Hakuna Ugumu wa kurudi Misri...

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Yanayotokea katika nchi yetu kwa sasa yanatutaka tufikiri kwa bidii. Kama nchi kuna safari tumeifunga. Na tulivyo Waafrika, tu mahodari wa kufunga safari, lakini si mahodari wa kupanga safari. Kufunga na kupanga safari ni vitu viwili tofauti.

Ndugu zangu,

Ni vigumu leo kwa Wana wa Israel kuamua kurudi tena Misri, hata kama, pamoja na chawa na kunguni walioaacha Misri, bado, kuna wanaokumbuka samaki na masufuria ya pilau waliyoayaacha Misri. Lakini, kijamii, na kwa kuingalia jamii yetu hii ilikotoka, ilipo sasa na inakoelekea, na tuone sasa, kuwa hakuna ugumu wa kurudi tena Misri. Na hapa nitazungumzia umuhimu wa sisi WaTanzania kujitambua.

Nahofia, kuwa moja ya kiini ya haya yanayotukuta sasa ni dhambi ya Ubaguzi iliyoanza kututafuna pole pole. Taratibu tunapoteza uwezo wetu wa kujitambua. Ni ukweli sasa, kuwa Watanzania hatujitambui, na kibaya zaidi, baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa na kidini wanapoonyesha wazi wazi kuwa hawajitambui.

Maana, tumeanza sasa kuzungumza lugha za ' Wao Wakristo' na ' Sisi Waislamu'. Tunasahau, kuwa sisi ni ndugu wa damu. Kuwa SISI ni Watanzania Kwanza. Na lililo la kwanza kwetu ni ' Nchi Yetu' na maslahi yake.

Hii ni Nchi Yetu Sote. Kila Mtanzania kwa nafasi yake ana lazima ya kupigania Usalama wa Taifa letu. Usalama wa Nchi Yetu tuliyozaliwa. Hatuwezi kuilinda na kuijenga Nchi Yetu kwenye mazingira ya kubaguana. Kwenye mazingira ya kugawanyika kwa misingi ya udini, ukabila na rangi. Na hapa nitamrejea tena Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na dhana ya Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa.

Ni Mwalimu Nyerere aliyeuanzisha na kuusimamia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa, hata hivyo, tunaona sasa unavyoporomoka na kuliacha taifa letu mashakani. Ndio, Mwalimu alijenga misingi imara ya Ujenzi wa Umoja Wa Kitaifa ( Nation Building).

Kuijenga jamii ya Watanzania yenye kuamini kwenye ukweli kuwa sisi sote ni ndugu. Kwamba Nchi yetu haina dini. Yenye kupiga vita ubaguzi wa aina zote, iwe wa rangi, kabila au dini. Ilimchukua Mwalimu na taifa letu miaka mingi sana kuijenga misingi hiyo iliyowawezesha pia Watanzania kuwa na mioyo ya uzalendo kwa Taifa lao.

Tunaona sasa, kazi hiyo iliyochukua miaka mingi, kutokana na ubinafsi na uroho wa madaraka ya baadhi ya wanasiasa wetu, wanapelekea kubomoka kwa misingi hiyo na kuliacha taifa letu kwenye hatari ya kuangamia.

Ndio, msingi wake ni ubaguzi wa kisiasa unaotokana na ubinafsi na tamaa ya mali kwa baadhi ya tuliowapa dhamana za kufanya maamuzi makubwa kwa niaba yetu. Ni hali ya baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi kuishiwa chembe chembe za uzalendo; mapenzi kwa nchi yao.Ni watu wenye kulinda maslahi yao na ya wanaowazunguka. Wako tayari hata kutumia mbinu za Umafia kutimiza malengo yao. Kuna Watanzania wengi sasa wanaopoteza mioyo ya uzalendo kwa nchi yao.

Kuna hata wenye kufikia kutamka; 'Nchi hii ina wenyewe'. Kuna anayetamka hilo kwa lengo la kumtishia mwenzake au kulazimisha kitu fulani kifanyike. Lakini, kuna wenye kutamka hivyo kuashiria kukata tamaa. Kuwa hata wafanye nini, hakuna anayewasikiliza ama kuwajali. Hizi si dalili njema kwa taifa. Kuna wanaoiba mali ya umma mchana wa jua kali. Hakuna anayewagusa.

Ukiuliza utajibiwa; "Ah! Nchi ina wenyewe!". Kwamba kuna baadhi yetu hawajisikii kuguswa na nchi hii, hawajisikii kuwa na nguvu ya kupiga vita maovu yanayotusumbua. Baadhi yetu wameanza kupungukiwa na mapenzi na nchi yao.

Juni 16, 2004 nilipata kuandika hili kwenye gazeti la Majira; kuwa Tanzania ina vyote, kasoro Watanzania. Niliandika; kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana. Ni nchi ya kujivunia. Kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana kwa eneo. Ni nchi yenye rasilimali nyingi; ardhi yenye rutuba, mito, maziwa, milima, mabonde, bahari na vivutio vingi vya asili.

Hata hivyo, Tanzania ni moja ya nchi masikini sana duniani. Kwa nini? Ndio, kikubwa kinachokosekana Tanzania ni Watanzania. Tanzania tunayoijenga sasa ni mkusanyiko tu wa watu wa makundi mbali mbali wenye kwenda kwa staili ya 'kila mtu na lwake'. Idadi ya Watanzania wenye uzalendo na mapenzi kwa nchi yao inazidi kupungua. Ubinafsi umekithiri, na ubinafsi mbaya zaidi ni ule wenye kufanywa na viongozi.

Ndugu zangu, Hakuna ugumu wa kurudi Misri. Tuna lazima ya kupanga safari ya kurudi tena Misri. Inawezekana.

Na hilo ni Neno la Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa,
 
Ndugu yangu Mjengwa,

Umeandika vizuri. Swali kubwa ni kuwa "wangapi kati yetu watakuelewa?"
 
Mkishaanza kubagauana, KAMWE hamtabaki salama. RIP Nyerere
 
Nakubaliana kabisa na wewe udini ni chachu inayotumiwa na wana siasa wachache ili waweze kupata kutawala kwasababu ya kukosa sifa nyingi zinazohitajika kwa watu wanaotaka kuwa viongozi. Lakini historia itawatupa kwenye makapu na mambo yao ya hovyo hovyo....time will tell. Yoooote yatajulikana tu as we slowly rolling forward, ingawa inawezekana pia nchi yetu ikawa imeharibiwa kwa ubaguzi huu.
 
Kiongozi Dhaifu ni yule anayetumia Udini kama Catalyst ya kuingia madarakani. hili tumeliona 2010 mavuno yake ndio sasa tunayapata
 
big up mjengwa. hivyo wa tanzania hatuwezi kubuni namna yetu itakayotuwezesha tuishi kwa amani bila kumeza kila kitu kinacholetwa na wageni? nafasi ya dini katika kulifanya taifa hili liwe moja ni kubwa sana na ni makosa kwa viongozi wetu wa dini wakafikiria kuwa serikali inatosha. wao ndio wako karibu na watoto tokea wanapoujua ulimwengu huu. waangalie namna ya kupeana mawazo na kusaidiana katika masuala ya elimu na afya kwa uchache badala ya kuwa katika ushindani.
 
Mjegwa ; unachanganya madesa,
Uwezi kulinganisha Taifa km israel na Misri na Tanzania,

Kwanza wewe ndo unashiria udini, vita vyote , histori yote khs nchi hizo ni dini.

njoo na topic mpya isiyo na mifano ya dini , hakuna unalojenga ; ukisema misri - muslim; israel-chrstian
Irrelevant topic to current situation , this is secular state the Example must based on secular countries performance
 
JK ndo muasisi wa ubaguzi wa kidini hapa nchini...

Na nyerere jee hakua mdini kwa kuipinga oic na kuikumbatia vatican jee EL vp kila kukicha na biblia makanisani mpaka padri kudiriki kama lowasa hakua rais 2015 wamuue jee si maskofu waliosema kikwete chaguo la mungu
 
Zamani kidogo mara tu baada ya awamu ya pili kuanza wakati huo nikiwa jeshini,nilisikia waziri wa elimu akiruhusu wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo vya ualimu KUVAA HIJABU akisema ndivyo mwislamu anavyo takiwa kujisitiri. wenye kuona mbali wakapaaza sauti wakasema ni mwanzo wa KUBAGUANA shuleni.watu watasema yule mwislamu na yule siyo mwislamu. hakusikia la mtu aya mpya miongoni mwa watanzania ikafunguliwa.
mwalimu JK. NYERERE alitaka wanaotaka kuvaa kama dini zao zinavyo taka wakasome seminari iwe waislamu au wakristo au wasabato.ndege wa aina moja huruka pamoja, serikalini wanafunzi wote wavae sare.sare maana yake kufanana kwa kila kitu.hakusikia kapuya,hakusikia Mwinyi,UBAGUZI UKAANZA.Wapenda udini wakapongezana kwamba walau wamepiga hatua moja mbele.tena wakaanza kutaka kulazimisha swala tano mashuleni ikawa vita, vita kwelikweli waliotumwa wanaelekezwa wasirudi nyuma mpaka kieleweke!! wengine wakaambiwa ninyi mkienda kuswali wakristo wataendelea kusoma na ukimkuta mwalimu ameingia darasani usingie mpaka kipindi chake kiishe. wenye akili wakaona haina tija wakaacha.ambao hawakuchanganya na zao wakaendeleza madai mengine ikiwa ni pamoja na kujengewa misikiti shuleni!!! udini ukawa unashamiri.wakalazimisha waislamu watengewe mahali maalumu kwaajili ya ibada zao.AGENTS WA UDINI HAWAFAI,LAKINI WAPO SERIKALINI.
Kwa maoni yangu,watu waendelee kuwa na dini zao zozote wazitakazo lakini serikalini kusiwe na elementi yoyote inayo mtambulisha mtumishi wa umma au mwanafunzi kwa dini yake. wanaotaka kujipambanua kwa dini zao waende kufanyakazi kwenye madhehebu yao au dini zao vivyo hivyo kwa wanafunzi wote wanao soma shule za serikali sharti wafanane. Anae taka kuvaa msalaba aende shule za seminari,anae taka kuvaa hijabu na aende seminari za kiislamu.naona siku hizi kuna watu wanavaa baragashia na misalaba mikubwa kwenye ofisi za umma, ni mwanzo wa kubaguana kwa dini zetu na inawezekana na huduma kwa wateja zinatolewa kwa mtazamo huohuo. ni HATARI SANA KWA UMOJA WA TAIFA LETU.
 
Kweli nimeamini kuwa humu JF kuna watu wa kila aina.wengine ndio kwanza wapo std 5.angalia huyu ni kama amelishwa maneno hajui anaongea nini. watanzania wana dini,lakina NCHI haina dini.VATICAN NI NCHI kwahiyo inahaki ya kuwa na balozi TANZANIA.OIC purely ni shirika la kidini.Endelea kujifunza kutoka GREAT THINKERS iko siku utajua kuto kuchanganya mambo kama ulivyo fanya leo.
 
Mjegwa ; unachanganya madesa,
Uwezi kulinganisha Taifa km israel na Misri na Tanzania,

Kwanza wewe ndo unashiria udini, vita vyote , histori yote khs nchi hizo ni dini.

njoo na topic mpya isiyo na mifano ya dini , hakuna unalojenga ; ukisema misri - muslim; israel-chrstian
Irrelevant topic to current situation , this is secular state the Example must based on secular countries performance
Hujamwelewa mtoa mada ametumia lugha ya falsafa,msome vizuri.
 
Kweli nimeamini kuwa humu JF kuna watu wa kila aina.wengine ndio kwanza wapo std 5.angalia huyu ni kama amelishwa maneno hajui anaongea nini. watanzania wana dini,lakina NCHI haina dini.VATICAN NI NCHI kwahiyo inahaki ya kuwa na balozi TANZANIA.OIC purely ni shirika la kidini.Endelea kujifunza kutoka GREAT THINKERS iko siku utajua kuto kuchanganya mambo kama ulivyo fanya leo.
Dah kama ndo wewe great thinker basi dunia imeshaisha haya hiyo vatican unayosema ni nchi hebu ilocate ki geographier na unipe cabinet yake ya mawaziri pm bunge na kila kitu dah ww kweli kilaza tena mbumbumbu
 
Zamani kidogo mara tu baada ya awamu ya pili kuanza wakati huo nikiwa jeshini,nilisikia waziri wa elimu akiruhusu wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo vya ualimu KUVAA HIJABU akisema ndivyo mwislamu anavyo takiwa kujisitiri. wenye kuona mbali wakapaaza sauti wakasema ni mwanzo wa KUBAGUANA shuleni.watu watasema yule mwislamu na yule siyo mwislamu. hakusikia la mtu aya mpya miongoni mwa watanzania ikafunguliwa.
mwalimu JK. NYERERE alitaka wanaotaka kuvaa kama dini zao zinavyo taka wakasome seminari iwe waislamu au wakristo au wasabato.ndege wa aina moja huruka pamoja, serikalini wanafunzi wote wavae sare.sare maana yake kufanana kwa kila kitu.hakusikia kapuya,hakusikia Mwinyi,UBAGUZI UKAANZA.Wapenda udini wakapongezana kwamba walau wamepiga hatua moja mbele.tena wakaanza kutaka kulazimisha swala tano mashuleni ikawa vita, vita kwelikweli waliotumwa wanaelekezwa wasirudi nyuma mpaka kieleweke!! wengine wakaambiwa ninyi mkienda kuswali wakristo wataendelea kusoma na ukimkuta mwalimu ameingia darasani usingie mpaka kipindi chake kiishe. wenye akili wakaona haina tija wakaacha.ambao hawakuchanganya na zao wakaendeleza madai mengine ikiwa ni pamoja na kujengewa misikiti shuleni!!! udini ukawa unashamiri.wakalazimisha waislamu watengewe mahali maalumu kwaajili ya ibada zao.AGENTS WA UDINI HAWAFAI,LAKINI WAPO SERIKALINI.
Kwa maoni yangu,watu waendelee kuwa na dini zao zozote wazitakazo lakini serikalini kusiwe na elementi yoyote inayo mtambulisha mtumishi wa umma au mwanafunzi kwa dini yake. wanaotaka kujipambanua kwa dini zao waende kufanyakazi kwenye madhehebu yao au dini zao vivyo hivyo kwa wanafunzi wote wanao soma shule za serikali sharti wafanane. Anae taka kuvaa msalaba aende shule za seminari,anae taka kuvaa hijabu na aende seminari za kiislamu.naona siku hizi kuna watu wanavaa baragashia na misalaba mikubwa kwenye ofisi za umma, ni mwanzo wa kubaguana kwa dini zetu na inawezekana na huduma kwa wateja zinatolewa kwa mtazamo huohuo. ni HATARI SANA KWA UMOJA WA TAIFA LETU.

Dini ya kislaam inaalaani ndoa za jinsia moja bt dini yako ww ukiwa shoga unahaki ya kuolewa na mwanaume mwenzako mwanamke akaolewa na mwanamke mwenzake dini ya kiislam imemtaka mwanamke ajistiri dini yako ww inataka mwanamke aoneshe utupu wake na ajidhalilishe mbele ya watu. Mkuu rudi shule
 
Mkuu, MG! Nikuunge mkono kwa pambio dogo!Kwa wale wanaoamini Mungu! "Baada ya Mungu kuumba Dunia ndipo alipomuweka mwanadamu na kumuwekea utaratibu wa kuishi humo!" Kwa maana kwamba UTAIFA (dunia) NI KITU CHA KWANZA na kitu cha pili DINI (Utaratibu wa kuishi ndani ya dunia) Na ndio sababu ukienda kuhiji maka au roma ukipitiliza siku moja tu lazima uwekwe lupango, kama Uislamu au Ukristo wako kafanyie kwenu hapa kwetu! Sivyo?Tufanye nini?1 Somo la uraia lifundishwe kuanzia kwenye familia majumbani! Na mtoto asiandikishwe darasa la kwanza kama hakufaulu hilo somo!2 Walimu wajuzi wa hilo somo ndio wafundishe tu, kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu!3 JKT Iboreshwe na kuwezeshwa kupokea na kuwanoa vijana wote wa umri utakaokubalika! Na iwekwe sheria kusimamia utekelezaji!4 Viongozi wote wa nchi pamoja na dini pawepo utaratibu wa kuwapiga msasa na kuwe na viwango maalum kwa ajili yao!......!Nchi yetu wote tuongeze maoni ili tuboreshe!
 
Kweli nimeamini kuwa humu JF kuna watu wa kila aina.wengine ndio kwanza wapo std 5.angalia huyu ni kama amelishwa maneno hajui anaongea nini. watanzania wana dini,lakina NCHI haina dini.VATICAN NI NCHI kwahiyo inahaki ya kuwa na balozi TANZANIA.OIC purely ni shirika la kidini.Endelea kujifunza kutoka GREAT THINKERS iko siku utajua kuto kuchanganya mambo kama ulivyo fanya leo.

Naongezea tu mkuu JERUSALEMU..Vatican ni nchi na ina kiti Umoja wa Mataifa...OIC ni shirika na sio mashirika yote tuna uhusiano nayo.
 
Dah kama ndo wewe great thinker basi dunia imeshaisha haya hiyo vatican unayosema ni nchi hebu ilocate ki geographier na unipe cabinet yake ya mawaziri pm bunge na kila kitu dah ww kweli kilaza tena mbumbumbu

siku ukisoma mwenyewe utajua kuwa ni Nchi.achana na mahubiri ya sheik wa kuchonga ponda.
 
Back
Top Bottom