Hakuna taifa linalotaka taifa jingine liwe na nguvu

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Isitokee hata siku moja tukafikiri watu kutoka nje watakuja kujenga umoja wetu na kuliletea maendeleo taifa letu, Kama tumeshindwa kujenga umoja wetu huku ndani, hakuna mtu, au taifa lolote litakuja kujenga umoja huo. Hakuna taifa litakalo kuja kujenga taifa letu na kulifanya liwe lenye nguvu. Ni sisi wenyewe kwa jitihada zetu.

Hakuna taifa jingine linapenda taifa jingine liwe na nguvu zaidi yao. Wanajua wakiliacha liwe hivyo ni hatari kwao na hivyo mataifa makubwa hufanya kila jitihada kuyashusha mataifa yanayoinukia kuwa yenye nguvu, hawataki mataifa hayo yawe na umoja. Wanawagawanya watu na kuwatawala.

Mataifa ya ulaya yanaposema yanasaidia mataifa ya afrika ili yaondoe umaskini ili wainukie kiuchumi na kielimu ni uongo mkuu. Wanapenda kuona watu wa mataifa haya madogo kuwa watu wasio na dira wala mwelekeo kwa mataifa yao. Watu wa mataifa haya madogo watakapoanza kupata akili lazima watajenga uadui na kupanga mapinduzi.

Ni nani awezaye kumpa mtu maarifa kuliko aliyonayo au kumfanya awe na nguvu kuliko alizonazo? Hata Mungu awezi kumpa maarifa na nguvu alizonazo binadamu.

Wanahitaji Afrika kibiashara tu na kwaajili wa malighafi. Wanapenda na wangependa afrika iendelee kuwa dhaifu na waendelee kuinyonya. Wanapenda na wangependa kuiona afrika tegemezi na sio afrika inayojitegemea ili waendelee kuitawala.

Kwahiyo mkae mkijua jukumu la kujenga taifa hili ili linyanyuke na liwe na nguvu duniani ni letu na kazi hiyo ni yetu sio ya taifa jingine lolote. Hakuna taifa lolote litakalo kupa uwelewa wa kulifanya taifa lako liwe lenye nguvu hizo ni jitihada tunazotakiwa kuzifanya wenyewe.

Kizazi hiki na kingine lazima kijue hili na hata tunapo deal nao tufahamu hivyo na tusijisahau. Tujue ulinzi wetu ni jukumu la wote na maendeleo yetu ni jukumu la kila mmoja wetu. Na tuhusiane nao kwa kutumia akili na hekima na kuwa na machale sio kuwaamini moja kwa moja. Kwasababu historia inaonyesha wazungu hawaaminiki hata unapowaamini.

Tunapaswa kujua malengo yetu na kujua kwamba hakuna taifa jingine lolote linalotaka taifa jingine liwe na nguvu zaidi na kupokea amri kutoka katika taifa jingine. Kila taifa linataka utukufu wa kuwa taifa kubwa na linaloheshimika.

Tunatakiwa tujiulize tumefanya nini toka ukoloni na utumwa mpaka sasa na tunafanya jitihada gani kujikomboa? Na hili ni jukumu letu la dhati tunatakiwa tuache uzembe.

Ni lini simba akataka swala awe na nguvu zaidi yake? atakula wapi?

Nguvu ni kitu ambacho tunatakiwa tukitafute wenyewe kwa jitihada zetu. Kama mnadhani ukoloni umeisha mnajidanganya.

Ni muhimu kuhakikisha kwamba tumesimama kama taifa na tuna nguvu kubwa ya kujilinda na kujenga uchumi imara unaojitegemea kwa kuwa na uwezo wa kuzalisha mkubwa.
 
Back
Top Bottom