, wake/waume, watoto, wazazi na ndugu wengine. Je nao hao wakipigwa japo rungu (achilia mbali risasi), wakarushiwa udongo (achilia mbali mabomu ya machozi) mtajisikiaje?? Mtafurahi???
Nijuavyo mimi ni "hata muuaji akifiwa hulia machozi ya kweli".
Tafuteni suluhu inayowafaa nyote
 
itabidi serikali imwombe kiongozi wao/Mbunge sugu akatulize hali lasivyo mafisadi watatumia risasi mpaka zitaisha na huu ukata sijui watazinunua wapi.

Peoples power inafanya kazi.

Si wanang'ang'ania hiyo sheria ya kununua vichakavu ipitishwe? Watanunuliwa mabomu na risasi used.
 
Majimbo yanayaoongozwa na chadema ni vurugu tu, uzalishaji umesimama! Halafu tunalalamika tanzania masikin!
 
jamani huku sasa ni vita wakati najiandaa kwenda ofisini mana nipo kikazi huku ttcl kutoka hotelini mabomu yanapigwa sio mchezo watu wamejifungia kazi imeanza upya huu mgogoro utaweka historia ktk hii nchi naona magari ya matangazo yanapita kutangazia watu kwamba mapambano yasitishwe watu wakae mezani hali ni mbaya hivi hapa nafanya maarifa nitafte gari linalokuja dar nirud hata kazi cwez fanya vzur

Wenzio wako kazini zaidi kuliko wewe. nani akubali kufa njaa wakati mafisadi wanaendelea kujimegea keki na vizazi vyao
 
Yataisha tena na askari watachoka, watashindwa hasa pale familiua zao zinazoishi uswahilini na raia zitakapoanza kulipizwa kisasi. Hapo hali itazidi kuwa mbaya.

JK na Serikali yako muyatizame haya, Diplomasia ni kitu muhimu sana kuliko mtutu wa bunduki.

Tena naomba Mungu tusifike huko kwenye kulipizana kisasi. Serikali fanyeni hima mmalize mgogoro huo.
 
Hawawajui watu wa mbeya hao, na huyo Kandoro wao aliyevuruga Mwanza sasa amehamia Mbeya nako kutamshinda, labda wampeleke tabora lakini sio miko ya watu wenye akili zao timamu
 
Back
Top Bottom